Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Yanga watoa msaada Gongolamboto


Na Elizabeth Mayemba

WACHEZAJI wa Yanga, jana waliwakumbuka waathirika wa mabomu ya Gongolamboto, Dar es Salaam kwa kuwapelekea msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo
maji, sabuni na kalamu (peni).

Akikabidhi vifaa hivyo nahodha wa timu hiyo, Fredy Mbuna alisema wameguswa na tukio hilo la kuhuzunisha na ndiyo maana wakaona hawana budi kuwachangia kitu kidogo walichonacho kama wachezaji.

"Wakati janga hili linatokea tulikuwa Bukoba kwenye mchezo wetu na Kagera Sugar, hivyo tukaahidi kwamba tutakaporejea Dar es Salaam tutakuja kuwapa pole waathirika wa mabomu na kutoa kile tulichonacho kama wachezaji," alisema Mbuna.

Alisema siku zote wataendelea kuwakumbuka waathirika hao na wakipata chochote tena, hawatasita kwenda kuwasaidia.

Mbuna alisema kuwa hata mchezaji mwenzao, Godfrey Bonny ni mkazi wa Gongolamboto, hivyo endapo angekuwepo huenda adha hiyo ingemkuta.

Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo Mohammed Bhinda, alisema msaada huo ambao umetolewa ni wachezaji wenyewe ndiyo walioamua kufanya hivyo kwa jinsi walivyoguswa na janga hilo.

Alisema viongozi nao watapanga siku maalum kwa ajili ya kwenda kutoa pole kama walivyofanya wachezaji wao.

"Wachezaji wetu waliahidi kwamba wakitoka Bukoba watakwenda kuwapa pole waathirika wa mabomu na sisi tukawapa baraka zote, kwani kitendo walichokifanya ni cha ubinadamu," alisema Bhinda.
 
Samatta, Ulimwengu kuingoza Vijana Stars


Na Addolph Bruno

KIPA wa timu ya taifa 'Taifa Stars' na Mtibwa Sugar Shaabani Kado, Mbwana Samatha wa Simba na Thomas Ulimwengu anayecheza soka
Sweden wameitwa katika kikosi cha taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 23, 'Vijana Stars' ambacho kitaanza mazoezi leo.

Kikosi hicho hicho kinatarajia kushiriki mashindano ya Afrika ya kuwania kufuzu fainali za Olimpiki mwakani London, Uingereza.

Akizungumza kabla ya kutangaza kikosi hicho Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo 'Julio' alisema katika uteuzi huo wamezingatia zaidi uwezo wa mchezaji husika ambao wanacheza Ligi kuu na Ligi Daraja la Kwanza zilizomalizika juzi mkoani Tanga.

Alisema wengine wamechaguliwa kutoka katika mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu 'Uhai Cup', yaliyofanyika Dar es Salaam Januari mwaka huu.

Aliwataja wachezaji hao ni makipa Salehe Malande wa (TSA), Daud Gabriel (Azam FC), mabeki ni Hassan Kessy, Issa Rashid (Mtibwa Sugar) na Salumu Telela (Yanga).

Wengine ni mabeki Louis Tumba, Omary Mtaki (Azam FC), Zahoro Pazi (African Lyoni), Mbwana Hamis (Simba) na Babu Ally (Morani FC) huku viungo ni Ibrahim Juma, Himidi Mao na Salum Abubakar (Azam FC), Samweli Ngassa (African Lyon), Omega Seme (Yanga), Frank Domayo (JKT Ruvu) na Godfrey Innocent (Simba).

Wengine ni Jamal Mnyanje, Cosmas Freddy (Azam FC), Edward Shija (Simba), huku washambuliaji ni Benedict Ngassa (Moro United) na Atupele Green (Yanga).

Wakati huo huo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema kikosi hicho kitaingia kambini Jumamosi na kitacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kuondoka Machi 23 mwaka huu kwenda Younde, Cameroon kwa ajili ya mechi ya michuano hiyo itakayofanyika machi 26.
 
Vyama vyasuasua kujiandaa All Africa Game


Na Amina Athumani

VYAMA vya michezo nchini ambavyo vitashiriki mashindano ya mataifa ya Afrika 'All Afrika Game' bado inasuasua na maandalizi ya michuano
hiyo.

Akizungumza jana kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Henri Lihaya alisema wataviita vyama hivyo hivi karibuni ili kuzungumza navyo kwa ajili ya kujua michezo iliyopewa dhamana ya katika michuano hiyo.

"Tungekuwa tumeshakifanya kikao hicho, lakini kuna baadhi ya mambo yaliingiliana hapa katikati na ndiyo maana hadi leo hii, bado hatujakifanya lakini tutaviita vyama vyote vinavyotarajiwa kushiriki michuano hii hivi karibuni, ili kuongea navyo," alisema Lihaya.

Vyama vitakavyokwenda kushiriki michuano hiyo ni pamoja na Chama cha kuogelea Tanzania (TSA), Shirikisho la ngumi za Ridhaa (BFT), Chama cha Riadha (RT) na Chama cha Netiboli (CHANETA).

Michuano hiyo ya Afrika inatarajia kufanyika Maputo, Msumbiji mwishoni mwa mwaka huu.

 
Kado, Samatta kuifufua Vijana Stars
Imeandikwa na Zena Chande; Tarehe: 22nd February 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 184; Jumla ya maoni: 0








KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ‘Vijana Stars', Jamhuri Kihwelo ‘Julio', jana alitangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachojiandaa na mechi dhidi ya Cameroon kuwania kufuzu michuano ya Olimpiki itakayofanyika Uingereza mwakani.

