Miaka nenda rudi ya madeni, hakuna Ulaya au Amerika walipotaifisha mali

Ukiskia ukahaba ndo huu
images-547.jpg
 
Jiwe alipoona mikopo ua china haingiliwi maswala ya utawala bora na demokrasia akakimbilia huko akidai ni marafiki wa muda mrefu.

Bagamoyo Port tu ilimtoa baru
Jpm anamapungufu yake mengi kwny demokrasia,

Ila sio Siri jamaa alikua mzalendo Sana.

Na ukiona na mkataba wa bagamoyo kaukataa, ujue Kuna walakini
 
Miaka ya katibuni, baadhi ya watanzania na waafrika kwa ujumla, wamewehukia mikopo ya kutoka China. Tena wengine kufikia kuwadharau wahisani na wakopeshaji wetu wa asili ambao ni mataifa ya Ulaya na America.

Kwa ujinga tu, wengine wakafikia kuwaita hawa watoaji misaada na wakopeshaji wetu wa asili, yaani nchi za Ulaya na America, kuwa ni mabeberu wanaopora rasilimali za Afrika, na huku wakiongezea kuwa wamempata rafiki mpya, mwenye mapenzi mema na Afrika, Mchina.

Pamoja na Afrika kuelemewa na madeni makubwa toka nchi za Ulaya na America, haikuwahi kutokea wakopeshaji hao kuchukua vitega uchumi vya nchi mdaiwa, kama viwanja vya ndege au bandari, hata mara moja, kama anavyofanya Mchina.

Nadhani,memesikia, Airport ya Uganda imechukuliwa na wachina kwa sababu Uganda imeshindwa kulipa deni kwa wakati. Bandari ya Mombasa inanyemelewa kwa sababu hizo hizo. Airport na Shirika la umeme Zambia, vipo mbioni kuchukuliwa. Bandari ya Gambia imechukuliwa kwa sababu hizo hizo.

Hivi China, inapochukua vyanzo hivyo vikubwa vya mapato vya mataifa haya maskini, huo ndio upendo wao kwa Afrika au ni mbinu ya kuididimiza Afrika?

China inanufaika sana kutoka Afrika kuliko nchi za Afrika zinavyonufaishwa na China. Afrika limekuwa ndiyo soko kubwa la bidhaa zake duni na zisizo na ubora. Haijaridhika na hayo yote, sasa wanataka kuja moja kwa moja na kubeba hata kile kidogo ambacho nchi za Afrika inacho.

Kwangu mimi, China inaitumbukiza kwenye umaskini mkubwa Afrika kwa bidhaa zake duni. Waafrika kwa sababu ya umaskini, wanalazimika kununua bidha hizi duni za China ambazo ni aghali sana. Nasema ni aghali sana, kwa sababu, ukinunua kiatu toka China cha shilingi laki 1 kinadumu miezi 6, ukinunua kiatu toka Italy sh laki 2, kinadumu miaka 6, kipi ni aghali zaidi? Kiatu cha China kinachodumu miezi sita ni sawa unatumia sh 100,000÷6 kwa mwezi. Ina maana kila mwezi imekugharimu zaidi ya sh 16,000. Cha Italy, kilichodumu miaka 6 (miezi 72) ina maana kila mwezi imekugharimu 200,000÷72, sawa na sh 2,777. Na hiyo ipo kwenye magari, jenereta za umeme, na kila aina ya machine.

Bidhaa za China ni bei nafuu wakati unanunua, ukienda kwenye matumizi, bidhaa za China ni aghali sana.

Kama una kiwanda au shughuli yako inayotumia mashine mbalimbali, na unataka kufanya shughuli zako kwa uhakika, ziepuke sana bidhaa za China. Utafilisika, huku wachina wakitajirika bila ya kukuonea huruma.

Ukoloni wa Mchina utakuwa mbaya zaidi kuzidi hata biashara ya utumwa iliyofanywa na mwarabu. Mataifa ya Afrika yajihadhari sana Mchina. China inaiona Afrika kama ndilo bara litakaloifanya ibadilishe maisha ya wananchi wake, ambao wengi wapo kwenye umaskini mkubwa.
Umenena vema. Tumejitakia wenyewe kama Africa. Tumekuwa ni watu wa kutaka misaada na mikopo y hata pale tunapoweza kujisimamimia wenyewe. Tumebaki kuamini kwamba hatuwezi bila wao. Tunakopa blindly bila kujali athari zilizo mbele yetu na consequences zitokanazo na mikopo hiyo. Pia china wanatumia advantage za tamaa za baadhi ya viongozi wa kiafrika wasio na chembe ya aibu katika ku misuse hela za mikopo kwenye mambo yao binafsi. Hata hivyo China haina haki ya kuchukua vitega uchumi vya nchi maskini za kiafrika ndani ya nchi hizo. Waafrika tusikubali ukoloni huu na utapeli huu
 
