Miaka nenda rudi ya madeni, hakuna Ulaya au Amerika walipotaifisha mali

Are you serious?
====
SOMA hapa
Hilo siyo deni la Serikali ya US kwa Serikali ya China. Hizo ni US government treasury bills zilizonunuliwa na makampuni ya China. Hata wewe ukiwa na pesa, unaweza kununua treasury bills za Uas, baada ya hapo utakuwa unaidai serikali ya US.

Hii biashara ya kununua government treasury bills, hata hapa kwetu, nadhani ulianzishwa wakati wa Jakaya, ingawa waliokuwa wakifaidika na hiyo biashara ni wahindi. Lakini ni risk free business. Na ina faida kuliko kuweka pesa bank. Kwa hiyo Wachina wanashindana hasa, kununua US treasury bills ili kujitengenezea faida ya uhakika.
 
Picha kamili ya mchina inaonekana kwa wawekezaji na wakandarasi wa kichina tulio nao. Kama wana uwezo wa kupiga na kudhulumu wafanyakazi bila oga wowote mnategemea nini?

Wachina wanakubalika kwa viongozi wa kiafrica kwa sababu ni watoaji na wapokeaji rushwa wazuri nje ya mazingira ya kwao. Na hii ni strategy na sera ya china kama nchi kwa ajili ya kushinda tenda na kukamata nchi za ulimwengu sehemu ambayo rushwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.

INGEPENDEZA UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO UKAFANYIWA UPEMBUZI YAKINIFU TENA KWA KULETA WATALAAM MAKINI ILI KUEPUKA FEDHEHA YA KUWA KICHEKO DUNIANI NA WAJUKUU NA VITUKUU WETU
Ukaitaka ufe maskini, fanya kazi kwenye kampuni za Wachina maisha yako yote.
 
Miaka ya karibuni, baadhi ya watanzania na waafrika kwa ujumla, wamewehukia mikopo ya kutoka China. Tena wengine kufikia kuwadharau wahisani na wakopeshaji wetu wa asili ambao ni mataifa ya Ulaya na America.

Kwa ujinga tu, wengine wakafikia kuwaita hawa watoaji misaada na wakopeshaji wetu wa asili, yaani nchi za Ulaya na America, kuwa ni mabeberu wanaopora rasilimali za Afrika, na huku wakiongezea kuwa wamempata rafiki mpya, mwenye mapenzi mema na Afrika, Mchina.

Pamoja na Afrika kuelemewa na madeni makubwa toka nchi za Ulaya na America, haikuwahi kutokea wakopeshaji hao kuchukua vitega uchumi vya nchi mdaiwa, kama viwanja vya ndege au bandari, hata mara moja, kama anavyofanya Mchina.

Nadhani,memesikia, Airport ya Uganda imechukuliwa na wachina kwa sababu Uganda imeshindwa kulipa deni kwa wakati. Bandari ya Mombasa inanyemelewa kwa sababu hizo hizo. Airport na Shirika la umeme Zambia, vipo mbioni kuchukuliwa. Bandari ya Gambia imechukuliwa kwa sababu hizo hizo.

Hivi China, inapochukua vyanzo hivyo vikubwa vya mapato vya mataifa haya maskini, huo ndio upendo wao kwa Afrika au ni mbinu ya kuididimiza Afrika?

China inanufaika sana kutoka Afrika kuliko nchi za Afrika zinavyonufaishwa na China. Afrika limekuwa ndiyo soko kubwa la bidhaa zake duni na zisizo na ubora. Haijaridhika na hayo yote, sasa wanataka kuja moja kwa moja na kubeba hata kile kidogo ambacho nchi za Afrika inacho.