Katika kikosi hicho, Julio amemwita kipa wa Mtibwa Sugar na timu ya Taifa, Taifa Stars, Shaaban Kado pamoja na mshambuliaji Mbwana Samatta wa Simba na kiungo Omega Seme wa Yanga.

Mara ya mwisho Vijana Stars ilishiriki mashindano kama hayo mwaka 1999 kuwania kucheza Olimpiki ya mwaka 2000 iliyofanyika Sydney, Australia, wakati wa utawala wa Chama cha Soka Tanzania (FAT-sasa TFF), ikiwa chini ya Mwenyekiti Muhidin Ndolanga, Katibu Mkuu, Ismail Rage, Makamu Mwenyekiti Subira Mambo (sasa marehemu) na Katibu Msaidizi Amin Bakhressa ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).

Timu hiyo katika hatua hiyo ya awali ilicheza na timu ya Taifa ya Ghana, ambapo mchezo wa kwanza uliofanyika mjini Acca, Ghana, Vijana Stars ilifungwa mabao 2-1 na ziliporudiana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam (sasa Uwanja wa Uhuru), Vijana Stars pia ilifungwa mabao 2-1 mgeni rasmi akiwa Frederick Sumaye wakati huo akiwa Waziri Mkuu.

Baadhi ya wachezaji waliokuwepo kwenye kikosi hicho cha mwisho cha Vijana Stars, ambao baadaye walikuja kung'ara na timu mbalimbali ni Renatus Njohole, Steven Mapunda, Athumani Machupa, Wilfred Kidau, Omari Kapilima, Ngawina Ngawina, Adinani Mohammed (sasa marehemu), Amani Simba, Abdallah Sabebe, Mnenge Suluja, Ally Mayay, Omary Tamba, Abuu Mkangwa, Victor Kilowoko.

Wengine ni Kelvin Mhagama, Lameck Sichula, Ephraim Makoye, Jumanne Sabula, Zuberi Katwila, Hussein Mataka, Paschal Tungaraza, Mtindi Ally, Kassim Issa na Athumani Machepe (sasa marehemu).

Tangu wakati huo Vijana Stars haikuwahi kucheza mashindano yoyote, badala yake TFF imekuwa ikitumia timu mbili za vijana ambazo ni ile ya chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), hivyo kuitwa kwa Vijana Stars baada ya miaka 12 ni hatua mpya katika maendeleo ya soka.

Kulingana na Ofisa Habari TFF, Boniface Wambura wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, alisema shirikisho hilo kwa kushirikiana na benchi la ufundi limepanga kuitafutia timu hiyo mechi mbili za kirafiki kabla ya kuikabili Cameroon.

Kwa upande wake akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Julio alisema kwa kushirikiana na kocha mwenzake Adolph Rishard wametafuta wachezaji hao ambao wanaamini watafanya vizuri na kwa vile wengi wao ni vijana, hakuna shaka kuwa ndio watakaounda timu ya taifa ya wakubwa siku zijazo.

"Tumemchagua Kado kwa sababu yuko chini ya miaka 23 na tunajua ni kipa mzuri na pia kocha Jan Poulsen anamtumia kwenye timu ya Taifa, lakini tunamuomba tumtumie kwetu," alisema.

Timu hiyo itacheza mechi ya kwanza dhidi ya Cameroon Machi 26 mjini Yaounde. Timu itaanza mazoezi leo kabla ya kuanza kambi rasmi Jumamosi.

Kikosi kamili kilichotangazwa na Julio na timu zao katika mabano ni makipa: Salehe Malande (TSA), Daudi Gabriel (Azam FC), Shaaban Kado (Mtibwa Sugar).

Mabeki wa pembeni: Salum Telela (Yanga), Hassan Kessy (Mtibwa/TSA), Issa Rashid (Mtibwa Sugar).

Mabeki wa Kati: Zahoro Pazi (African Lyon), Mbwana Hamisi (Simba), Louis Tumba, Omary Mtaki (Azam FC), Babu Ally (Morani).

Viungo: Godfrey Innocent (Simba), Ibrahim Juma, Himid Mao, Salum Abubakar (Azam FC), Frank Damayo (JKT Ruvu), Samwel Ngasa (African Lyon). Wengine ni Jamal Mnyate, Cosmas Freddy (Azam FC), Edward Shija (Simba).

Washambuliaji: Benedict Ngasa (Moro United), Atupele Green (Yanga), Samatta (Simba) na Thomas Ulimwengu.

 
Mahanga aifagilia Moro United kupanda daraja
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd February 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 63; Jumla ya maoni: 0








MBUNGE wa Segerea, Dk. Milton Mahanga, ameipongeza timu ya soka ya Moro United kwa kufanikiwa kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mahanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, amesema amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na mafanikio ya Moro United ambayo ilishika nafasi ya tatu katika fainali za ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora zilizomalizika juzi Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

"Hii ni mara ya kwanza katika historia ya jimbo la Segerea na kabla ya hapo Ukonga ambalo liligawanywa na kupatikana hili la Segerea kuwa na timu kwenye Ligi Kuu.

"Nawapongeza wachezaji, viongozi na wadau wenzangu wa Tabata ambao kwa namna mbalimbali tulishirikiana kuhakikisha timu yetu inapanda daraja.

"Tuliinunua timu hii na kufanya maandalizi katika kipindi kigumu, lakini juhudi zetu zimezaa matunda, hivyo nawaomba ndugu zangu wote wa Segerea na Tabata tuhakikishe tunashirikiana kwenye maandalizi ya Ligi Kuu msimu ujao," alisema Mahanga.

