Michango Sasa Basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Michango Sasa Basi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by X-PASTER, Jun 21, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  This is what is happening to my life now - nimechoka kabisa kuamka asubuhi
  sana only to find out that my salary ends kwenye michango ya watu!

  MICHANGO! Ah Mungu wangu weee... Nchi gani hii kila ukiamka, kila ukiwa
  njiani, ofisini au ukilala ni kusakamwa na michango tu?

  Michangooo, michangooo, michangoo tu! Twatolewa weeeee mpaka tumepata
  pancha.

  Hapana jamani. Hakikyanani tena sasa mmezidi.
  Amka asubuhi utasikia hodi, ukifungua kuna mtoto wa jirani na kikadi
  kilichoburuzwa kwenye kompyuta kikiomba mchango wa "Kipaimara." Toba!
  Unamwambia utawasiliana na baba yake anaondoka.

  Upo kwenye daladala unawahi Pugu rodi kazini, kufika kazini unaombwa samahani na mfanyakazi
  mwenzako... akidai alikuwa na barua yako na anakupatia bila hiana. Mtumeee! Unafungua
  unakuta ni kakadi kengine ka mchango. Safari hii ni ka "chicken party I mean Kitchen party na
  kameonyesha kiwango kabisaa. Kwa fasheni ya sasa ni 20,000/-.
  Huyu ni wa aibu, hivyo unampa dala ukidai zingine siku nyingine.

  Unatoka kazini hujala chochote kwa vile 5,OOO/= ulitoa kwenye"chicken party" ... Kitchen party
  ambayo hata maana ya neno lenyewe hujui. Unakuta kengine nyumbani. Hako ni
  ka mchango wa "send off'. Jamani mwanitakani lakiniiii?

  Unaoga, ghafla aja mtu na kadi, tena safari hii ni mchango wa harusi ya
  shemejiyo. unajikamua kamua ili usiadhirike ukweni. Unampatia kiasi
  kilichokuwa ada ya mtoto shuleni.

  Hapo bado kuhudhuria vikao vya shemejio vya harusi. Nako kuna ka mchango ka
  kila mkutanapo kanaitwa uchache au chakaza.Shemeji mtu tena si ni lazima
  wakukamue kamasi mwanangu?

  Haiishii hapo. Unakuja ujumbe kuwa dada yake dada wa mama yako mzazi kafia
  Muhimbii yuko mochwari. Hapo achilia mbali bakuli la mchango utakalokuta
  linakungoja. Patakuwepo pia kitabu cha kujiorodhesha wanandugu na kiasi
  mtakachotoa.

  Yallah! Michango haitoshi. sasa yabidi wale wa karibu yake mjazie ili
  iwezekane kukodisha "Fuso" ya kumpleka kwao Mbagala. Na huko nako ni lazima
  mkamuliwe tena hela ya kununulia mboga.

  Unasema walau sasa napumua. Mara inatoka barua kwa wajomba zako kuwa ile
  arobaini ya babu ni mwezi ujao. Na unatakiwa mchango wa kununulia nyama na
  mchele kwa ulaji wa siku hiyo.

  Kwani utakimbia jamii yenu kwa vile imekuwa ya michango?
  Haya tena. Kazini nako wameanza kukukata mshahara kwa madeni uliyo nayo
  SACCOS. Mtoto wa jirani ambaye umemdhamini ubatizo naye aja akidai mchango
  wa kununulia gauni la "birthday".

  Ebo! Sasa mwanangu? Utasahau mdogo wenu wa mwisho aliepigwa ritrenchi na
  sasa ana mtoto mchanga wa kubatiza... Utakwepa vipi usimchangie kitu kidogo
  atakapowahi kwako majogoo?

  Afadhali usingezaliwa Kipatimo mwanangu. Mwezi huu ni wa kuwacheza watoto.
  Utawaambla nini huko kwenu wakuelewe kama hukutuma mchango wa hilo tamasha
  ambapo mwezi uliopita mtaa wa pili alipochezwa Sikuzani watu walikula
  wakasaza?

  Bado wana wewe kaka!
  Mtoto wa kaka yako anapata komunio utamkwepaje mbele ya jamii
  iliyokuzunguka? Na asavali tajiri yako asingekuwa na mtoto Chuo Kikuu
  anayegradueti mwisho wa mwezi na keshakuletea kadi ya mchango.
  Utachangia sana graduesheni ya sekondari, chekechea hata na darasa la
  saba, nini VETA...
  Mtajiju ! Kwani nani aliyewatuma kuzaliwa Bongo? Asavali wanajeshi hawana
  sherehe hata wapatapo usaameja.

  Utadhani sasa utapumua uendapo nyumba za ibada. Toba yaillahi! Huko
  Utakutana na michango ya ofisi ya paroko, mchango wa jengo na pikipiki ya
  shemasi - kama sio mchango wa madrasa, mchango wa majamvi msikitini ama
  mchango wa kofia ya imamu. Upo hapo?

