INAUZWA Miche ya kisasa ya matunda inauzwa

Tunapatikana SUA,Horticulture(Tiba road)
Contacts:0719527062/0757056472
 
Nimesoma uzi woote, nimeng'amua changamoto moja,
Kuna watu waliwahi kununua miche(sio kwako) na haijaleta matokeo(mavuno)

Je nyinyi sasa mnatusaidia vipi wateja wenu likitokea suala kama hilo?

Maana kununua miche ya miembe/mipapai ya heka 3-10 halafu zote zikafeli mie si nitakufa kwa kihoro.
@Lily Tony
 
@Lily Tony
oh samahani mkuu.Sikuona hili swali.

zipo sababu mbalimbali zinazoweza kufanya mche/miche isilete matokeo yaliyotarajiwa.Sababu hizo zimegawanyika katika makundi tofauti
1.Mabadiliko ya tabia nchi
2.Magonjwa
3.kutokufuata mashrti na muongozo uliopewa na mtaalamu
4.Uchaguzi usio sahihi wa aina ya miche kulingana na eneo/hali ya hewa husika
5. Mkulima kushindwa kuupa mche/miche mahitaji unaostahili kwa wakati n.k
6.Mtaalamu kushindwa kufanya uchaguzi sahihi wa aina nzuri ya mche husika kwa ajili grafting au budding n.k

Sababu zote hizo nilizozitaja(na nyinginezo) kwa sehemu kubwa zinamlenga mkulima.Isipokuwa sababu ya 6.

Hivyo ni wajibu wako mkulima kufanya uhakiki wa eneo lako kabla ya kuanza kilimo. Kama unalima kibiashara nikimaanisha utapanda miche mingi ni bora ufanye treatment ya udongo kabla,kupima PH etc.
Uwe tayari kukabiliana na mabadiliko ya tabia inchi pindi yatakapotokea katikati ya safari yako.

Hudumia miche yako kwa kuipa mahitaji na matunzo yote muhimu ,pamoja na kusafisha shamba lako kila wakati.

Fuata maelekezo yote utakayopewa na mtoa huduma pindi tu utakaponunua miche Hasa miche iliyofanyiwa gratting na budding.Hii ni point muhimu sana,Hapa ndipo wateja wengi wanapokosea.

Nina amini ukifuata hayo yote lazima utapata matokeo mazuri.
 
@Lily Tony
Kwa Upande wangu nimerecord audio ambayo inamaelekezo yote muhimu
Hivyo kila mteja anaponunua miche lazima nimtumie.

Pili lazima nifanye follow up kwa wateja wote kila inapofika mwisho wa mwezi(Walionunua miche kwangu watakuwa ni mashahidi katika hili maana ni jana tu nimewasiliana nao mmoja baada ya mwingine) Lengo kujua maendeleo na changamoto wanazokutana nazo ili kuzitatua.

Pia kwa upande wetu tunahakikisha tunafanya uchaguzi uliosahihi wa mche wa kufanyia graffting na budding.

Sababu zote hizi zinaniweka upande salama hakuna mteja alienunua miche kwetu ambae aliewahi kupata changamoto uliyotaja.
 
@Lily Tony
Mwisho hakikisha mawasiliano kati ua mtaalamu na mkulima yanakuwa endelevu kuanzia siku unaponunua miche.Nisumbue kila wakati,uliza maswali bila kuchoka.Hii itatusaidia kutatua changamoto yako katika hatua za awali kabla miche yako haijateketea yote
 
Screenshot_2021-03-04-08-39-01.png
kitalu cha miti ya mbao
 
Kama ni huyo jamaa wa Kigamboni nilishawahi mwambia Lily, kwamba huyo jamaa wa miche ya apple ni mbabaishaji.
Nimepokea haya malalamiko kwa zaidi ya wateja 4 mkuu.Niombe samahani kwa usumbufu.
Tayari nimepata mawasiliano ya mtu mwingine ana miche ya apple.Yuko Morogoro,kama utahitaji apple basi utanitafuta nikupe namba
 
chungwa mavuno baada ya miaka 2 mpaka 3

Chenza mavuno baada ya miaka 2 na nusu

Passion aina zote mavuno baada ya miezi 9

Tende mavuno baada ya miaka 8
 
0719527062/0757056472

Location: Chuo cha Kilimo, SUA kitengo cha Horticulture,tiba road.

Ushauri na muongozo ni bure.
 
Wakuu karibuni,mvua zimeanza kunyesha kwa baadhi ya maeneo ndio msimu mzuri wa kupanda miche kabla mvua za masika hazijaanza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom