Michepuko inafilisi

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
39,595
Reaction score
61,015
Mida yote ni kupigwa mizinga tu;nikitafakari matumizi ya mwezi mmoja najikuta hakuna la maana nililofanya zaidi ya kukaa kati na kugaramia tu.Nikitazama mbele naona mwisho ni mbaya,kutimiza malengo binafsi inakuwa changamoto.....tuishi na michepuko kwa akili,ikiwezekana acha kabisa.
 
Mchepuko ukimuonyesha kwamba unazitumbua pesa kuanzia siku ya kwanza lazima Akupunuse mkuu
 
kuna mmoja ni mwanachuo fulan,ana chura matata leo anataka umpe fedha ya matumizi ya mwezi mzima,hujakaa sawa anataka laptop,hujageuka unaambiwa wazazi wangu wanataka matumizi....maji yamenifika shingoni inabidi nikimbie tu.
 
Unajua mkuu binadamu tunatofautiana malengo.

Kuna wengine kuwa na mchepuko ni moja ya malengo yake kwenye maisha au ni moja ya kukosa malengo kwenye maisha. Na kuna wale wameshatimiza malengo yao yote sasa wana kula raha na michepuko kukizi tamaa za kimwili.

Ni vizuri umegundua mapema kwamba ni lengo ambalo linakurudisha nyuma kimaendeleo.

Punguza gharama , piga mzigo, weka akiba na uitumie kuongeza kipato chako.
 
Ndiyo umelitambua leo, nyumbani ekfu5, mchepuko laki 2 tena zakutunzia mtoto asiye wako halafu mtu anajiita kidume,
mke michunusi mpaka mgongoni kisa pesa hakuna Mungu awaponye wanaume dizaini hii
ha ha ha ha mkuu we acha tu;naweka mikakati ya kupiga chini bila kumuumiza
 
Nilijitathmini nikaona mambo hayaendi,akiba inapungua tu badala ya kuongezeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…