  Huko kijijini ndo usiseme. Kuna barabara, shule, maji, zahanati, ugeni wa
  DC, vyote vyadai mchango na mara nyingi hakuna risiti. Si ni jamaa zako una
  wasiwasi gani weye?

  Umesahau mfereji wa kijiji, trekta la mshikamano, shamba la kijiji na
  kadhalika - vyote navyo vyataka michango; achilia mbali mchango wa damu
  Muhimbili! Ila asavali huu wa damu kwa vile hauhusu fedha.

  Unafikia mahali unasema utapanchi hiyo michango. Ukiwaza hayo, mara anapita
  Katibu kata mwenyewe. Huyu anadai mchango wa mapokezi ya Waziri Mkuu au ya
  Mwenge utasemaje?

  Unaambiwa hakuna cha huruma na mtu wala hakuna wa kutaka kujua kipato
  chako kabla hajakupa kadi ya mchango.
  Shuleni watatuma barua kuhusu mchango wa kumuaga mwalimu mkuu. Bado
  michango ya tuisheni, uji wa saa nne, safari ya Serengeti na T-shirt za siku
  ya michezo shuleni.

  Hapo usisahau redio ya shule ikikosa betri wazazi shurti mchangishwe.
  Mwashangaa nini, kwani hospitalini hamchangii?

  Michango hii! Sasa mtatukamua mpaka damu. Ipo ya kwaya, Saidia Simba Ishinde, usafi wa
  makaburi, basi la kijiji. Bado sijasema michango ya SACCOS na upatu kazini
  kwenu.

  Enheee, halafu mama watoto anacheza mchezo. wiki hii zamu yake kutoa na
  mama nanihino kaja jana kukumbushia asicheleweshewe kama safari ileee...

  Hujakaa sawa hodi! Wakala wa wazoa taka yuko mlangoni na kitabu chake cha
  risiti mkononi. Anang'aka kwamba safari hii usipotoa atakuripoti kwa
  mwenyekiti wa mtaa kwamba huna ushirikiano katika mambo ya kutunza
  mazingara.

  aaaaaaaaaah...! Nachoka kabisa!

   
 2. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli inaumiza sana. Ukijulikana tu kuwa umepata kazi basi ujue balaa la michango ndo linahamia kwako. Jitu lingine linaamua kuoa hata mwanamke asiyeoleka ili naye awakamue wachangiaaji eti kwa kuwa naye alisha changia sana. Hivi sasa mpaka mtu kuchukua fomu ya kugombea uongozi anatembeza bakuli la michango.

  Jamani kwa mwenendo huu mtatuuuuuuuuuuuuuua
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  tutafute mbadala jamani wa jambo hili tuumuchi jamani mwe
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  nimesoma nusu tu yote hayo umetype wewe ama umempa secretary wako???
  hata mie michango imenichosha sana
   
 5. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #5
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shida ukiwaambia wabongo kuhusu hili watakuchukia sana, tu bado maskini saana tuna priorities nyingi kuliko hizo "chicken party", hatuwezi kujenga nchi kwa sherehe, tullishasema kama imeshindikana tuachane na KILIMO KWANZA na kuzindua rasmi UTALII KWANZA ndo ambao utaendana na haya madudu tunayoyafanya!
   
 6. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  maukweli yako yanabamba...so what can we do?
   
 7. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni vigumu sana kusema harusi zisichangiwe, hii inatokana na tabia ambayo tumejiwekea ya kutaka kufanya sherehe kubwa kubwa za harusi ambazo ni vigumu sana kwa mtu mmoja kuweza kufanya hivyo, ndio maana utamkuta mtu anatembeza bakuli la mchango (card za mchango) ili aweze kukamilisha malengo yake aliyo ta weka.....

  Hivi juzi tu jamaa yangu wakaribu ali funga ndoa na harusi yake ili gharimu takribani tsh million 17, na kulikuwa hakuna pombe, kilicho ni shangaza kwenye harusi hii haikufana sana japo ili gharimu pesa nyingi sana, nimesema hivyo kwa kuwa kuna rafiki yangu alifanya harusi ya tsh million 4 tu huwezi hamini ilifana sana na watu walikuwa wengi kushinda hiyo iliyo gharimu million 17.

  Nilicho jifunza hapa ni kwamba harusi unaweza kujipanga mwenyewe kwa kuigharamikia , kwa mfano hiyo ya million 4 ni pesa ndogo sana ambayo mtu unaweza kujipanga kwa mwaka mmoja na kipata na kufunga ndoa pasipo kuwasumbua watu.

  Tatizo kubwa lipo kwetu wenyewe kwamba tuna taka vitu vya gharama kubwa na ambavyo hatuwezi kivi fanya wenyewe pasipo kutegemea michango ya watu.

