Michakato ya kidemokrasia inachelewesha sana mambo

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,220
12,725
Cheki mchakato kama wa wabunge kumi na tisa wa CDM. Nikupotezeana tu muda. Mwananchi anafaidika nini? Leo nchi kama US wanahangaika na habari za bunduki lakini hawawezi kufanya kitu sababu ya michakato ya kidemokrasia yenye kuchosha. Leo China inaweza anzisha sera kwaajili ya maendeleo ya nchi na kesho kuitekeleza. Ikisema inajenga reli ya mwendo kasi inajenga fasta. Marekani wameshindwa kabisa kujenga reli kama hizo sababu ya michakato ya kidemokrasia.

Demokrasia ni janga kwa mwanadamu. Haiwezekani nchi ikaongozwa na raia wote.
 
Leo wakisema ndugu yako anyongwe bila kujitetea, anyongwe?

Wakisema wachukue fedha kwenye account yako wajenge reli, wachukue?

Wakisema uende kuchimba mtaro hela utakayopata uchangie mshahara wa Diwani, uende?

Waje wakuhunguze kwako na mkeo usiku, waje?

Huelewi kitu kaa kimya.

Pato la mtu china ni $11,713
US pato la mtu ni $66,144
Tanzania ni $1,132
 
Hata kwenye familia ukiendekeza demokrasia lazima baba apandwe kichwani na mama. Watoto na house girl wakiona mama amefanikiwa nao wanamsapoti na wao wanakupanda kichwani.
 
Kwa hiyo tumuache Samia achape kazi tuache haya makelele ya kila siku sio?
 
Demokrasia ni kitu cha msingi saaana ni sawa na neno haki.na penye haki kuna Mungu na kwenye Mungu kuna furaha na Amani.Huwezi kutenganisha demokrasia na maendeleo.afrika demokrasia 0 na maendeleo 0
 
Kwahiyo unataka utashi wa mtu mmoja (dikteta ) amue hatma ya taifa? Mleta mada taratibu bwana.

Dikteta ni mzuri kama atakuamuria Jambo jema lifanyike juu yako. Lkn vipi akiamuru duka lako la fedha za kigeni liporwe? Fedha zako kwenye akaunti zichukuliwe? Matokeo yako ya ushindi wa uchaguzi yaporwe?
Think twice mleta mada
 
Leo wakisema ndugu yako anyongwe bila kujitetea, anyongwe?

Wakisema wachukue fedha kwenye account yako wajenge reli, wachukue?

Wakisema uende kuchimba mtaro hela utakayopata uchangie mshahara wa Diwani, uende?

Waje wakuhunguze kwako na mkeo usiku, waje?

Huelewi kitu kaa kimya.

Pato la mtu china ni $11,713
US pato la mtu ni $66,144
Tanzania ni $1,132
Hajui hata kuandika hizo pumba zake hapa ni demokrasia tosha,
 
Cheki mchakato kama wa wabunge kumi na tisa wa CDM. Nikupotezeana tu muda. Mwananchi anafaidika nini? Leo nchi kama US wanahangaika na habari za bunduki lakini hawawezi kufanya kitu sababu ya michakato ya kidemokrasia yenye kuchosha. Leo China inaweza anzisha sera kwaajili ya maendeleo ya nchi na kesho kuitekeleza. Ikisema inajenga reli ya mwendo kasi inajenga fasta. Marekani wameshindwa kabisa kujenga reli kama hizo sababu ya michakato ya kidemokrasia.

Demokrasia ni janga kwa mwanadamu. Haiwezekani nchi ikaongozwa na raia wote.

Tatizo sio demokrasia per se. Tatizo ni demokrasia ya vyama vingi. Chama A (ambacho hakiko madarakani) kikiruhusu chama B (ambacho kiko madarakani) kitekeleze mipango mizuri itakayoleta manufaa makubwa kwa taifa, basi uwezekano wa chama A kushinda uchaguzi na kuingia madarakani unakuwa mdogo sana. Kwa hiyo, strategy ya kwanza ya chama A ni kukikwamisha chama B kutekeleza mipango yake ili wananchi wakione chama B kwamba hakifai kutawala nchi.
 
Watu wengi Tanzania hawajaelimika, mmoja wao ni wewe hapo. Makubaliano katika maamuzi ya maisha ya watu lazima yawe ya pande mbili yaani ikiwezekana hata mtuhumiwa akiri kosa lake na sheria iangaliwe ili kutoa hukumu. Kuna kipindi watu waliuliwa, walionekana hawana maana, waliteswa, walidhurumiwa, walikuwa na furaha fake kumfurahisha kiongozi, hawakusema wala kuhoji maamuzi batili ya kiongozi😠😠😠
 
Leo wakisema ndugu yako anyongwe bila kujitetea, anyongwe?

Wakisema wachukue fedha kwenye account yako wajenge reli, wachukue?

Wakisema uende kuchimba mtaro hela utakayopata uchangie mshahara wa Diwani, uende?