Alieleza kuwa yeye hakutaka kusubiri mpaka timu ipande ndipo atoe ushirikiano ama asubiri
kupongeza, badala yake alifanya hivyo kuanzia hatua ya kwanza kwani timu hiyo ni ya wana-Segerea wote.

Juzi Moro United ilikamilisha orodha ya timu nne zitakazocheza Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara zikitoka ligi daraja la kwanza baada ya kuifunga Morani mabao 2-1.

Moro United iliungana na JKT Oljoro, Coastal Union na Villa Squad ambazo zilijihakikishia
kupata nafasi ya kupanda daraja kabla ya Februari 21.

Wakati huo huo, Dk. Mahanga alisema kuwa wameanza mchakato wa kubadili jina la timu hiyo kutoka Moro United na kuwa Tabata FC ambalo ni jina la timu ya wadau wa Tabata.

Alisema wana matumaini makubwa kwamba mchakato wao utakuwa wa manufaa na timu hiyo itashiriki vyema Ligi Kuu. Moro United ilishuka daraja msimu wa mwaka 2009/2010.
 
Kanumba: Wasanii si chanzo kuporomoka maadili
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd February 2011 @ 23:45 Imesomwa na watu: 27; Jumla ya maoni: 0








MUIGIZAJI maarufu wa filamu nchini Steven Kanumba amesema wasanii si chanzo cha kuporomoka maadili katika jamii bali tatizo hili linasababishwa kwa kiasi kikubwa na utandawazi unaoambatana na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Akiwasilisha mada kuhusu Harakati za kuivusha tasnia ya filamu katika ngazi za kimataifa
kwenye Jukwaa la Sanaa juzi kwenye ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Kanumba alipuuza malalamiko kwamba, wasanii wa filamu wamekuwa chanzo cha kuipotosha jamii kupitia yale wanayoyaigiza.

Badala yake alisema malezi na utandawazi ni tatizo kubwa kwa sasa katika taifa na wazazi hawana budi kudhibiti watoto wao ili kuwaepusha na wimbi hilo.

"Maadili hayako katika filamu tu, tunapozungumzia maadili ni katika nyanja nyingi.

Leo mtoto mwenye miaka tisa anamiliki simu tena yenye intaneti, humo anaangalia facebook na picha za ajabu halafu mtoto huyu akiharibika watu wanasema ni filamu, hii si kweli, " alisisitiza Kanumba.

Alisema kwa kawaida wanapoandaa filamu wamekuwa wakiandika umri wa watazamaji wake, lakini wazazi wengi wamekuwa wakipuuza na kuwaacha watoto kuangalia filamu ambazo hawapaswi kuangalia.

Alitaja filamu kama ya This Is It ambayo anasema kuna watoto hawaruhusiwi kuiangalia
lakini wazazi na walezi wengi wanapuuza hilo.

"Filamu zetu tunazotengeneza zinakuwa na ujumbe kwa jamii, zinabeba masuala yaliyomo ndani ya jamii. Suala la nani aangalie kilichomo tumekuwa tukiziwekea umri wa watazamaji.

Naomba mniambie jamani hayo tunayoyaonyesha katika filamu yetu hayapo katika jamii? Alihoji Kanumba.

Juu ya wizi katika kazi zao, Kanumba alisema kwamba Chama cha Hakimiliki (Cosota) kimekuwa kikijitahidi lakini tatizo limekuwa kwenye nguvukazi ya mamlaka hiyo lakini pia sheria ambazo zinaonekana hazikidhi matakwa.

Hata hivyo, akizungumzia hilo kwa niaba ya Cosota, Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche

Materego alisema kwamba, sheria mpya za hakimiliki ziko katika kiwango cha kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa na uwezekano mkubwa ni kwenye bunge la Aprili.
 
Polisi, Hamambe moto netiboli
Imeandikwa na John Nditi, Morogoro; Tarehe: 22nd February 2011 @ 23:40 Imesomwa na watu: 16; Jumla ya maoni: 0








KINYANG'ANYIRO cha ligi ya netiboli daraja la pili hatua ya fainali kiliendelea jana Uwanja wa Jamhuri mjini hapa, huku timu za Ruvu JKT, Alliance One, Polisi Pwani na Hamambe ya Jiji la Mbeya zikiibuka videdea dhidi ya wapinzani wao.

Timu hizo zilipata ushindi kwenye michezo iliyofanyika jana asubuhi, ambapo JKT Ruvu ya
Pwani ilifuta unyonge wao pamoja na kukosekana mshambuliaji wake mahiri, Jawa Hassan aliyeumia mkono na kuukosa mchezo huo ulioifanya timu yake kuishinda Ruangwa ya Lindi mabao 34-25.

Mchezo mwingine wa kuvutia ulikuwa kati ya Alliance One ya mjini hapa na Tigo ya Dar es Salaam, ambapo wenyeji walishinda kwa mabao 26-16 na katika michezo iliyofuatiwa, Hamambe ya Mbeya iliishinda Polisi Arusha mabao 34- 13 .

Hata hiyo wakati Polisi Arusha wakipoteza mchezo wao, Polisi Pwani waliendeleza wimbi la
ushindi baada ya kuibuka kidedea kwa kuifunga Tandahimba ya Mtwara mabao 25-13.

Katika michezo iliyofanyika juzi jioni JKT Ruvu ililala kwa mabao 16-11 mbele ya Polisi Pwani.
Michezo mingine juzi jioni Hamambe ya Mbeya iliifunga Ruangwa ya Lindi kwa mabao 39 -15 .

