Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,220
- 12,724
Zamani wakati wa ufalme, nchi ilikuwa mali ya mfalme. Mapato yote ya nchi ni yake mwenyewe. Akikopa akashindwa kulipa anafilisika mwenyewe. Wafalme walikuwa makini sana kwenye kukopa. Maana walijua wasipolipa watafilisiwa. Mfalme wa Misri, Mohammed Ali alikopa sana.
Deni liliposhindwa kilipwa Uingereza na Ufaransa, wakavamia nchi. Wakachukua mfereji wa Suez na kuweka waziri wa fedha wao kuhakikisha deni linalipwa. Dynasty yake ikaingia katika aibu.
Leo hii watawala wa kidemokrasia hawamiliki nchi, ni wadhamini tu. Madeni wanayokopa hayawahusu. Kufilisika kwa nchi hakuwahusu. Wapo tu kwa muda mfupi na kisha wanasepa zao. Hata moja ya sababu ya Sri Lanka kuingia shidani ni pamoja na madeni makubwa waliyoshindwa kuyalipa.
Na ubaya demokrasia inakulazimisha tu kukopa. Watu wanataka kodi nafuu, mishahara mikubwa, chakula cha kama bure nk nk. Nafikiri serikali za kidemokrasia, hasa za nchi maskini ziko doomed kufeli.