Miaka nenda rudi ya madeni, hakuna Ulaya au Amerika walipotaifisha mali

Wachina waliamua mpaka kumwita Kikwete profesa, hata mwenyewe alisema kuwa alishangaa sana.

Kuna rafiki yangu alienda China kwaajili ya kusaini mkataba wa kutengenezwa mashine za kiwandani kwake, zilikuwa na thamani ya kama dola 1.2m. Anasema alishangaa namna alivyopokelewa. Airport alienda kupokelewa na maafisa wa kiwanda, wasichana 8 warembo, akapelekwa hoteli kubwa ya kifahari, na kisha akaambiwa kuwa kati ya wale wasichana 8, anaweza kuchagua yeyote anayetaka akae naye pale hotelini. Na kwamba, hata kama akitaka kuketewa mwingine tofauti kila siku, ingewezekana pia.

Mambo haya madogo madogo, ukiona yanafanyika, ujue wamekwishafanya utafiti, na kuona kuwa kwa mwafrika yana nguvu katika kufanya maamuzi. Ni viongozi wangapi wa Afrika wanafanyiwa hayo, na kisha kuwa vipofu katika maamuzi yao? Na kuna uwezekano mkubwa, wazungu hawafanyiwi hivyo vioja.
😅😅😅kwa hawa wazee wa bongo kama Wasira anakuwa kashamalizwa
 
Kuna siku nilikuwa na ongea na mtu mmoja mkubwa alie kuwa akishabikia sana wachina na kukuwa kwa dola ya wachina kitu nilimwambia na hiki umekiandika nikama mimi na wewe tumewahi kitana na tukapanga hii story.
Ngoja nikwambie jambo siku China itakuwa super power nation. Shetani atatoka ktk hali yakuto onekana na kuwa dhahiri ktk macho yetu. Dunia itakuwa mahali pa hatari na shida kuishi haki za watu zita vunjwa na dam nyingi itamwagika. Naimani kama kila taifa lina kisima cha damu za watu wake zilizo mwagika basi china uwenda ikawa ktk top ten nation zinazo mwaga dam kwa wingi duniani.
Mtu anaye support wachina hajuwi kesho yake wala hajuwi ana support kitu gani. Hili ndio taifa halina Mungu na ndio taifa siku moja Mungu atalipa kichapo kitakatifu yani mpaka wakiri Mungu yupo na anaishi Milele na milele.

Sasa Tutawapa Jandari yetu na Hutotufanya Kitu! Na Tutajenga!kelele zako hazisaidii kitu!
Ni wivu tuu!
 
Picha kamili ya mchina inaonekana kwa wawekezaji na wakandarasi wa kichina tulio nao. Kama wana uwezo wa kupiga na kudhulumu wafanyakazi bila oga wowote mnategemea nini?

Wachina wanakubalika kwa viongozi wa kiafrica kwa sababu ni watoaji na wapokeaji rushwa wazuri nje ya mazingira ya kwao. Na hii ni strategy na sera ya china kama nchi kwa ajili ya kushinda tenda na kukamata nchi za ulimwengu sehemu ambayo rushwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.

INGEPENDEZA UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO UKAFANYIWA UPEMBUZI YAKINIFU TENA KWA KULETA WATALAAM MAKINI ILI KUEPUKA FEDHEHA YA KUWA KICHEKO DUNIANI NA WAJUKUU NA VITUKUU WETU
 
China inakumbatia wala rushwa na wavunjifu wa haki za binadamu
Ni mbinu hiyo hiyo inatumiwa na Marekani. Ndiyo maana hata mashirika yao ya kijasusi yanapata wakati mgumu sana kufanya kazi kwenye nchi zenye kiwango kidogo cha ulaji rushwa.

Kilichofanyika China kawashinda wamarekani na wenzake kwenye mchezo wao wenyewe!!!
 
