Miaka mitatu baadae unagundua mtoto si wako

Miaka mitatu baadae unagundua mtoto si wako

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,773
Nielekee kwenye Mada,

Huwa inatokea mara kadhaa kukuta miaka kadhaa baadae mtu anakuja
kugundua kuwa mtoto ambaye amezaliwa ndani ya ndoa yake si wake.

Miaka fulani nikiwa Newala na kwa wale wahenga wa Newala watakuwa
wanakumbuka vyema tukio la bosi wa kihindi ambaye alizaa na mke wa
Meneja wake. Meneja aliamua kuachana moja kwa moja na yule mwanamke
na kumkana mtoto.

Niulize tu kwa wataalamu wa JF, utafanya nini ukishagundua kuwa mtoto
ambaye umemlea kwa mapenzi makubwa miaka mitatu na zaidi unakuja
kugundua kwa dalili za wazi kabisa zisizo na shaka kuwa huyo mtoto si damu
yako, yaani hata bila kutumia DNA?
 
Mwache huyo mwanamke, halafu chagua kama Kumkana mtoto
au amua tu kumlea. Hili la pili jibu au chaguo unalo mwenyewe
 
Mtoto wa miaka mitatu nampeleka kwa baba ake halisi, baba yake akimkataa nitamlea mwenyewe

Mwanamke namtimua na asijitie ujasiri wa kutaka huyo mtoto hapo naweza kuchinja kabisa
 
Kitanda hakizai haramu.

Mtoto wa mkeo ni wako bila kujari mbegu ya uzazi kaipata kwa nani.

Mke kupata mtoto nje ya ndoa, kosa ni la mumewe na sio la mke.

Mlee mtoto kwani ni mtoto wako aliyezaliwa na mkeo.
 
70% ya wanaume wanalea watoto Wasio wa kwao, hii ni kwa mujibu wa mkemia mkuu wa serikali
 
Kitanda hakizai haramu.

Mtoto wa mkeo ni wako bila kujari mbegu ya uzazi kaipata kwa nani.

Mke kupata mtoto nje ya ndoa, kosa ni la mumewe na sio la mke.

Mlee mtoto kwani ni mtoto wako aliyezaliwa na mkeo.
Hii ndio tofauti ya wanandoa wa sasa na wale wa zamani.Enzi za babu zetu, issue kama hizi zilikuwa zinamalizwa kimya kimya na maisha ya ndoa yaliendelea.
Unamkanaje mtoto ilhali wewe mwenyewe hapo ulipo huna uhakika wa asilimia 100 kuwa unayemwita baba ndiye mzazi wako halali?
 
Kuchapiwa ni siri ya ndani, unakuta mke mzuri ukimwangalia tu hasira zinakwisha
 
Kitu cha ajabu ni kuwa; Matoto hayo ya mlango wa nje ndio huwa yanapata mafanikio kuliko mliozaa ndani ya hiyo ndoa. Mlee vizuri ila mwambie mkeo amweleze mwenye mtoto kuwa kuna litoto lake pale kwako. Akitaka alichukue akitaka aliache kwa mkeo. Siku ya siku asijelidai tena kwa sababu mambo yameliendea vizuri.
 
Mie hua Mada hizi sizipendiiiiiii🙁🙁🙁.kuna kitu hua kinanijia halafu namlani shetani nasema haya ukimchokonoa sana kuku utashindwa kumla..
 
Back
Top Bottom