Miaka Mitatu sina Mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka Mitatu sina Mtoto

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ramos, May 13, 2010.

 1. R

  Ramos JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hi wanaJF
  Mimi ni mwanaume, nimeoa miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa nina miaka 32 ya umri. Mimi na mke wangu hatuna mtoto kwa miaka hiyo mitatu. Tatizo ni kuwa siku hizi nimeanza kuingiwa na kaushawishi ka kutafuta mtoto nje ya ndoa. Najua ni hatari kiafya lakini najishawishi kuwa nitafanya taratibu zote za kuwa mwangalifu. Siku zote kila ninapowaza hilo la kwenda nje ya ndoa nakumbuka siku ile pale kanisani nilipoahidi mbele ya mashahidi, mbele ya padre na mbele ya mungu kumpenda na kumlinda mke wangu katika SHIDA na raha. Kinachonishangaza ni kuwa hiyo consiousness siku hizi inapungua, nazidiwa na ushawishi. Nikisikia rafiki zangu wakiongelea watoto wao, nikisikia stori kuwa kuna watu hawakuwa na watoto kwenye ndoa, wakajawapata nje, na nikiwaza kuwa nina kazi nzuri kidogo itakayonofanya pengine niwe na raslimali zitakazohitaji kurithishwa baadae najihisi kama nitashawishika. Jingine kubwa ni kuwa mke wangu nae ni mkubwa kidogo (miaka 31) na siku zinakwenda.

  Tulishachukua hatua ya kucheki kama tuna matatizo kiafya, lakini sote hatukuonekana kuwa na matatizo, ingawa ni katika vipimo vile vya kawaida hospitali zetu ziliweza kuhandle (najua kuna vipimo complex nje ya nchi ambavyo uchumi hauturuhusu kuvipata). mi na mke wangu tunaheshimiana sana, tunapendana sana lakini naogopa na sijawahi kuonyesha hali yoyote kwake kuwa nawaza kutafuta mtoto nje.

  WanaJf naombeni ushauri wenu...
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Kuna watu wanapata watoto wakiwa na 40 na kuendelea - Mimi sio malaika (nina mtoto nje ya ndoa pia), lakini na ndani ya ndoa ninao wawili - Tatizo kubwa ni kwamba ukitoka nje ya ndoa unaweza usirudi! Also unaweza kutoka na bado uka-end up hupati mtoto : Hii ni Game of Chance! Kwahiyo ni vyema ukaendelea kuwa na uvumilivu na kutafuta ushauri wa Madaktari wnegi zaidi - Kwa ushauri wangu, mpaka pale Daktari atakapowahakikishieni kuwa HAMUWEZI kupata mtoto/watoto ndio ufanye yafuatayo:

  1. Chukua mtoto kutoka nyumba za watoto (orphanage) = Adopt
  2. Jadili na mke wako kwa kina kuwa unadhamira ya kutoka nje na aridhie (ni ngumu sana hapa - hasa kwa wakristo)
  3. Ishi hivyo milele mpaka mwisho wa maisha (waweza kuwachukua watoto wa ndugu na ukakaa nao kama wanao)

  Pole sana - Hii hali huwa ni mtihani mkubwa na inahitaji uvumilivu wa kupita kiasi
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,729
  Likes Received: 8,302
  Trophy Points: 280
  Pole ndugu...sina ushauri ila nitawaweka mikononi mwa Mungu na Mungu atawasaidia!
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Usikate tamaa ndugu yangu kama huna tatizo mie nina watu ambao ninawafahau in and out walikaa miaka 20 ya ndoa wakaja pata watoto 2 kwa kuaatana waswahiliwanasema j3 na j4 baada ya hapo wakuzaa tena hadi walipo tangulia mbele ya haki kwa hiyo usikate tamaa muombe sana mungu wako atasikia kilio chako na wala hawakutoka nje yz ndoa zao
   
 5. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pole sana ndugu yangu;
  Lakini mi naona miaka mitatu ni kidogo mno kuogopa...
  Pia mmepima nyote mkajikuta mko Ok...Je unajuaje km mwenye tatizo(iwapo lipo na vipimo havikugundua) ni wewe au mkeo?