Kwangu mimi, China inaitumbukiza kwenye umaskini mkubwa Afrika kwa bidhaa zake duni. Waafrika kwa sababu ya umaskini, wanalazimika kununua bidha hizi duni za China ambazo ni aghali sana. Nasema ni aghali sana, kwa sababu, ukinunua kiatu toka China cha shilingi laki 1 kinadumu miezi 6, ukinunua kiatu toka Italy sh laki 2, kinadumu miaka 6, kipi ni aghali zaidi? Kiatu cha China kinachodumu miezi sita ni sawa unatumia sh 100,000÷6 kwa mwezi. Ina maana kila mwezi imekugharimu zaidi ya sh 16,000. Cha Italy, kilichodumu miaka 6 (miezi 72) ina maana kila mwezi imekugharimu 200,000÷72, sawa na sh 2,777. Na hiyo ipo kwenye magari, jenereta za umeme, na kila aina ya machine.

Bidhaa za China ni bei nafuu wakati unanunua, ukienda kwenye matumizi, bidhaa za China ni aghali sana.

Kama una kiwanda au shughuli yako inayotumia mashine mbalimbali, na unataka kufanya shughuli zako kwa uhakika, ziepuke sana bidhaa za China. Utafilisika, huku wachina wakitajirika bila ya kukuonea huruma.

Ukoloni wa Mchina utakuwa mbaya zaidi kuzidi hata biashara ya utumwa iliyofanywa na mwarabu. Mataifa ya Afrika yajihadhari sana Mchina. China inaiona Afrika kama ndilo bara litakaloifanya ibadilishe maisha ya wananchi wake, ambao wengi wapo kwenye umaskini mkubwa.
Hawa mbwa sio wa kucheka nao
 
Inajua kitu wanaita ku freeze assets? Wanafanya sana mchezo huo. Waulize waafighanistan na wavenezuela watakwambia. Ni zuluma juu ya zulima.
 
Naona lawama zetu zote tumeamua kuzielekeza kwa mchina sasa.
Naona wamesahau anayesaini hiyo mikataba ni mwafrica mwenyewe, tuache kulia lia na kujifanya victim wa kila kitu, lakini kama mifereji mbele ya nyumba zetu imejaa mbu na mavi na hatuwezi kusafisha wenyewe mpaka halmashauri zetu maskini ambazo hazina hata fagio zije zisafishe sina matumaini kama tutabadilika
 
Inajua kitu wanaita ku freeze assets? Wanafanya sana mchezo huo. Waulize waafighanistan na wavenezuela watakwambia. Ni zuluma juu ya zulima.
Ndio system iliyopo na capitalist wote wanaitumia , waulize Greece au Argentina, tatizo culture ya kulipa hatuna tumezoea kuchukua mikopo tukijua kabisa hatuna mpango wa kulipa na sometimes hatujui hata kilichoandikwa kwenye contract, na hiyo ipo mpaka kwa raia wa kawaida bongo, na usichukue pesa za watu then kwenye kulipa ukaita zuluma
 
Mchina hana mbinu ya kuididimiza Africa bali anataka kuwa na vyanzo vingi africa na sehemu nyingi kwa ajili ya chakula cha raia wake huko kwani ardhi yao kubwa wamewekeza kutanua miji na kujenga viwanda vikubwa sana

Sasa mashamba yanahitajika na sehemu ya kusafirishia mazao hayo

Ndio maana Think tank wa huko wakaja na mkakati wa kuwakopa mafala kwa kuwasainisha kwa kupewa nao kiasi kikubwa cha hela kama asante kama watafanikisha kusaini mkataba wa kupora ardhi

Mtu mweusi akaanguka kalamu kwa kuona hizo hongo kwenye acc yake bila kujali anauza ardhi ya nchi

Sasa mchina atamiliki bandari na airports halafu ardhi anakodi kwa miaka 30 au zaidi
Mtu mweusi atalimishwa sana na mazao yatapelekwa China mtake msitake

Huu ndio mkakati na strategy zao

Kama inauma kunywa maji tu hali ndio hii

Walisema mzungu masharti yake analazimisha na ushoga
Haya sasa
Mungu wabariki mabeberu
 
Naona wamesahau anayesaini hiyo mikataba ni mwafrica mwenyewe, tuache kulia lia na kujifanya victim wa kila kitu, lakini kama mifereji mbele ya nyumba zetu imejaa mbu na mavi na hatuwezi kusafisha wenyewe mpaka halmashauri zetu maskini ambazo hazina hata fagio zije zisafishe sina matumaini kama tutabadilika
Madikteta ndio usaini wananchi tunashirkishwa kwenye ulipaji.
Jiwe kakopa zaidi ya tilioni 52 kilichofanyika akionekani.Hayupo deni katuachia sisi, maisha magumu vitu bei juu tunaokamuliwa ni sisi kulipa deni,ye hayupo.
 