Tena usiombe alikulia kwenye utapiamlo wa umasikini shule kilometa 10,anagombea matunda pori na nyani anashindia viporo kasoma kwa msaada wa kijiji mtu huyu akipata madaraka au akiwa lecture mbona mtakoma.
"OCD kamata huyu weka ndani "
"Atakae faulu somo langu ni mwanaume"
Maskini tunakuwaga na roho za kikatili sn
 
"Atakae faulu somo langu ni mwanaume"
Kwa kauli hizi kuna uwezekano mwenyewe somo hilo linamshinda ama mwenyewe hana mbinu za ufundisha. Kwa sababu kama huwezi kufafanua concepts na theories za somo husika kwa urahisi wanafunzi wakaelewa, basi kati ya mawili ama yote hapo juu yanakuhusu.
 
Marekani yenyewe wanakopa China
Msiwe mnalishwa ujinga, bila ya kufanya utafiti. US haijawahi kukopa China. Bali, China ili kujiimarisha kiuchumi, imekuwa ikinunua treasury bill za US government, sawa na yeyote abayetaka kununua.
 
Kwa kauli hizi kuna uwezekano mwenyewe somo hilo linamshinda ama mwenyewe hana mbinu za ufundisha. Kwa sababu kama huwezi kufafanua concepts na theories za somo husika kwa urahisi wanafunzi wakaelewa, basi kati ya mawili ama yote hapo juu yanakuhusu.
Wapo walimu badala ya kurahisisha lugha Ili mtahiniwa aelewe swali wao utumia lugha ngumu kukomoa,hapo ndipo upatikana vyeti vya chupi,na degree chupi wakipata ajira nao uumiza watu kwa kumbuka alivyokaa mguu pande Ili afaulu mtihani sababu ya tu lugha ngumu kwa swali jepesi
 
Asians wanakulipa mshahara Ili usife kesho urudi tena kufanya Kazi nadharia za kimasikini kabisa.
Check waliofanya Kazi kwa mabeberu migodini,Unapiga job wiki sita unaenda off wiki 2 ndege ya kuja dar kupumzisha akili ipo hata mia utoi.
Hahahahahahah hapo unachokaje kazi? Nina mwanangu alifanya Ministry of Land walikuwa na mpango wa kusajili hati zote kwenye system flani! Mfaransa ndio alipewa ule mchongo jamaa walikuwa wanamenya yani kila siku 100K!

Likizo unakula 700K ya kwenda kupumzika kwa week 2 tu!

Ishu haikudumu zaidi ya miezi 6! Wakawa wamemaliza pilot phase, hapo mpango wa mradi kuanza rasmi sasa ndio wabongo wakafanya figisu yani dah😅 ila jamaa alitoka na mtaji wa kutosha ndani ya muda mfupi tu!
 
Hahahahahahah hapo unachokaje kazi? Nina mwanangu alifanya Ministry of Land walikuwa na mpango wa kusajili hati zote kwenye system flani! Mfaransa ndio alipewa ule mchongo jamaa walikuwa wanamenya yani kila siku 100K!

Likizo unakula 700K ya kwenda kupumzika kwa week 2 tu!

Ishu haikudumu zaidi ya miezi 6! Wakawa wamemaliza pilot phase, hapo mpango wa mradi kuanza rasmi sasa ndio wabongo wakafanya figisu yani dah😅 ila jamaa alitoka na mtaji wa kutosha ndani ya muda mfupi tu!
Beberu analipa maslai mazuri Sana hasa asipoingiliwa na mamlaka za kiswahili au ma HR weusi kwenye kubana.
 
Beberu analipa maslai mazuri Sana hasa asipoingiliwa na mamlaka za kiswahili au ma HR weusi kwenye kubana.
Eeh tabu ni ngozi nyeusi ndio inazingua yani huwa lazma wanatengeneza kamati ya kupiga panga😅!
Kama ilikuwa mlipwe laki mnakula 40K 🤩 60K wanagawana
 
Back
Top Bottom