Timu ya Tigo kutoka jijini Dar es Salaam, iliendelea kugawa pointi baada ya kufungwa na Polisi Arusha mabao 27-14, ambapo Alliance One iliifunga Tandahimba mabao 34-15.

Akizungumza na viongozi wa timu zinazoshiriki ligi hiyo baada ya michuano hiyo juzi jioni, Mkufunzi Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania ( Chaneta), Mary Protas , aliwataka viongozi hao kuendeleza utulivu katika mashindano hayo kwa kusisitiza suala la nidhamu kwa wachezaji wao.
 
‘Wasanii wasaidie waathirika wa mabomu'
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd February 2011 @ 23:30 Imesomwa na watu: 14; Jumla ya maoni: 0








WASANII nchini wameombwa kushirikiana na jamii kusaidia waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea Gongo la Mboto, Dar es Salaam wiki iliyopita.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama amesema Dar es Salaam kuwa kuna haja ya wasanii kushirikiana na wadau wengine katika kusaidia waathirika hao.

"Mimi na Kamati yangu tayari Jumamosi tulikabidhi mchango wetu, naomba na wengine nao wafanye hivyo," alisema.

Kulingana na taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mwenyekiti huyo alisema amepokea simu kutoka kwa watu mbalimbali wakiipongeza kamati yake kwa kuonesha moyo wa kiungwana.

Aliwataja baadhi ya walioipongeza Kamati yake kuwa ni Sheikh Mkuu wa Tanzania, Muft Issa Shaaban Simba na aliyekuwa Katibu wake wa zamani, Sheikh Abdul Shakulu.

"Tunapopatwa na majanga kama haya, ni jukumu letu wote kujitokeza kwa wingi kusaidiana bila kujali tofauti za kiitikadi, kidini wala kabila," alisema Msama akimnukuu Sheikh Simba.

Jumamosi Kampuni ya Msama Promotions inayoandaa tamasha la Pasaka ilikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa waathirika wa milipuko hiyo vyenye thamani ya Sh milioni 3.
 
Man. United kuwakosa saba Ulaya leo Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 20:36

PARIS, Ufaransa
MANCHESTER United itaingia Stade Velodrome, Ufaransa kucheza na Olimpique Marseille bila ya nyota wake saba ambao ni majeruhi na hawakusafiri na timu hiyo huko.

Mbali na mchezo huo, Inter Milan itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wake wa San Siro kuwakaribisha Bayern Munich katika mechi nyingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua hiyo ya 16 bora.

Manchester imesafiri bila ya mkongwe wake, Ryan Giggs na Anderson pamoja na Jonny Evans, Rio Ferdinand, Michael Owen, Ji-sung Park na Antonio Valencia ambaye kwa muda mrefu amekuwa nje ya dimba.

Kocha wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson alikuwa na wakati mgumu jana wakati akizngumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano kabla ya mchezo huo dhidi ya Marseille.

Kipa wa timu hiyo, Anders Lindegaard amesafiri na timu hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza licha ya kuwa mkongwe, Edwin van der Sar anatarajia kusimama langoni baada ya kupumzishwa katika mechi ya FA dhidi ya Crawley Town.

Katika kikosi hicho wamo 'madogo' Joshua King na kiungo Ryan Tunnicliffe. Vijana hao waliisaidia timu yao kuingia nusu fainali ya Kombe la FA, na walisajiliwa na timu hiyo Ijumaa.

Marseille moja ya timu zisizotabirika, kwa upande wake, itamkosa Andre-Pierre Gignac aliyeumia nyonga katika mechi ya ligi waliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya St Etienne.

Mshambuliaji mwenzake, Brandao na Loic Remy wanasumbuliwa na magoti lakini kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps alisema kuwa wanaweza kuwa fiti kuikabili United.

Hata hivyo, Deschamps alisema kuwa hana wasiwasi na wachezaji wake waliosalia: ìHii si mara ya kwanza kucheza na Manchester United."

ìCha msingi ni kuangalia matokeo ya mwisho, na kikubwa ni kwamba tumefuzu hatua ya 16 bora.î Manchester United itakuwa ikimtarajia Rooney katika safu ya ushambuliaji kuwapa mabao timu hiyo.

ìNimekuwa nikiangalia mechi za Marseille kila wakati, ninachokiona ni kwamba wachezaji wake si wakutisha sana, lakini wamekuwa wakiungwa mkono sana na mashabiki,î Ferguson aliwaambia waandishi wa habari. "Haitakuwa rahisi, lakini tutajitahidi tufuzu."

Timu zaweza kupangwa hivi: Olympique Marseille: 30-Steve Mandanda; 12-Charles Kabore, 21-Souleymane Diawara, 19-Gabriel Heinze, 3-Taye Taiwo; 8-Lucho Gonzalez, 6-Edouard Cisse, 7-Benoit Cheyrou; 20-Andre Ayew, 11-Loic Remy, 9-Brandao

Manchester United: 1-Edwin van der Sar; 22-John OíShea, 15-Nemanja Vidic, 12-Chris Smalling, 3-Patrice Evra; 24-Darren Fletcher, 18-Paul Scholes, 11-Ryan Giggs, 17-Nani; 10-Wayne Rooney, 9-Dimitar Berbatov
 
Blackpool 3-1 Tottenham


FOX Soccer.com



PRINT RSS

79 comments »

Updated Feb 22, 2011 6:30 PM ET
Blackpool pulled off an impressive 3-1 home win over Tottenham on Tuesday to move five points clear of the Premier League relegation zone.
Seasiders captain Charlie Adam - who so nearly joined Spurs in January - opened the scoring at Bloomfield Road with a firm penalty in the 18th minute after Sebastien Bassong had fouled DJ Campbell in the box.
Campbell then netted his ninth goal of the season a minute before the interval by connecting with James Beattie's cross before substitute Brett Ormerod netted a third with 10 minutes of normal time remaining, rendering Roman Pavlyuchenko's effort at the death a mere consolation.