  Imagine,unasafiri kwa miezi miwili, unaporudi unamkuta mkeo ana mimba ya mwezi mmoja na nusu...Utalipokeje hilo...?mtoto utamtunza au utamkataa?
  Vumilia walau ifike mitano au sita...Pia fanya utambuzi wa nani ana tatizo,maana unaweza kutafuta ugonjwa badala ya mtoto
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  KARIBU SANA jf NDUGU RAMOS, maana naona weye ni mgeni!
  Pole sana ndugu yangu!...
  Usifikie uamuzi huo unaowaza,(ushauri wa Baba Enock-no-2 hapo juu) ni hatari!...Unaweza ukakumbana na matatizo makubwa sana huko mpaka ukajuta.(
  Mi naona bado kuna nafasi ya kutosha kwenu, hasa kwa upande wa TIBA na ushauri-nasaha!
   
 7. JS

  JS JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kaka Ramos, kwanza karibu JF waonekana bado mgeni jukwaani hapa.
  Pili, kutoka nje ya ndoa si sulhisho kaka yangu uvumilivu ndo tija. Nina story kama hiyo ya kwako ya watu wa karibu sana kwangu. wamekaa kwenye ndoa miaka 6 bila mtoto na jitihada zikawa zinaendelea. mama anashika ujauzito miezi mbili tatu hata miezi nane zikawa zinatoka hivyo hivyo. lakini mume aliendelea kuwa mwaminifu kwa mkewe na mvumilivu pia. mwishowe mwaka jana mungu kawaajalia na furaha ndani ya nyumba imeongezeka.

  Tamaa ziko sana tena sana kwa mtu kama wewe unayehitaji mtoto hasa lakini nikuambie kitu hata ukisema utoke nje ukapate mtoto hutamfurahia kihivyo kama ambavyo ungempata na mkeo unayeishi naye for the rest of your life.

  cha msingi muombe mungu akuepushie na mawazo hayo endelea kuwa mwaminifu na kama mungu hakuwajalia basi adopt a kid from orphanage. it is way better kuliko kutoka nje ya ndoa.

  usiwe na simanzi pia live your life to the fullest my brother with your lovely wife and god will bless you abundantly.

  TAKE CARE
   
 8. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu. Naelewa unavyojisikia. Sisi pia tulikaa miaka miaka mitatu bila mtoto ingawa tulikuwa tunahitaji mtoto. Actually ni almost exactly situation kama yako kwani hata sisi sote tulikuwa medically okay. Kimsingi hakuna kitu cha tofauti sana tulichofanya zaidi ya kusubiri na kwa kweli baadae Mungu akajibu maombi yetu.

  Kukosa mtoto inaweza kusababishwa na mambo mengi tu.... inawezekana fertilization inatokea lakini 'mimba' inashindwa kutunga au fertilisation haitokei kabisa. Sasa ni vema kuwa clear ni tatizo gani linalowasibu. Jaribuni kupata ushauri zaidi wa kitabibu. Kama mmekwenda kwa daktari mmoja tu jaribuni kwenda kwa mwingine pia. Ni kweli pia kuna matatizo mengine madaktari bado hawana utaalamu wa kuweza kuyatatua.

  Kama unaamini katika mungu mimi ningekushauri uendelee kuwa mvumilivu hadi hapo Mungu atakapo amua kukupa mtoto. Watoto wa nje ya ndoa katika umri wako nadhani sio muafaka. Bado hujachelewa.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mbona 32 ni kijana mno kuanza kuingia wasi wasi kuhusu mtoto?

  hebu kwanza chana life na mkeo kwa mapenzi ya raha. ukiona lazima sasa uwe na mtoto ka adopt mmoja au kaa na mtoto wa jamaa ( am sure wapo maskini sana ambe wangefurahi kupokewa mtoto)

  ukianza kutafuta zinaa nje huko ndio unatoa baraka zote kwenye ndoa yako.

  fikiria hivi: utakapozaa mtoto nje unakusudia kumtambulisha kwa mkeo au? kama ni ndio, jee yeye akitafuta mwanamme akazaa mtoto utajiskiaje? utalea mtoto huyo?
   