Ndio system iliyopo na capitalist wote wanaitumia , waulize Greece au Argentina, tatizo culture ya kulipa hatuna tumezoea kuchukua mikopo tukijua kabisa hatuna mpango wa kulipa na sometimes hatujui hata kilichoandikwa kwenye contract, na hiyo ipo mpaka kwa raia wa kawaida bongo, na usichukue pesa za watu then kwenye kulipa ukaita zuluma
Ni zuluma kwa sababu sababu zilizotolewa na US kiasi cha kushikilia mali za Venezuela zilikuwa hazihusiani na mambo ya mkopo. US ilitaka kuweka kibara wao Guido kuwa rais wa Venezuela wananchi wa nchi hiyo wakakataa, kuona hivyo US akashikilia mali na fedha za nchi hiyo kiharamia. Vivo hivyo UK alishikilia madini ya Venezuela kisa eti Guido kanyimwa urais, hukukua na suala la mikopo hapo, ni zuluma.
 
Asante kwa mchango mrefu usio na ukweki wowote.

1) Ufahamu kuwa mpaka sasa nchi inayoongoza kutafuta na kuvutia wawekezaji wa kigeni kutoka Ulaya na America, ni China. Ni hayo makampuni ya Ulaya na America yaliyowekeza China kwa sababu ya cheap labour na huge market ya China, ndiyo yanayotengeneza bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu, na masoko yao makubwa ni huko huko kwao, Ulaya na America.

2) Makampuni ya China yanayomilikiwa na wachina wenyewe, ndiyo yanayotengeneza bidhaa duni, ambazo zaidi ni za kuiga, na wanaziuza zaidi Afrika.

3) Wakati viongozi wa China kila wakati wapo Ulaya na America kutafuta wawekezaji, Waafrika wanaamini kuwa Wachina wana uwezo mkubwa wa kuwekeza na wanaweza kubadilisha uchumi wa Afrika

4) Ni uwongo mkubwa kuwa eti ili upate maendeleo unahitaji mfumo wa kidikteta kuongoza nchi. Ipo mifano mingi kuthibitisha hilo. Kama udikteta ungekuwa unasababisha nchi kuwa tajiri, North Korea ingekuwa tajiri sana, Cuba ingekuwa tajiri sana, Togo ingekuwa tajiri sana, Burundi ingekuwa tajiri sana. Yatazame mataifa yenye demokrasia kubwa kama Botswana. Linganisha South Korea yenye demokrasia vs North Korea, China vs Japan, Singapore, Hong Kong na Malaysia. China, pamoja na uwekezaji mkubwa wa mataifa ya kigeni, bado ni nchi inayoendelea. Ni nchi ya 89 kwenye human development. Pato lake kubwa linatokana na uwingi wa watu na ukubwa wa nchi lakini siyo quality of living. Ukienda kwenye quality of living, China is in a developing country category. Ndiyo maana, hata China yenyewe ililikataa pendekezo la US kwenye UN security council lililotaka nchi ya China iingizwe kwenye mataifa tajiri. Waziri Mkuu wa China alikataa akieleza kuwa wananchi wake wengi bado wanaishi kwenye umaskini mkubwa.
Ahsante na ww kwa porojo zisizokuwa na ukweli.
1)Kutafta wawekezaji sio jambo baya hukuza uchumi wa nchi.Hayo makampuni ya Ulaya yalyowekeza China yanatumia skilled cheap labours wa Kichina.Hiyo inajulisha ya kuwa China Ina watu wenye vipawa na akili.
2)Kusema China inatengeneza bidhaa duni kwa makampuni yake ya kizalendo ni UONGO MKUBWA NA UONGO DHAMBI tuanze na makampuni ya simu Oppo,xiamo, Huawei,Infinix , Tecno zote ni Chinese made tena Oppo na xiamo hizo simu zimeingia ktk simu Tano bora duniani ukianzia Samsung ikija iphone ikifuatiwa Huawei kesha oppo na xiamo.
Waundaji wa miundombinu bora ya reli na majengo ni china .
Utasemaje china anaunda vitu feki?
Je makampuni ya kizungu yanawekezaje wa watu wanaounda vitu feki?
3) Duniani takriban asilimia 63 ya vitu vya viwandani vinazalishwa na China bidhaa za high standard zikuuzwa mataifa ya ulimwengu wa kwanza na vya medium na low standards vikiuzwa mataifa maskini hususan Afrika na Asia.
4)Suala la China wananchi wake kuwa na low standard of living ni UONGo ndio kunachomfanya China akatae kuunganishwa na developed nations ni ile kukwepa ushuru MKUBWA wa exportation kwasababu mataifa yaliyoendelea hulipa ushuru tofauti na mataifa yanayoendelea.Ila China Ina high living standards fuatilia documentaries zao tena zinarushwa na wazungu wenyewe.
MWISHO BILA MCHINA AFRIKA TUSINGEKUA HAPA
 