Sun., Feb. 20
West Brom 1-1 Wolves | Recap
Tue., Feb. 22
Blackpool 3-1 Tottenham | Recap
Wed., Feb. 23
Arsenal vs. Stoke City
Sat., Feb. 26
Aston Villa vs. Blackburn
Everton vs. Sunderland
Newcastle vs. Bolton
Wigan vs. Man Utd
Wolves vs. Blackpool
BPL Scores | Table | Fixtures


The win was remarkable not only in that in brought Tottenham back down to earth after their famous Champions League win at AC Milan last week, but also because the visitors had numerous opportunities to score throughout the 90 minutes.
A couple of goal-line clearances and some superb saves by goalkeeper Richard Kingson kept Spurs out until just before the final whistle, though, as the Seasiders secured three vital points that move them up to 12th in the table.
Blackpool created the game's first goalscoring opportunity in the fourth minute when Adam won a free-kick and lofted it on to the head of Ian Evatt, who headed wide.
At the other end, Jermain Defoe was crowded out as he attempted to get a shot away and the ball went behind for a corner, which was swung in by Steven Pienaar.
Kingson met it with a less-than-convincing punch and Pienaar picked up possession, but after dancing along the edge of the box, he scuffed his shot over.
Pavlyuchenko was next to try an ambitious effort that went wide by some distance, but having soaked up the pressure, Blackpool hit back to take the lead.
Bassong wrapped his leg around Campbell as the striker ran across the box and after referee Chris Foy pointed to the penalty spot, Adam rifled the ball home beyond the diving grasp of Heurelho Gomes.
Tottenham had a chance to level things just before the half-hour mark as Pavlyuchenko laid a pass to Pienaar in the area, but the South African's shot was blocked by Craig Cathcart.
Adam then blasted the loose ball over his own bar off Pienaar as the hosts clung on to their advantage.
Spurs went even closer soon after as Defoe clipped the ball over Kingson towards goal, but Cathcart was again on hand to avert the danger with an excellent header off the line.
Adam then wastefully sliced a free-kick off target and Aaron Lennon's touch let him down after he was fed by Wilson Palacios.
An uncertain moment from Kingson led to Blackpool making another goal-line clearance towards the end of the half, this time Alex Baptiste the man to deny Defoe.

The home of the best LIVE soccer and rugby awaits at FoxSoccer.tv -- don't miss a second of the action.

But having almost managed to grab an equaliser, Spurs suddenly found themselves 2-0 down just before the break.
Beattie collected debutant Sergei Kornilenko's back-heel and chipped the ball to Campbell at the far post, who gleefully tucked it away.
Campbell looked as if he might have been offside as he finished, but the effort stood and Blackpool were firmly in the driving seat.
Spurs boss Harry Redknapp brought Jermaine Jenas on for Palacios at the break and Spurs looked to exert some pressure from the word go at the start of the second half, with Pienaar sending a shot wide.
Campbell called Gomes into action moments later, but Tottenham were soon on the front foot again, with Jenas striking off target and Kingson doing well to save a header from Pavlyuchenko.
Luka Modric hit an effort over at the end of a nice passing move and Pavlyuchenko sent another attempt over, but having weathered the storm, Blackpool almost made it 3-0 as Adam unleashed a low drive that went just the wrong side of the post.
Back came Spurs and after William Gallas had blazed over, the visitors were twice inches away from making a breakthrough.
First Pavlyuchenko was unable to get on the end of Defoe's cross and then Lennon was too late to slide in the pass returned across the box by Niko Kranjcar, on as a substitute for Pienaar.
Kingson then pulled off a fantastic point-blank save to keep Pavlyuchenko's header out.
Blackpool's goal seemed to be leading a charmed life and they somehow managed to keep Spurs at bay again in the 72nd minute as Modric dinked the ball over Kingson but Baptiste intervened before it could cross the line.
Crouch, who had also come off the bench, then flashed a header wide but Spurs' luck appeared to be out and in the 80th minute, the Seasiders struck again.
It was two of their substitutes who combined to make the goal as Matt Phillips broke into the box, Benoit Assou-Ekotto got muddled as he attempted to make a challenge and the ball broke to Ormerod, who slotted past Gomes.
Pavlyuchenko managed to loop in a shot in stoppage time but it counted for little.
 
Moro United yafanya kweli
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Tanga; Tarehe: 22nd February 2011 @ 10:42 Imesomwa na watu: 218; Jumla ya maoni: 0






TIMU ya Moro United imekamilisha orodha ya timu nne zitakazocheza Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara zikitoka ligi daraja la kwanza baada ya kuifunga Morani mabao 2-1.

Moro United sasa inaungana na JKT Oljoro, Coastal Union na Villa Squad ambazo ndizo timu nne bora katika fainali za ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora ambayo karibu wiki tatu ilikuwa ikitimua vumbi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kumalizika jana.

Tofauti na wengi walivyodhania kwamba Morani ambayo inashika mkia kwenye ligi hiyo iliyoshirikisha timu tisa ikiwa na pointi moja ingeonesha mchezo dhaifu, lakini hali ikuwa tofauti na iliwabana vilivyo Moro United.

