RockCarnegie
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 963
- 1,927
Habari wana JF
Ukijifunza kwa nadharia tu, mara nyingi watu walio wengi huwa ni vigumu kupata ufahamu mpaka wafanye vitendo (practical).
Mwaka 2015 vyama upinzani viliwaeleza namna wananchi watakavyooshwa na Serikali chini ya Rais Magufuli lakini hawakuamini! Miaka mitano baadaye kila mtu anaweza kuelewa kuwa kukosea kuchagua kiongozi wa nchi, gharama inayolipwa na kila mtu ni kubwa haijalishi wewe ni kada mtiifu ama ni mpinzani!
1. Wafanyabiashara wanalia biashara zao zimekufa lakini wanasahau kuwa hawakutimiza wajibu wao ili kulipatia taifa kiongozi bora.
2. Wakulima wa korosho, pamba, mbaazi, choroko, ndegu, ufuta nk wanalia mazao yao yanakosa wanunuzi, lakini wanasahau kuwa walifanya kosa la kiufundi mwaka 2015 kuchagua rais na chama kisicho na uwezo wa kuwatafutia masoko ya mazao yao.
3. Wananchi waliokumbwa majanga ya matetemeko na mafuriko mnaweza kusimulia vizuri baada ya kufikisha vilio vyenu kwa mfariji mkuu wa taifa. Aliwaambia yeye hakuleta tetemeko, na waliosombwa na mafuriko aliwaambia acha mabonde 'yawabondoe'.
4. Jana mkulu awatangazia ambao hawakufanikiwa kupata mavuno mazuri ya mazao ya chakula 'watwangwe'! Ni somo la uraia kwa vitendo!
5. Wanahabari habari mnazo, ukijifanya mjuaji hutaki kusifu na kuabudu, uhujumu uchumi na uchochezi unakuhusu! Wote wimbo ni mmoja tu, nao ni Heko mtukufu kwa kuletea ndege, SGR, Stiglers na mabarabara ya juu kwa juu!
6. Wafanyakazi mpo! Miaka mitano jamaa kapiga pasi ndefu, hata mia haijaongezwa kwenye mishahara!
7. Wafugaji na wavuvi nao wanayakusimulia, umasikini ulioasisiwa na Magufuli na chama chake si wa kuisha leo ama kesho!
8. Wamachinga nao hawajabaki salama. Siku hizi wanapanga bidhaa mpaka katikati ya barabara, lakini wateja hamna! Uchumi umebaki wa kuhemea ubwabwa tu!
9. Wahitimu wa vyuo nao hawajaachwa salama kwenye somo hili la uraia kwa vitendo! Hakuna ajira na viwanda vinafungwa kila siku!
10. Bunge na Mahakama nao ni kuimba "asifiwe chaguo la Mungu". Wananchi hakuna pa kukimbilia kwani mhimili uliojichimbia unafanya kazi kwa maagizo na si kwa sheria na katiba!
Jiwe linataka miaka mingine mitano, sipati picha maisha ya watu yatakuwaje, kwani kwa ni heri punda afe ila mzigo ufike! Tayari mahabusu wametangaziwa kiama cha kazi ngumu kabla ya kutiwa hatiani, na kila mtu ni mahabusu mtarajiwa!
Uchaguzi mkuu wa October ni upenyo wa kuikataa CCM na mgombea wake Rais Magufuli ambaye kwa miaka mitano amedhihirisha kuwa kwake vitu ni bora kuliko utu!
Pamoja na kuwa Tume ya uchaguzi, polisi na usalama ni mbeleko za chuma zinazo mhakikishia Jiwe kuapishwa kuwa rais kwa miaka mingine mitano, Mungu huwa yuko upande wa wenye haki, Mwananchi timiza wajibu wako, kataa mateso na umasikini unaoletwa kwa makusudi na CCM chini ya Jiwe.