Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
- #9,901
Linex awatamani Lady Jaydee, Kidumu
na Dina Ismail
MSANII wa muziki kizazi kipya nchini, Sunday Mangu, maarufu kama ‘Linex' amesema iwapo mambo yatakwenda vema anatarajia kuwashirikisha katika albamu yake ya pili wasanii maarufu ukanda wa Afrika Mashariki, Lady Jaydee, Kidumu na Radio, kutoka nchini Uganda.
Akizungumza hivi karibuni, mkali huyo alisema tayari ameishaanza matayarisho ya albamu yake hiyo na wakali hao ni miongoni mwa wasanii ambao atawashirikisha katika kazi zake.
"Nawazimia sana wasanii hawa na kama mambo yatakwenda vema, nitawashirikisha katika baadhi ya nyimbo zangu zitakazokuwemo katika albamu yangu ya pili, ikishindikana nitafanya hivyo hata wakati mwingine," alisema Linex.
Mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake ‘Moyo wa Subira', aliongeza kuwa mbali na nyota hao, pia ataifanyia matayarisho albamu yake katika studio tofauti ili kuifanya iwe na vionjo tofauti.
Msanii huyo ambaye albamu yake ya kwanza inajulikana kwa jina la ‘Mama Halima' huku ikibebwa na singo kadhaa ukiwemo uliobeba jina la albamu ‘Mama Halima', pia aliwahi kutoka na vibao kama ‘Top Up' sambamba na kushirikishwa na wasanii wengine.