Bao la kwanza la Moro United lilifungwa dakika ya nne na Samuel Samuel kwa mkwaju wa penalti, baada ya Fred Kahonga kuangushwa ndani ya eneo la hatari, kabla ya Morani kusawazisha dakika ya 43 mfungaji akiwa Hassan Kodo.

Moro United ilifunga bao la pili dakika ya 77 mfungaji akiwa Bakari Mpakala baada ya beki wa Morani Rashid Yusuph kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Kutokana na matokeo hayo Moro United imefikisha pointi 13 na inashika nafasi ya tatu nyuma ya JKT Oljoro inayoongoza ikiwa na pointi 15 na Coastal Union yenye pointi 14, wakati Villa Squad inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 12.

Kulingana na kanuni za ligi hiyo msimu huu timu nne za juu zinapanda daraja na kabla ya mchezo wa Moro United jana, tayari timu nyingine tatu za kupanda zilikuwa zimefahamika.

Timu nyingine zilizoshiriki ligi hiyo ni Rhino ya Tabora iliyoshika nafasi ya sita ikiwa na pointi 11, Prisons ya Mbeya nafasi ya saba ikiwa na pointi tisa, TMK United nafasi ya nane ikiwa na pointi saba na Morani nafasi ya mwisho ikiwa na pointi moja.

Katika mchezo wa awali jana Coastal Union na TMK United zilifungana bao 1-1.


 
Toto waikaribisha Mtibwa Kirumba Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 20:35

Vicky Kimaro
WAKATI timu ya soka ya Azam ikiendelea kuongoza Ligi Kuu ikiwa na ponti 35, ligi hiyo inendelea kutimua vumbi leo kwenye viwanja vitatu tofauti ikiwa ni hatua ya lala salama.

Toto African ambayo inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi, itawakaribisha Mtibwa Sugar ambayo ipo nafasi ya nne katika msimamo ikiwa na pointi 27, mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mechi nyingine itakayo pigwa leo ni kati ya African Lyon dhidi ya Ruvu Shooting ambayo ipo nafasi ya tisa ikiwa na ponti 14 na imekwishacheza mechi 15.

Vibonde wa Ligi Kuu msimu huu, Polisi Dodoma ambayo inashika nafasi ya tatu kutoka chini, itawakaribisha Kagera Sugar, mchezo utakofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Hata hivyo, kocha mkuu wa Polisi Dodoma John Simkoko alisema timu yake ipo tayari kwa mchezo huo ambao ameupa umuhimu mkubwa ili aweze kujiweka katika mazingira mazuri ya kuepukana na balaa la kushuka daraja.

Mechi hizo za lala salama ni vita ya kufa na kupona kwa kila timu ambayo inajitahidi kujinasua kushuka daraja lakini AFC na Majimaji zipo kwenye hatari zaidi ya kushuka kutokana na kushika mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo inayomalizika Aprili 10.
 
Wanaowania tuzo za Kilimanjaro watajwa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd February 2011 @ 09:42 Imesomwa na watu: 110; Jumla ya maoni: 0








KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imetangaza wateule watakaowania tuzo za muziki za Kilimanjaro, wasanii, 20% na Linah wanaongoza baada ya kupendekezwa katika vipengele vitano.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ndio waratibu wa tuzo hizo, George Kavishe alisema wateule hao waliteuliwa kwenye academy iliyofanyika wiki iliyopita.

Msanii 20% ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo zake za Tamaa Mbaya na Ya Nini Malumbano ameteuliwa kwenye tuzo ya Msanii Bora wa kiume pamoja na Ali Kiba, Barnaba, Diamond, AY na Belle 9.

Aidha msanii huyo pia ameteuliwa kwenye tuzo ya Mwimbaji Bora wa kiume pamoja na Barnaba, Ali Kiba, Banana Zorro, Belle 9 na Diamond.

20% ambaye anatamba pia na filamu yake ya Furaha Iko Wapi, ameteuliwa tena kuwania tuzo ya Wimbo bora wa mwaka kupitia wimbo wake wa Ya Nini Malumbano na Tamaa Mbaya.

Wengine wanaowania tuzo hiyo na nyimbo zao zinazoshindanishwa zikiwa kwenye mabano ni Gelly wa Rymes Feat. AT, Ray C (Mama Ntilie), Sam wa Ukweli (Sina Raha), Chege, Temba Feat Wahu (Mkono Mmoja) na Tip Top Connection (Bado Tunapanda).

20% pia ameteuliwa kuwania tuzo ya Mtunzi Bora wa nyimbo ambapo anawania pamoja na Barnaba, Lady Jay Dee, Mrisho Mpoto na Mzee Yusuph. Tuzo nyingine anayowania ni ya wimbo wa Afro Pop kupitia nyimbo zake za Ya nini Malumbano na Tamaa Mbaya.

Wengine ni Gelly wa Rymes feat AT, Ray C (Mama Ntilie), Bon Junior (Oyoyo) na Diamond (Mbagala).

Kwa upande wa Linah ambaye ni zao la THT ameteuliwa kuwania tuzo ya Msanii Bora wa kike wa muziki pamoja na Lady Jay Dee, Mwasiti, Shah na malkia wa mipasho, Khadija Kopa.

Wasanii haohao pia wameteuliwa kwania tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike. Linah pia anawania tuzo ya wimbo bora wa R&B kupitia wimbo wake wa Atatamani ambapo katika kipengele hiki anawania na Belle 9 (We ni Wangu), Ben Poul (Nikikupata), Hussein Machozi Feat Maunda Zorro (Hello) na Z- Anto kupitia wimbo wake wa Kisiwa cha Malavidavi.