Bila wazungu, Afrika lingekuwa dimbwi la damu. Ni heri maradufu ubaya wa mzungu kuliko wema wa kiongozi mnafiki mwafrika.
MuNGu Anakuona kaka.
Hii Dunia imeharibiwa na mzungu.
Vita mashariki ya kati,upandikizaji magonjwa,upandikizaji ugaidi ,unyonyaji kupitia mikopo.
Kopa mashirika ya kizungu ushindwe kulipa maliasili zako zinawahusu.
Kwan hatujaona maafa yalosababishwa na wazungu Duniani?
 
Unapokopa jua kulipa.
China ana haki ya kufanya atakacho kwasababu akati mnaenda kukopa hamkulazimishwa.
Msilaumu watu kwa umaskini wenu unaotokana na ufinyu wenu wa uwajibikaji.
Mzungu mlisema anawaekea masharti nyonyaji sasa mnamlaumu MCHINA kutaifisha Mali zenu.
We fikiria mtu kasamehe mataifa 38 mikopo alokopesha bado unataka awe na huruma kiasi gani !?
Afrika mtakapojua kuwajibika vizuri madarakani hz porojo mtaziacha.
Miaka ya karibuni, baadhi ya watanzania na waafrika kwa ujumla, wamewehukia mikopo ya kutoka China. Tena wengine kufikia kuwadharau wahisani na wakopeshaji wetu wa asili ambao ni mataifa ya Ulaya na America.

Kwa ujinga tu, wengine wakafikia kuwaita hawa watoaji misaada na wakopeshaji wetu wa asili, yaani nchi za Ulaya na America, kuwa ni mabeberu wanaopora rasilimali za Afrika, na huku wakiongezea kuwa wamempata rafiki mpya, mwenye mapenzi mema na Afrika, Mchina.

Pamoja na Afrika kuelemewa na madeni makubwa toka nchi za Ulaya na America, haikuwahi kutokea wakopeshaji hao kuchukua vitega uchumi vya nchi mdaiwa, kama viwanja vya ndege au bandari, hata mara moja, kama anavyofanya Mchina.

Nadhani,memesikia, Airport ya Uganda imechukuliwa na wachina kwa sababu Uganda imeshindwa kulipa deni kwa wakati. Bandari ya Mombasa inanyemelewa kwa sababu hizo hizo. Airport na Shirika la umeme Zambia, vipo mbioni kuchukuliwa. Bandari ya Gambia imechukuliwa kwa sababu hizo hizo.

Hivi China, inapochukua vyanzo hivyo vikubwa vya mapato vya mataifa haya maskini, huo ndio upendo wao kwa Afrika au ni mbinu ya kuididimiza Afrika?

China inanufaika sana kutoka Afrika kuliko nchi za Afrika zinavyonufaishwa na China. Afrika limekuwa ndiyo soko kubwa la bidhaa zake duni na zisizo na ubora. Haijaridhika na hayo yote, sasa wanataka kuja moja kwa moja na kubeba hata kile kidogo ambacho nchi za Afrika inacho.

