Kama nabii niliyejituma, nitawafunza ya upole na ya huruma
Afrika Bado Ipo nyuma
mpaka ivunjwe mipaka, tung'oe vibaraka
na tuzike matabaka
nikisema niseme kweli manjagu watanisaka
natamani kutoa sadaka, mifuko ina viraka
Kama mnataka wepesi mshike huu waraka
natambaa Kama ukoka, majani nimeshang'oka