Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
- #8,041
Mkutano Mkuu wa CAF waanza Sudan Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 20:31
KHARTOUM, Sudan
MKUTANO mkuu wa 33 wa Shirikisho la soka Afrika, CAF, unaanza leo kwenye mji wa Khartoum nchini Sudan huku ukishirikisha viongozi mbalimbali wa vyama vya michezo kutoka kila kona ya Afrika.
Mkutano huo ni mkutano halali wa CAF, ambao pia utapitia taarifa ya fedha pamoja na kuchagua wajumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na kuzungumzia maendeleo ya mchezo huo Afrika.
Wajumbe watakaochaguliwa watakuwa wakiiwakilisha Afrika katika mikutano ya FIFA na Kamati za Utendaji za CAF.
Kwa Kamati ya Utendaji ya CAF, Kanda ya Kaskazini inawaniwa na Hani Aboo Rida (Misri), aliyejitoa pamoja na Tarek Bouchamaoui wa Tunisia ambaye kwa sasa anawania nafasi hiyo bila kuwa na mpinzani.
Almamy Kabele Camara wa Guinea anawania bila kuwa na mpinzani kwa Kanda ya Magharibi A na Anjorin Moucharafou (Benin), Kwesi Nyantakyi (Ghana), Tata Adaglo Avlessi (Togo) na Hima Souley (Niger), ambaye amejitoa, huku wengine wakiwania nafasi ya Kanda ya Magahribi B outgoing member General Seyi Memene (Togo).
Constant Omari (DR Congo) hana mpinzani na aanawania kumrithi Thierry Kamach (Afrika ya Kati) kwa Ukanda wa Kati, pmoja na Leodegar Tenga (Tanzania) anapambana na Celestin Musabyimana wa Rwanda kwa tiketi ya Afrika Mashariki na Kati.
Mjumbe anayemaliza muda wake wa Ukanda wa Kusini, Dk. Molefi Oliphant (Afrika Kusini) nafasi yake inawaniwa na Adam Mthethwa (Swaziland), Kalusha Bwalya (Zambia), Danny Jordan (Afrika Kusini), Walter Nyamilandu (Malawi), John Muinjo (Namibia) na Justino Fernandes wa Angola.
majina ya watu sita, Ibrahim Galadima (Nigeria), Jacques Bernard Anouma (Cote díIvoire), Danny Jordan (Afrika Kusini), Kalusha Bwalya (Zambia) aliyejitoa, Mohamed Raouraoua (Algeria) na Suketu Patel (Shelisheli) wanawania nafasi ya kuiwakilisha Afrika katika Kamati ya Utendaji ya FIFA. Dk. Amos Adamu (Nigeria) na Jacques Bernard Anouma (Cote díIvoire) wanamaliza muda wao.
Hii ni mara ya tatu kwa Sudan kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa CAF, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1970 na 2007.
Katika hatua nyingine, wakati mkutano ukianza na kutarajiwa kufanyika kwa uchaguzi, Kanda ya Kusini mwa Afrika chini ya Shirikisho la Soka Kusini mwa Afrika, COSAFA, limegawanyika.
Mkutano wa 33 wa CAF, unafanyika Friendship Hall mjini Khartoum huku mlengo hasa ukiangalia kujaza nafasi mbalimbali za uongozi katika shirikisho hilo na zaidi ni nafasi nne za u wakilishi FIFA.
Lakini, mbali na hilo, wajumbe 14- wa Ukanda wa Cosafa wamekuwa na wakari mgumu baada ya kuingiza wajumbe wawili katika nafasi moja, mkongwe wa soka Zambia, Kalusha Bwalya, Walter Nyamilandu wa Malawi, Rais wa Cosafa, Suketu Patel na John Muinjo pamoja na Adam Mthethwa ni miongoni mwa wanaowania ukanda huo.
Danny Jordaan, mwenyekiti wa iliyokuwa kamati ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Dunia 2010 amejitoa kuwania nafasi ya ujumbe na sasa anawania uwakilishi Fifa.
Jordaan,59, ambaye alikuwa gumzo baada ya kuamua kufanya hivyo kuwania nafasi hiyo ya Fifa, moja ya nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Amos Adamu wa Nigeria ambaye amesimamishwa na Fifa kwa kile kilichodaiwa kulamba mshiko wa kura yake kwa waliokuwa wanawania kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2018 na 2022 .
Katibu Mkuu wa zamani wa Cosafa, Ashford Mamelodi alisema kuwa hali ya mgawanyiko pekee, itawafanya wajumbe 53 wanachama wa Caf kushindwa kuwaelewa.
Mamelodi alionya kuwa Ukanda wa Cosafa ulikuwa ukihitaji kujipanga tangu Septemba mwaka jana kwa kuunganisha nguyvu na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati badala ya kulalamikia mataifa ya Magharibu na Kaskazini kuwa yanapendelewa.
"Kama Katibu wa heshima wa Cosafa,sidhani kama tunaihujumu timu yetu. Cosafa ina nchi 14 na Cecafa 13 kama wangeunganisha nguvu, kati ya wajumbe 50 wa Caf, muungano wa ukanda huo ungekuwa na nguvu.
"Kaskazini una mataifa ya Misri, Algeria, Tunisia, Morocco na Libya na Magharibi kuna A na B na wana wawakilishi wawili CAF.
"Wako wapi viongozi wa kupigania yao? Nafikiri kuna haja ya kuwa angalizo katika hili," Mamelodi alisema.
Lakini mjumbe huyo wa FIFA wa maendeleo ya soka Kusini mwa Afrika alisema wajumbe wa Cosafa wakiwa na akili zao timilifu na huko wataamua kama ni kumwachi Rais wa Chama cha Soka Zambia, Bwalya na Patel wa Shelisheli.

PRINT