Kwangu mimi, China inaitumbukiza kwenye umaskini mkubwa Afrika kwa bidhaa zake duni. Waafrika kwa sababu ya umaskini, wanalazimika kununua bidha hizi duni za China ambazo ni aghali sana. Nasema ni aghali sana, kwa sababu, ukinunua kiatu toka China cha shilingi laki 1 kinadumu miezi 6, ukinunua kiatu toka Italy sh laki 2, kinadumu miaka 6, kipi ni aghali zaidi? Kiatu cha China kinachodumu miezi sita ni sawa unatumia sh 100,000÷6 kwa mwezi. Ina maana kila mwezi imekugharimu zaidi ya sh 16,000. Cha Italy, kilichodumu miaka 6 (miezi 72) ina maana kila mwezi imekugharimu 200,000÷72, sawa na sh 2,777. Na hiyo ipo kwenye magari, jenereta za umeme, na kila aina ya machine.

Bidhaa za China ni bei nafuu wakati unanunua, ukienda kwenye matumizi, bidhaa za China ni aghali sana.

Kama una kiwanda au shughuli yako inayotumia mashine mbalimbali, na unataka kufanya shughuli zako kwa uhakika, ziepuke sana bidhaa za China. Utafilisika, huku wachina wakitajirika bila ya kukuonea huruma.

Ukoloni wa Mchina utakuwa mbaya zaidi kuzidi hata biashara ya utumwa iliyofanywa na mwarabu. Mataifa ya Afrika yajihadhari sana Mchina. China inaiona Afrika kama ndilo bara litakaloifanya ibadilishe maisha ya wananchi wake, ambao wengi wapo kwenye umaskini mkubwa.
 
MuNGu Anakuona kaka.
Hii Dunia imeharibiwa na mzungu.
Vita mashariki ya kati,upandikizaji magonjwa,upandikizaji ugaidi ,unyonyaji kupitia mikopo.
Kopa mashirika ya kizungu ushindwe kulipa maliasili zako zinawahusu.
Kwan hatujaona maafa yalosababishwa na wazungu Duniani?
Kila kitu mnatafuta wa kumlaumu, ugaidi si wanawatumia nyie wenyewe then mnaishia kulipuana kwa ukabila na chuki? mikopo si tunakopa wenyewe na mafisadi kula kila kitu au nadanganya? yes mzungu anahusika lakini na sisi wenyewe ni tatizo kubwa zaidi, hakuna maji wala umeme lakini viongozi wote mpaka wa halmashauri wanatembelea VX 8 za milion 400, kiongozi anajenga apartment 100 na hana biashara yeyote na hakuna anayehoji? tatizo ni sisi wenyewe tuache kutafuta visingizio na tubadilike
 
Kaka sijakataa km sisi hatuna tatizo.
Km umeona kuna quote yangu Moja nilisema "Kama tutakua wawajibikaji tutaacha lawama".
ILa nachompinga huyu jamaa ni yeye kusema hii dunia ipo salama kwasababu mzungu yupo.Ndio maana nikampa hizo facts.
Nimelenga kumrekebisha huyo msujudia wazungu.
Ila hujakosea ulichosema.
 
Fake news. China haikuchukua Entebbe Airport. Halafu uwe unasoma historia. Hao Wazungu unaowasifu walikuwa wanafanya hivyo, mpaka walipogundua kuongeza riba ni bora zaidi kuliko kukamata rasilmali. Mfereji wa Suez (Suez canal) huko Misri uliwahi kuhodhiwa na Waingereza na Wafaransa kutokana na deni. Na hata wakalazimisha Waziri wa fedha wa Misri awe Mwingereza kuhakikisha deni lao linarudi. Hii ni moja ya sababu wanajeshi wakapindua serikali ya mfalme akaja Nasser, naye akataifisha Suez. Hapo Wazungu wakamtangazia vita mwaka 1956 wakiungana Waingereza, Wafaransa na Waisraeli!
 
Back
Top Bottom