 10. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  watoto ni zawadi toka kwa Mungu, Mungu atakupatia watoto. ila kumbuka, kuna wakati mwingine kizazi huwa kinazibwa na shetani, utaenda hospital na hutaona tatizo, kumbe adui shetani kafunga kizazi... watu wengi wanakuwa na wivu na pia kizazi ni dili kwa watu wengine kichawi, wanakufunga halafu wewe ukiwa unaumia moyo uchawi wao unazidi kupata nguvu wanakuwa wanaulisha. kuna watu wengi nawafahamu walikuwa na tatizo kama hili, walipookoka wakavunja nguvu za shetani, wana watoto mapacha. ninaye ndugu yangu mwaka jana alihamia kanisa moja linaitwa siloam kule mbezi beach makonde, aliombewa na sasahivi ana mtoto wa kiume baada ya kukaa miaka kumi bila mtoto huku akisutwa na mawifi na ndugu. pia, kuna watu wengiiii nawafahamu, walikuwa na tatizo kama lako, wameenda kwenye mafundisho ya mchungaji Gwajima kule ubungo, kwasasa nasikia amehamia kawe, wamepata watoto tena mapacha...NAOMBA NIKWAMBIE KUWA, SISEMI TOKA HEWANI, naongea kitu cha kweli kabisa, kweli kabisa. Mungu ana nguvu ya kufungua vizazi vilivyofunga...jua kuwa shetani ana nguvu kuliko waganga wa hospital hivyo ni kitu cha kawaida kuona mtu anaumwa kwasababu shetani kafanya kitu na akienda hospital hawaoni ugonjwa wowote. pamoja na yote hayo, Mungu wetu ana nguvu kuliko shetani, amemshinda shetani, nguvu ya Jina la Yesu inavunja kila kifungo alichoweka shetani, I tell you, kama kweli una tatizo, nakushauri nenda pale siloam mbezi beach makonde, nenda pale kwa Gwajima kawe, nenda efatha etc, UOKOKE, MKABIDHI YESU MAISHA YAKO, NAYE ATAKUPATIA WATOTO.

  Neno la Mungu linasema, Mungu huweka nyumbani mwake mwanamke tasa ili awe mama wa watoto wenye furaha, pia wale wamtumainio Bwana Mungu ameahidi kuwa atawapatia watoto, hakutakuwa na mwenye kuharibu mimba wala aliye tasa....ukimpa Yesu maisha yako, ndo hayo yatatokea kwasababu utakuwa umejikabidhi kwake...kama hautampa maisha yako, utakuwa chini ya shetani na mwishowe atafunga kabisa kizazi, na miaka ndo inaenda....wala usipate shida ndugu yangu, usipoteze muda, chukua ushauri huu niiliokupa, hata kama hauamini basi jaribu hata kujaribu tu, ukiona mimi nimesema uongo basi nishitaki mimi pamoja na Mungu aliyeahidi katika Neno lake....I assure you, utapata jibu kama utaenda ukiwa na nia na ufahamu huu, Mungu akusaidie..Mungu akusaidie.
   
 11. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #11
  May 13, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ramos, pole sana kwa hii hali. najua siyo rahisi kwa wanandoa kukubali kuishi bila watoto. Ngoja nikuonye kabla ya ushauri, huko nje ya ndoa unaenda kutafuta mengine sasa. kama umeshaambiwa wote hamna tatizo sasa huko nje unaenda kutafuta nini? hivi hii hali ya siku hizi huogopi hata kuwaza kwenda nje ya ndoa? unaweza kweli ukapata mtoto lakini ukapata na magonjwa ambayo yatakufanya usifaidi hata kuishi na huyo mtoto unayemtafuta. Utajisikiaje mkeo naye akipatwa na vishawishi kama vyako na kutafuta mtoto nje ya ndoa? maana inawezekana pia akajaribu nje na akapata mtoto.
  Majaribu yapo, na hatuna jinsi ya kufanya tusiingie majaribuni. Ni kazi kwako kama Mkristo kuongea na Mungu wako akuepushe na hivyo vishawishi. Tena umkemee kabisa huyo shetani ashindwe kwa Jina la Yesu! Unakumbuka Sara na Abraham walipata mtoto wakiwa na umri gani? Muombe Mungu, hakuna linaloshindikana kwake.
  All the best
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  May 13, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mmh,miaka mitatu tu umeshaanza kutoka nje ya ndoa?kazi kweli kweli.kwani mlioana kwa lengo la kupata watoto bila nyie kupendana?watoto ni majaliwa hata kama hamtapata mnatakiwa kubaki waaminifu milele kwenye penzi lenu.What if tatizo ni wewe,utatembea na wangapi?
   