  Umefika mda sasa watanzania tu funguke macho na kufanya mambo ya maendeleo na kuachana na hizi hanasa na masaa 4/6 ambazo mwishoe ndoa ina vunjika ndani ya wiki moja huku ukiwaacha ndugu zako kwa kilala njaa kutokana na harusi yako.

  Kwa wenzetu ulaya kwa jinsi nilivyoona huwa wanafanya harusi ya kawaida sana na ambayo hai gharimu pesa nyingi sana na muoaji na muolewaji ndio huwa wana gharamia kwa 90% gharama ya harusi yao,ambapo ni tofauti na huku bongo ambako utakuwa bwana harusi mara nyingine anachangiwa hadi kununua gauni la bibi harusi.
   
 8. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mengi ya hayo yanaendekezwa na uvivu,umwinyi na kupenda makuu!!
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mkuu umesahau michango ya vyama vya siasa kupitia SMS kwa ajili ya uchaguzi, kila asubuhi wanakumbusha
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu safari bado ndefu, yaani hata vyama vya siasa, inamaana hwapati tena ruzuku au...?
   
 11. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  wewe changa tu,tenda wema huende zako,you will be repaid in heaven
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,827
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona hukuweka na michango ya JF? lol! Najua tukianza kuorodhesha hapa michango patakuwa hapatoshi. Hivi JF inashindwa kweli kutafuta vyanzo vyake vya kibiashara ili kuweza kujiendesha bila utegemezi wa michango ya wanachama. Ina maana kama wanachama wakiacha kuchangia basi hili jamvi letu lililokuwa maarufu sana kwa Watanzania wa ndani na nje ya nchi linaweza kuzimika na kupotea katika anga za mtandao? mhhhhh! msisahau mkono mtupu haulambwi!
   
 13. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,718
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  Michango ya harusi,kitchen party, ubarikio ni kuukuza umaskini katika jamii zetu. Mnachanga kwa ajili ya nini kama ni harusi muhimu ni kwenda kuwashuhudia wawili wanavyoahidi/toa ahadi zao kila mmoja aelekee kwao wabakie wanafamilia kama inahitajika otherwise inakuwa ni mwisho wa shughuli.Mbona nchi za wenzetu hazina mambo kama haya eti mchango wa nini sijui nini. Mbadala wa yote haya ni kuanzisha kupitisha bakula kwa ajili ya mchango wa mtoto kwenda shule tuone!!!
   
 14. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2010
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umeona heeeeeee,haulambwi.
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  sisi wa bara tunajiendekeza sana tu, kila kitu michango....sijui hulka hii inatoka wapi

  wenzetu wa visiwani sijawasikia kuchangishana na kwenye harusi ukimpa mtu mchango wenyewe wanasema unamtukana, na wanafanya harusi za kiasi chao tu, si lazima harusi iwe kubwa ki hivyo

  anyway labda tunaweza kusema wao hawaweki pombe harusini kwa hiyo gharama zinapungua, lakini nafikiri tungeweza kupanga uzuri gharama zikapungua kwetu pia kwa kualika watu kidogo au kuweka pombe kidogo.
   
 16. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2010
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi binafsi michango naichukia sana..... Ila ukimweleza mtu swala hili anakwambia sababu wewe umeshaoa ndo maana unachukia michnago... Nikijaribu kumpatia sababu za kuchukia michango hanielewi kabisa....
  Kwa hapa Tanzania (hasa Bongo) Michango imechosha kwa kweli, na tunahitaji kuiepuka taratibu, maana inazidi kutuletea umaskini kwa hata wale ambao tunahuhakika wa kipato kidogo kila mwezi... Mshahara wa mwezi unashindwa kabisa kukutana na mshahara wa mwezi unaofuata...

  ....MIMI NAOMBA WA JF TUWE WA KWANZA KUWAELEZA WATU KUHUSU UMUHIMU WA KUACHANA TARATIBU NA TABIA HII...
   
 17. T

  Tall JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.sio lazima uchangie......usife na tai shingoni.kupewa kadi si lazima uchangie.unaona aibu kukataa mkuu?
  2.hizo ni mila zetu waafrika ni vigumu kuziepuka......hapa nilipo nina kadi kibao.
  3.unaweza kupunguza amount of contribution halafu si lazima uende kwenye sherehe.
  4.kumbuka hata wewe ulichangiwa/utajachangiwa.
   
 18. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,448
  Likes Received: 2,024
  Trophy Points: 280
  copy and paste hiyo, kuna mtu anajisumbua kuchapa siku hizi
   
 19. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Changeni tu jamani, Mungu atawazidishia... (espeshale pale kanisani)
   
 20. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Ukichangia JF huamki na Hangover, ukiwa kwenye forum hutatakiwa kwenda kutoa zawadi kwa uliowachangia, hakuna uchakavu etc sanasana unapata elimu ni mchango endelevu, elimishi na mchango wenye tija.
   
Loading...