Waje wakuhunguze kwako na mkeo usiku, waje?

Huelewi kitu kaa kimya.

Pato la mtu china ni $11,713
US pato la mtu ni $66,144
Tanzania ni $1,132
Kwani kutokuwa na demokrasia ndiyo kutokuwa na mambo hayo? Mbona hao US wenye demokrasia miaka mingi wamewadescriminate watu weusi kwa miaka mingi, na hata leo!!.
 
Demokrasia ni kitu cha msingi saaana ni sawa na neno haki.na penye haki kuna Mungu na kwenye Mungu kuna furaha na Amani.Huwezi kutenganisha demokrasia na maendeleo.afrika demokrasia 0 na maendeleo 0
Demokrasia haiwezi leta maendeleo. Inachofanya inaharibu maendeleo yaliyokwisha letwa. Haina maana kabisa.
 
Kwahiyo unataka utashi wa mtu mmoja (dikteta ) amue hatma ya taifa? Mleta mada taratibu bwana.

Dikteta ni mzuri kama atakuamuria Jambo jema lifanyike juu yako. Lkn vipi akiamuru duka lako la fedha za kigeni liporwe? Fedha zako kwenye akaunti zichukuliwe? Matokeo yako ya ushindi wa uchaguzi yaporwe?
Think twice mleta mada
Kuna mifumo mingi na si udikteta tu, japo nao si mbaya. Kiongozi mzuri na mbaya anaweza patikana hata kwa demokrasia na mifumo ya kumcheki ya kidemokrasia ikafeli, na kuleta michakato mirefu ya kuchosha na kupoteza wakati.
 
Demokrasia kwa hizi nchi zetu zinazoendelea ni upumbavu mmoja tu na haiwezi kuleta maendeleo, kibaya zaidi kisema hivi unakuta watu wanakutolea mifano ya U.S.A, UK na kwingineko😂.

Jamani hiyo demokrasia mnayoiona huko hawakuanza nayo from the scratch, wakati wao wapo level kama tuliyopo sisi leo hawakua na kitu kinaitwa demokrasia, watu walihenyeshwa hasa na hapakuwa na kucheka na kima mpaka baadae sana walipo fika level ambayo inahitaji hicho mlichokipigania na kiliwekwa kwa utaratibu mdogomdogo.

Demokrasia kwa nchi za AFRIKA NI UJINGA na hatutaweza kufika popote, maana waafrika by nature ni wavivu na wajinga wa akili.
 
Watu wengi Tanzania hawajaelimika, mmoja wao ni wewe hapo. Makubaliano katika maamuzi ya maisha ya watu lazima yawe ya pande mbili yaani ikiwezekana hata mtuhumiwa akiri kosa lake na sheria iangaliwe ili kutoa hukumu. Kuna kipindi watu waliuliwa, walionekana hawana maana, waliteswa, walidhurumiwa, walikuwa na furaha fake kumfurahisha kiongozi, hawakusema wala kuhoji maamuzi batili ya kiongozi😠😠😠
Kwani demokrasia ndiyo inazuia watu kuuwawa? Demokrasia ni vurugu tu. Na inafanya serikali kutekeleza sera zinazoumiza nchi ili asikose kura, au wapiga kura wengi wanataka. Na watu hawapendi kodi kubwa huku wakitaka welfare zaidi. Mwisho wa siku demokrasia ni janga kwa nchi.
 
Demokrasia kwa hizi nchi zetu zinazoendelea ni upumbavu mmoja tu na haiwezi kuleta maendeleo, kibaya zaidi kisema hivi unakuta watu wanakutolea mifano ya U.S.A, UK na kwingineko😂.

Jamani hiyo demokrasia mnayoiona huko hawakuanza nayo from the scratch, wakati wao wapo level kama tuliyopo sisi leo hawakua na kitu kinaitwa demokrasia, watu walihenyeshwa hasa na hapakuwa na kucheka na kima mpaka baadae sana walipo fika level ambayo inahitaji hicho mlichokipigania na kiliwekwa kwa utaratibu mdogomdogo.

Demokrasia kwa nchi za AFRIKA NI UJINGA na hatutaweza kufika popote, maana waafrika by nature ni wavivu na wajinga wa akili.
Demokrasia ni anasa ya matajiri. Na mbaya zaidi hata kwao huwa inaharibu maendeleo waliyojiletea. Kwenye demokrasia zao, huyu anataka hiki, analobby anapata. Huyu anataka kile, analobby anapata. Vita vya kihuni vinafanyika huku mambo ya maana yakikwamishwa.
 
Kiongozi mzuri na mbaya anaweza patikana hata kwa demokrasia na mifumo ya kumcheki ya kidemokrasia ikafeli, na kuleta michakato mirefu ya kuchosha na kupoteza wakati.
Kwenye nchi zenye demokrasia iliyopevuka kiongozi mbaya anaondolewa kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye ( ousting the HoS by casting the vote of no confidence)
 
Back
Top Bottom