 13. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #13
  May 13, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mungu ninayemjua mimi yupo kila kanisa. kuhamia huko unakokusema sio solution ya kupata mtoto. anachotakiwa ni Kumwamini Mungu wake, kiukweli na kumlilia, atafanikiwa tu. Mwana wa Mungu, unafahamu kuna makanisa mengine pia yanasaidia watu kupata watoto ambao wanatoka kwa shetani?
  Kuwa mwangalifu sana kwa hili Ramos, utashitukia unapata mtoto toka kwa shetani badala ya kutoka kwa Mungu.
   
 14. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mimi sijasema Mungu anapatikana kwenye hayo makanisa peke yake, actually mimi mwenyewe siko kwenye hayo makanisa, hapa nilikuwa natoa jambo ambalo nililishuhudia, na si vibaya kuwaambia watu wengine wajaribu. wewe hauna tatizo ndo maana unafikiri kila mtu tu anaweza kuomba akafanikiwa popote pale, subiri yakukute ndo utajua kuwa, haya makanisa ni tofauti. napenda kukurekebisha kitu kimoja, kuna myth moja watu mnasema kuwa watu wakiokoka wanapata watoto toka kwa shetani mkimaanisha kuwa walokole wanawapa mimba huko kanisani....msichume dhambi bureeee. mimi nilikuwa nampa ushauri ajaribu, akishindwa si atakuja kwenye ushauri wako wewe, tatizo liko wapi, kama anatatizo atafanya nilichomwambia, wewe mwenye shetani ndani ya moyo wako umeamua kutumika kumkatisha tamaa kuwa akienda kanisani nilikomwambia atapata watoto toka kwa shetani, uyo shetani unafanya naye kazi? ninao uwezo hata wa kumpa namba ya simu ya mtu niliyetoa ushuhuda hapo juu ili amwulize amtembelee na akaona hao watoto ninaosema. you people won't learn anything mpaka pale mtakapokutana na tatizo, ndo mtajua kuwa , sio makanisa yote yana Mungu, mengine ni dini tu, including myth uliyo nayo wewe kuwa, aombe Mungu popote tu atafanikiwa...unafikiri miaka yote mitatu atakuwa hajaomba, hebu mwulize kama hajaomba miaka yote hiyo? sasa ni ushauri gani huo unampa mwenzio? wait for your turn when you will be in his position in some way or another.
   
 15. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 500
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Pole sana Ramos, lakini bado nyote mna nafasi ya kupata watoto. Umri wa mkeo hata akipata mtoto miaka mitatu baadaye ataweza kuzaa bila shida.
  Lakini nakupongeza kwa kuweka wazi tatizo lako, naamini jamvini utapata ushauri tofauti tofauti na hatimaye kuangalia nini kinakufaa.
  Mchango wako mimi utakuwa na mtizamo wa kiimani kwa kiasi. Kwa vile wewe ni muumini wa kikristo, na kama unavyojua wakristo hawaruhusiwi kuwa na ndoa zaidi ya moja, jambo unalolifanya halina baraka mbele ya Mungu. Nakuhakikishia furaha ya kupata mtoto nje ya ndoa yako kama itatokea haitadumu hata wiki moja, zaidi zaidi roho itaanza kukusuta hata kabla ya mtoto kuzaliwa. Hebu imagine mke wako ambaye mwenyewe umekiri unampenda, anagundua kuwa umevunja kiapo cha ndoa ili kutafuta mtoto, unajua kusononeka kwake tu ni laana tosha kwako???
  Kama walivyochangia wenzangu, la msingi ni kusimama kwenye imani, mtegemee Mungu na endelea kupata ushauri kutoka kwa madaktari. Muda uliokaa si mrefu wa kukataa tamaa hata kwa kuhangaika kwa madaktari tofauti.
  Ningekushauri ufunge ili wazo la kutafuta mtoto nje ya ndoa likutoke. Mungu akutangulie.
   
