Miaka ijayo Ndoa nyingi zitakuwa hivi...

baptist

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
426
255
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Ann Magwi na Jonathan Munini kutoka Kenya, wamelazimika kukatisha zoezi la kufunga ndoa, baada ya James Sidai kujitokeza kanisani na kusema yeye ndio Baba yao Mzazi, Baba huyo aliingia kanisani akiwa na Dada yake na kusema ndoa hiyo isifungwe kwa kuwa Maharusi ni Ndugu wa damu.

"Mama zenu nyie, mmoja aliniacha akaondoka na Mtoto akiwa na mwaka mmoja, mwingine aliona uchumi wangu umeyumba akaondoka akiwa na mimba ya miezi minne na akaolewa na Mwalimu, nikaamua kumuoa mwingine na tuna Watoto watatu, nimeona tangazo la harusi yenu WhatsApp zile picha nikasema hawa ni Wanangu nikachunguza kwa Watu mlioishi nao wakasema ni kweli"-JAMES

Bwana harusi ambaye ni Mfanyabiashara katika mji wa Madogo aliondoka Kanisani kwa hasira akimuacha Mama yake akiwa analia huku Bibi Harusi akiondoka na Mama yake ambaye inadaiwa alikuwa amepoteza fahamu.

Hali ni mbaya Wazee, hii trend ya watoto wa Familia kutokufahamiana inazidi kuwa kubwa siku hadi siku.
 
Sasa si kunyanduana tayali washanyanduana inakuwaje hapo ebu wababa wachungaji na baba mapadre mkisaidiana na mashehe hii inshu imekaaje
 
Ubinafsi wa wanawake ndio unasababisha hayo.
Mtu ukizaa naye mtoto mwambie mtoto baba yake ni nani?
Haipunguzi kitu.
Makosa yao wanayahamishia kwa watoto ili wawachukie baba zao.
Ukiwa baba unamheshimu Sana baba yako.
Maana unagundua namna alikuwa anazinguliwa na Mama. Na shida zote ulikuwa unaambiwa kuhusu baba unagundua ulikuwa uzushi mwingi
 
Hao tayari wamesha laanika. Ndugu wa damu kufanya mapenzi. Wanatakiwa kufanya toba.
 
Hao tayari wamesha laanika. Ndugu wa damu kufanya mapenzi. Wanatakiwa kufanya toba.
Mungu ni mwenye rehema atawasamehe, wamefanya yote si kwa kukusudia kulala na Kaka au Dada yake, Mungu pia huitazama nia ya mtu ndani japo bado ni laana, maana imeandikwa amelaaniwa alalaye na binti wa Baba yake.
 
Back
Top Bottom