Miaka yangu 7 ndani ya JF, najivunia haya...

Miaka yangu 7 ndani ya JF, najivunia haya...

moniccca

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2015
Posts
2,383
Reaction score
3,287
Tarehe 15. Nov. Nitafikisha miaka Saba kamili ndani ya JF.

Ni safari ndefu na ngumu mno hasa kukabiliana na hoja za wadau wengine humu ndani.

Mbali na changamoto lakini JF imekuwa sehemu yangu ya maisha kwa sababu zifuatazo.

Nilijiunga JF nikiwa muajiriwa tu wa kawaida kabisa ambaye anafanya kazi kwaajili ya kufanya siku ziende. (Kupata mahitaji muhimu ya kuish) basic needs.

Nilikuwa single, sikuwa na mpenzi, mchumba wala hawala.

Lakini kupitia JF nimepata mume ambaye sijawahi kujuta kukutana nae.

Kupitia JF nimepata connections na michongo ya pesa ya maana mpaka kufikia hatua ya kuamua kuacha kazi.

Maisha yangu yamebadilika sana kutoka kuwa muajiriwa mpaka kuwa MUAJIRI.

Nilionekana ni mwanamke chakaram, Malaya, maji mara moja , maharage ya Mbeya lakini ukweli ni kwamba yote yale yalikuwa changamsha jukwaa tu.

Niliyobahatika kukutana nao uso kwa uso hawakuamini kama mimi ndiye Moniccca pasua kichwa wa JF.

Nilimua kujibrand vile ili kujiweka tofauti na wengine na pia kuendana na dhana ya fake I'd .

Ninaiheshimu mno JF na ntaendelea kuiheshimu kwa sababu imekuwa jukwaa muhimu sana katika mafanikio yangu yote.
 
moniccca nakumbuka sana harakati zako hapa jukwaani sijui ulipotelea wapi .daah hongera kwa kutimiza miaka 7
 
Happy 4 u dearest,
Ubarikiwe zaidi na zaidi.
 
Back
Top Bottom