Kpengele kingine anachowania Linah ni tuzo ya msanii anayechipukia ambapo atapambana na Sam wa Ukweli, Sajna anayetamba na wimbo wake wa Iveta, Bob Junior anayetamba na wimbo wa Oyoyo na Top C anayetamba na wimbo wa Lofa.

Pia Linah anawania tuzo ya wimbo bora wa zouk kupitia wimbo wake wa Bora Nikimbie akishindana na Sam wa Ukweli (Sina raha), Top C (Lofa), Barnaba (Nabembelezwa) na Amini (Robo Saa).

Kwa upande wa wimbo bora wa taarab, nyimbo zinazowania tuzo ni My Valentine (Jahazi), Top In Town (Khadija Kopa), Acheni Kuniandama (Isha Ramadhani ‘Mashauzi'), Langu Rohoni (Jahazi) na Mama Nile Radhi wa Isha Mashauzi.

Aidha wimbo bora wa Kiswahili (bendi) zitakazowania tuzo ni Shika Ushikapo (Mapacha watatu), Laptop (Extra Bongo), Kauli, Mapenzi Hayana Kiapo (Twanga Pepeta) na Pongezi Kwa Wanandoa (Akudo) huku kwa upande wa repa bora wa mwaka wakishindanishwa Saulo Ferguson wa Extra Bongo, Khalid Chokoraa wa mapacha watatu, Totoo za bingwa wa Akudo na Kitokololo wa FC Academia.

Kwa mujibu wa Kavishe, kura zitaanza kupigwa Machi mosi mpaka Machi 22 kabla ya kufanyika kwa fainali za tuzo hizo Machi 26.
 
Ligi ya Taifa yashika kasi Geita
Imeandikwa na David Azaria, Geita; Tarehe: 22nd February 2011 @ 09:42 Imesomwa na watu: 42; Jumla ya maoni: 0








MICHUANO ya soka Ligi ya Taifa ngazi ya Mkoa wa Mwanza kituo cha Geita imeanza kwa kasi baada ya timu ya Nyanza FC ya Geita kuifunga Geita Veterani kwa Mabao 2-1.

Geita Veterani walianza mchezo kwa kasi baada ya kufanya mashambulizi ya kushitukiza langoni mwa Nyanza dakika za 7,8,11 na 16, lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Karume Songoro walishindwa kutumbukiza mipira ndani ya nyavu za Nyanza.

Baada ya kushambuliwa kwa muda mrefu Nyanza waliigeuzia kibao Geita veterani na kufanya shambulizi la kushitukiza, ambapo ilijipatia bao kupitia kwa Baraka Jibson.

Baraka alifunga bao hilo baada ya kupata mpira mrefu uliopigwa na kipa wake na baada ya kuunasa huku mabeki wa Geita veterani wakidhani ameotea alichomoka kwa kasi na kumzunguka beki wa Veterani na kisha kutumbukiza mpira kimiani.

Pamoja na kupata bao hilo Nyanza walishindwa kutulia uwanjani na kufanya mashambulizi ya uhakika langoni mwa Veterani, hali iliyowapa mwanya washambuliaji wa Veterani kuingia ndani ya lango lao, lakini wakashindwa kufunga na kuifanya Nyanza kwenda mapumziko ikiongoza bao 1-0.

Kipindi cha pili Geita Veterani waliingia uwanjani kwa kasi kutaka kusawazisha bao, lakini walijikuta wakifungwa la pili dakika ya 52 mfungaji akiwa Mohamed Salum.

Dakika ya 75 Geita Veterani walipata bao lililofungwa na Shekilango Mkwizu ambaye aliuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Nyanza.
 
Watoto kushindana katika soka, netiboli

Imeandikwa na David Azaria, Geita; Tarehe: 22nd February 2011 @ 09:42 Imesomwa na watu: 28; Jumla ya maoni: 0








HALMASHAURI ya wilaya ya Geita Geita imeanzisha mashindano ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 14 wa shule za msingi watakaounda timu ya watoto ya wilaya.

Tayari mashindano hayo yameanza kuchezwa mpira wa miguu upande wa wavulana na netiboli kwa wasichana, ambapo michezo hiyo inafanyika kwenye Uwanja wa CCM Katoro wilayani hapa.

Akizungumza na HabariLeo, Ofisa Michezo wa wilaya ya Geita, Mary Mpemba alisema timu za watoto wa shule za msingi wenye umri wa chini ya miaka 14 kata za Katoro na Kalangalala walicheza michezo ya kirafiki ya kupimana nguvu ili kuunda timu ya wilaya.

Alisema, shule za msingi 12 kutoka kata za Katoro na Kalangalala zilishiriki mashindano hayo kwa kuunda timu mbili, moja kutoka shule za kata ya Katoro (timu ya Kombaini Katoro) na kata ya Kalangalala (timu ya Kombaini Kalangalala).

Katika mashindano ya michezo hiyo kwa upande wa netiboli timu ya Kombaini ya Katoro ilipata ushindi baada ya kuifunga Kombaini ya watoto wa Kalangalala kwa mabao 5-3.

Kwa upande wa mpira wa miguu Katoro ilitoka kifua mbele kwa kuitandika Kalangalala mabao 3-2.

Akizungumzia michezo hiyo kwa ujumla, ofisa huyo alisema mpango huo wa kukuza vipaji utakuwa endelevu kwa kuanzia ngazi ya watoto ili kupata vipaji halisi.
 
