Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,504
- 911,249
- Thread starter
- #9,081
Chaneta kukabidhiwa fedha za pongezi kesho
na Mwandishi wetu
MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Shy-Rose Bhanji kesho anatarajia kukabidhi kitita cha sh mil. 1.1 jijini Dar es Salaam kwa ajili ya timu nne zilizopanda daraja katika mashindano ya Ligi daraja la pili yaliyomalizika hivi karibuni Mjini Morogoro.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Kaimu Katibu Mkuu wa Chaneta, Rose Mkisi, alisema Bhanji ameamua kutoa fedha hizo ikiwa ni ishara ya kutambua juhudi zao na kuleta hamasa kwa timu nyingine kujituma kama hizo zilizopanda daraja.
Mkisi alisema Bhaji alitakiwa kuwa mgeni rasmi wa kufunga mashindano hayo lakini alishindwa kufika kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kazi badala yake aliwasiliana na viongozi na kutoa ahadi ya kutoa kiasi hicho cha fedha.
Alisema Mbeya iliyokuwa ya kwanza itapata sh 500,000, Polisi Arusha iliyoshika nafasi ya pili itapewa sh 300,000 huku timu za Polisi Pwani iliyoshika nafasi ya tatu na JKT Ruvu iliyokuwa ya nne kila mmoja atapata sh 200,000.
Aidha, Bhanji alitoa pongezi kwa timu zote zilizoshiriki mashindano hayo na kuahidi kutoa ushirikiano na kutambua mchango wao katika kuendeleza mchezo huo hapa nchini.
Mashindano hayo ya ligi daraja la pili yalianza kurindima mjini Morogoro, kuanzia Februari 16-Februari 26 ambapo Manispaa ya jiji la Mbeya wameibuka na ushindi wa mashindano hayo.

PRINT