Umenena kuna siku ndugai kapokelewa china na msafara plus watoto wazuri wa kichina yaani mapokezi ya vip, nadhani ajenda nyuma yake awatetee Bandari ya bagamoyo ipite, wachina wanajua Sana kuwamangungo watawala wa kiafrica yaani wanashangazwa wakienda china kusaini mikataba.
Wachina wanatoa sn rushwa
 
Ndie mfadhili wao Mkubwa kuuwa watu afrika,China,Urusi hawana humanity wala haki za binadamu.
Beberu aligoma kutoa pesa ya barabara kimara hadi walipwe fidia jiwe akagoma kuliko kulipa fidia bora akajenge Chato,mchina angetoa pesa.
Beberu ndie kimbilio la watu wote wanaoteswa na madikteta
Wazungu wanatutetea sn sisi watu weusi
 
Ccm na china ni ndugu wa damu tangu enzi.wanajiita China TANZANIA.Urafiki wetu kwao upo kwenye raslimali zetu.
Zhongzhong nio wakipewa kibali kimoja ukitumia kufanyia shughuli zingine nyingi.
 
Wachina wanatoa sn rushwa
Wachina waliamua mpaka kumwita Kikwete profesa, hata mwenyewe alisema kuwa alishangaa sana.

Kuna rafiki yangu alienda China kwaajili ya kusaini mkataba wa kutengenezwa mashine za kiwandani kwake, zilikuwa na thamani ya kama dola 1.2m. Anasema alishangaa namna alivyopokelewa. Airport alienda kupokelewa na maafisa wa kiwanda, wasichana 8 warembo, akapelekwa hoteli kubwa ya kifahari, na kisha akaambiwa kuwa kati ya wale wasichana 8, anaweza kuchagua yeyote anayetaka akae naye pale hotelini. Na kwamba, hata kama akitaka kuketewa mwingine tofauti kila siku, ingewezekana pia.

Mambo haya madogo madogo, ukiona yanafanyika, ujue wamekwishafanya utafiti, na kuona kuwa kwa mwafrika yana nguvu katika kufanya maamuzi. Ni viongozi wangapi wa Afrika wanafanyiwa hayo, na kisha kuwa vipofu katika maamuzi yao? Na kuna uwezekano mkubwa, wazungu hawafanyiwi hivyo vioja.
 
Wachina waliamua mpaka kumwita Kikwete profesa, hata mwenyewe alisema kuwa alishangaa sana.

Kuna rafiki yangu alienda China kwaajili ya kusaini mkataba wa kutengenezwa mashine za kiwandani kwake, zilikuwa na thamani ya kama dola 1.2m. Anasema alishangaa namna alivyopokelewa. Airport alienda kupokelewa na maafisa wa kiwanda, wasichana 8 warembo, akapelekwa hoteli kubwa ya kifahari, na kisha akaambiwa kuwa kati ya wale wasichana 8, anaweza kuchagua yeyote anayetaka akae naye pale hotelini. Na kwamba, hata kama akitaka kuketewa mwingine tofauti kila siku, ingewezekana pia.

Mambo haya madogo madogo, ukiona yanafanyika, ujue wamekwishafanya utafiti, na kuona kuwa kwa mwafrika yana nguvu katika kufanya maamuzi. Ni viongozi wangapi wa Afrika wanafanyiwa hayo, na kisha kuwa vipofu katika maamuzi yao? Na kuna uwezekano mkubwa, wazungu hawafanyiwi hivyo vioja.
Waafrica tukiitwa nyani tusichukie
 
Bila wao wakoloni weusi wangetugeuza bucha usiku na mchana,sema tu hofu ya The hague na kunyimwa misaada ndo kunawapunguza speed hawa wakoloni weusi wasimalize watu.
Bila wazungu, Afrika lingekuwa dimbwi la damu. Ni heri maradufu ubaya wa mzungu kuliko wema wa kiongozi mnafiki mwafrika.
 
Umeona, eh? Akina Magufuli wanapenda sana China kwa vile hata wakichinja watu wao, Wachina wanakauka tu. Hawasemi kitu. Wana policy inaitwa "non-interference"! Na Africa ilivyo na madikteta!
Viongozi wa africa wanaipenda China vile hawakemei maovu Yao Matokeo Sasa Africa inaanzwa kuuzwa kihalali in the name of mikopo
 
Back
Top Bottom