 16. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  afunge kabisa wazo la kutafuta mtoto nje, akifanya hivyo na mkewe naye ataamua kutafuta mtoto nje, mtaishia wapi? jueni ya kuwa watoto ni zawadi toka kwa Mungu, kama mtu hajamheshimu Mungu, nikimaanisha kuwa ameamua kufikiri kuwa akiwa kwenye ndoa Mungu hana uwezo wa kumpatia mtoto akaamua kwenda nje, inawezekana Mungu akaamua kumfunga kabisa kwasababu anakuwa amemsaliti sana kwa kwenda nje ya ndoa, ni kumtukana Mungu kuwa kama ataendelea kuvumilia ktk ndoa hiyo bila kutoka nje ya ndoa Mungu hana uwezo kumpatia mtoto ktk hali hiyohiyo aliyokuwa nayo.

  nakushauri kwa upendo wa Jina la Yesu, nenda kwenye ayo makanisa niliyokwambia, utapata jibu. nenda kwenye makanisa mengine mengi tu wanayoombea watu, jaribu utapata jibu. kama hauamini basi jaribu tu. Mungu anaweza na hategemei kuwa utamwona kama hawezi.....Mungu anachukia sana watu walioko kwenye ndoa wanapotoka nje ya ndoa, ndo maana anasema ndoa na iheshimiwe na watu wote, msikilize Mungu anavyosema, utapona, usipomsikiliza unaweza ukakuza tatizo badala ya kutatua.
   
 17. b

  bwanashamba Senior Member

  #17
  May 13, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Miaka 3 ni mingi na miaka mitatu pia kwa namna nyingine naweza sema pia sio mingi
  ila omba Mungu na usikate tamaa ata kidogo ipo siku mambo yatajipa tu,ila jaribu
  kubadilisha stail za kumuingilia wife pia iyo pia huchangia
   
 18. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  miaka mitatu yote unafikiri alikuwa anatumia staili moja tu? hahaha. sema wazi basi ni stail gani anatakiwa kuitumia. i am not criticizing you, I am just curious!
   
 19. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #19
  May 13, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ..........Mpendwa Ramos hebu jaribu kurelax wewe na mkeo, kama ulivyosema mlishaenda kufanya vipimo na wote mkakutwa mpo okay. Muda mwingine ni timing tu ndugu yangu, utakuta mpo busy sana na kazi kiasi kwamba mnakutana kimwili siku ambazo ovulation ilishapita.
  .........Muda wa miaka 3 si mwingi hadi upate jaribu la kutoka nje ya ndoa, na huo umri wa mkeo wa miaka 31 si tatizo la wewe kufikiri mkeo hawezi kuzaa.........wapo wanawake wamezaa na age ya 46 sembuse miaka 31 mbona bado msichana huyo.


  ..........Kuna mdada alikuwa na tatizo kama hilo la kwenu, walikaa kipindi cha miaka 5 bila kupata mtoto yeye na mume wake, kwenda kufanya vipimo hawakuonekana na tatizo lolote la uzazi. Daktari aliwashauri wawe wanafanya tendo la ndoa kila baada ya siku moja ili iwe rahisi kutarget ovulation day, maana kuna baadhi ya wanawake wana irregular ovulation ambayo inakuwa ngumu kushika mimba.Hivi ninavyoandika hapa hao wanandoa sasa wana watoto 2 na maisha yanaendelea kwa raha zao.Hivyo jitahidi wewe na mkeo kufanya tendo la ndoa kila baada ya siku moja, Mungu anaweza saidia mimba ikatungwa. Vile vile msisahau maombi, kabla ya tendo inabidi mfanye sala ya kumuomba Mungu ili awape hitaji la moyo wenu.


  ..........Hilo wazo la kutoka nje ya ndoa liondoe kabisa, nyumba ndogo wala sio faraja yako ndugu, na mtoto wa nje wa ndoa hatoleta furaha kama ukipata mtoto na mkeo mpenzi..........na unaweza kutoka nje ya ndoa na kipindi hicho hicho mkeo anashika mimba sijui utafanyaje?Jitahidi kuvumilia tu na kumbuka kila jaribu lina mlango wa kutokea.
   
 20. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pia jaribu kupitia thread mbalimbali hasa kwenye jukwaa la JF Doctor unaweza kupata msaada. Kwa kuwa wewe ni mgeni humu Jf hebu jaribu kutembea thread hizi hapa kwa kubofya tu.
  >Tarehe 13 & 14
  >Mke hashiki mimba
   
Loading...