Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,508
- 911,249
- Thread starter
- #9,921
Tenga ashukuru, aahidi makubwa Caf
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 4th March 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 40; Jumla ya maoni: 0
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Caf, Leodegar Tenga.
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono na wote waliofanikisha yeye kushinda Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Caf.
Wiki iliyopita Tenga alichaguliwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) baada ya kumshinda Celestine Musabiyima wa Rwanda aliyekuwa akitetea nafasi hiyo uchaguzi uliofanyika Khartoum, Sudan.
Akizungumza mjini Dar es Salaam, Tenga, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), alisema atatumia wadhifa huo kusaidia maendeleo ya soka kwa ukanda huu.
Pia alisema anaamini atashirikiana na viongozi wa kanda nyingine kuhakikisha kuwa soka la Afrika Mashariki linapiga hatua.
Aliishukuru TFF kwa kumdhamini agombee nafasi hiyo na kumuunga mkono na kuwashukuru Watanzania kwa kumfanikisha afikie hatua hiyo.
Alieleza changamoto mbalimbali ambazo zinamkabili, lakini aliahidi kwa kadri ya uwezo wake atahakikisha anapambana nazo na soka la Afrika Mashariki na Kati linasonga mbele.
Tenga anakuwa Mtanzania wa pili kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ya Caf baada ya Said Hamad El Maamry ambaye aliwahi kushinda nafasi hiyo mwanzoni mwa miaka ya 80 kwa vipindi viwili mfululizo.
Alishindwa kutetea nafasi hiyo katika kipindi cha tatu baada ya TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu (FAT) kutoidhinisha jina lake Caf.
El Maamry hivi sasa ni mjumbe wa heshima wa CAF.
Mtanzania mwingine aliyewahi kuwania nafasi hiyo mara mbili, lakini hakufanikiwa kushinda ni Muhidin Ndolanga ambaye aliwania wakati huo akiwa Mwenyekiti wa FAT.