sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,324
- 2,494
Katika jimbo la Rombo ambalo lipo chini ya Romani Selasini wa Chadema, nataka nitaje mambo mawili makubwa ambayo mbunge huyo alikuwa na nafasi ya kuyasukuma ila akashindwa kutokana na kutokuwa makini katika kuishawishi serikali na taasis husika pamoja na mashirika mbalimbali.
1. Mawasiliano ya radio, tv, simu. Minara ya Rombo ipo overloaded na minara ya Kenya ambapo kulipaswa kuwa na minara yenye nguvu kuliko ya Kenya ili watu wa Rombo waweze ku-access mawasiliano toka Tanzania. Alishindwa kushirikiana na serikali pamoja na idara husika kumaliza hilo tatizo.
2. Umeme wa REA.
Sasahivi maeneo mengi hakuna hata nguzo na wengine wamebaki na manguzo baada ya kushindwa kufuatilia huo umeme na kwa wakati kama ilivyo majimbo mengine, jukumu alilowaachia baadhi ya madiwani na watendaji wale ambao vijijini kwao hamna umeme kabisa wafuatilie wenyewe huku wengi wakikwama kwani hawana uelewa wa kutosha kwa kukosa mawasiliano ya vyombo vya habari vya ndani kama radio, tv, magazeti na pia madiwani hao hawana viti kule bungeni.
Matatizo mengine ya maji, uhaba wa ajira n.k yapo sehemu nyingi. Ila kwa kifupi, hajafanya chochote kwa muda wake wa ubunge.