Kayuni: Mfahamu Ligi Kuu si lelemama Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 20:34

Burhani Yakub, Tanga
MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Sunday Kayuni amesema Ligi Daraja la Kwanza imemalizika mapema ili kuziwezesha timu zilizofuzu kujiandaa kikamilifi na michunao ya ligi kuu msimu ujao.

Alisema hayo kwenye Uwanja wa Mkwakwani juzi wakati wa kukabidhi zawadi kwa timu nne zilizoingia Ligi Kuu msimu ujao mara baada ya kumalizika hatua ya tisa bora.

"Tumechezesha mapema ligi hii kwa makusudi ili kuzipa muda wa kutosha kujiandaa kikamilifu na Ligi Kuu msimu ujao kwani huko si lelemama"alisema Kayuni.

Timu zilizoingia Ligi Kuu baada ya kufuzu Ligi Daraja la Kwanza ni Oljoro JKT ya Arusha, Coastal Union ya Tanga, Moro United na Villa Squard za jijini Dar es salaam.

Alisema TFF imedhamiria kuendesha ligi yenye ushindani mwakani na kuzitaka timu kufuata taratibu kwani haitakubali ubabaishaji kuanzia hatua ya usajili hadi ushiriki wa timu.

Naye Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini, Profesa maji marefu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi alizipongeza timu zilizofuzu kuingia Ligi Kuu na kuzitaka kuanza maandalizi mapema.

Aliahidi kuisaidia Coastal Union ili iweze kuwa timu bora katika ligi kuu kama ilivyokuwa miaka ya 1980 ili kuleta ushindani wa kweli katika mchezo wa soka nchini.

Naye Calvin Kiwia anaripoti kuwa TFF imezipongeza timu nne zilizofanikiwa kupanda daraja na kushiriki Ligi Kuu msimu wa 2011/12 na kuzitaka kuanza maandalizi mapema kwa lengo la kuleta ushindani kwenye Ligi hiyo.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema ni mategemeo la shirikisho hilo zimepata nafasi hiyo kwa uhalali na si kubebwa na waamuzi hivyo zitatoa changamoto kwenye ligi.

"Tunaamini kuwa nafasi hizo wamezipata kwa uhalali kushiriki na si kubebwa na waamuzi hivyo tunategemea zitaleta ushindani mkubwa kwenye ligi kuu itakayoanza Agosti ," alisema Wambura
 
Watoto kushindana katika soka, netiboli
Imeandikwa na David Azaria, Geita; Tarehe: 22nd February 2011 @ 09:42 Imesomwa na watu: 28; Jumla ya maoni: 0








HALMASHAURI ya wilaya ya Geita Geita imeanzisha mashindano ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 14 wa shule za msingi watakaounda timu ya watoto ya wilaya.

Tayari mashindano hayo yameanza kuchezwa mpira wa miguu upande wa wavulana na netiboli kwa wasichana, ambapo michezo hiyo inafanyika kwenye Uwanja wa CCM Katoro wilayani hapa.

Akizungumza na HabariLeo, Ofisa Michezo wa wilaya ya Geita, Mary Mpemba alisema timu za watoto wa shule za msingi wenye umri wa chini ya miaka 14 kata za Katoro na Kalangalala walicheza michezo ya kirafiki ya kupimana nguvu ili kuunda timu ya wilaya.

Alisema, shule za msingi 12 kutoka kata za Katoro na Kalangalala zilishiriki mashindano hayo kwa kuunda timu mbili, moja kutoka shule za kata ya Katoro (timu ya Kombaini Katoro) na kata ya Kalangalala (timu ya Kombaini Kalangalala).

Katika mashindano ya michezo hiyo kwa upande wa netiboli timu ya Kombaini ya Katoro ilipata ushindi baada ya kuifunga Kombaini ya watoto wa Kalangalala kwa mabao 5-3.

Kwa upande wa mpira wa miguu Katoro ilitoka kifua mbele kwa kuitandika Kalangalala mabao 3-2.

Akizungumzia michezo hiyo kwa ujumla, ofisa huyo alisema mpango huo wa kukuza vipaji utakuwa endelevu kwa kuanzia ngazi ya watoto ili kupata vipaji halisi.
 
Simba Queens yaiparua TMK Queens Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 20:33

Salome Millinga
TIMU ya soka ya Simba Queens imeichapa Temeke Queens mabao 2-1 katika mpambano wa Ligi ya soka ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali, Simba Queens walianza kutikisa nyavu za wapinzani wao dakika 35 kwa bao maridadi lililowekwa kimiani na kiungo wake, Angela John wakati lile la pili lilipachikwa na Fatuma Abushiri dakika 45.

Kipindi cha pili kilianza taratibu huku timu zote zikionekana kucheza kwa tahadhari lakini walikuwa Temeke Queens walioamsha vicheko kwa mashabiki wao pale, Happy Henzero alipopachika bao dakika ya 57 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Simba Queens.

Baada ya bao hilo, Temeke waliongeza kasi na kuzidi kuliandama lango la Simba Queens lakini ngome yake iliyokuwa inaongozwa na Fatuma Bushiri ilikuwa makini kuondoa hatari zote na kufanya hadi mwisho wa mchezo timu hizo kuifungana mabao 2-1.

Kocha mkuu wa Simba Queens, Anthony Makunja alisema baada ya mchezo huo kuwa walistahili kupata ushindi huo kwa vile vijana wake walijituma ingawa pia kuna wakati walifanya makosa madogo madogo.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom