Mzee Leonard Rwizandekwe aliwashangaza Watanzania mwaka 1965 kwa kukiomba chama cha TANU kimpendekeza kwa wananchi awe mgombea pekee wa urais badala ya Mwalimu Nyerere, akiwa kijiji kwake Katendaguro Wilaya ya Misenye Mkoa wa Kagera alipofanyiwa mahojiano na Elisa Muhingo na Mathias Byabato...
www.jamiiforums.com
Mzee Leonard Rwizandekwe aliwashangaza Watanzania mwaka 1965 kwa kukiomba chama cha TANU kimpendekeza kwa wananchi awe mgombea pekee wa urais badala ya Mwalimu Nyerere, akiwa kijiji kwake Katendaguro Wilaya ya Misenye Mkoa wa Kagera alipofanyiwa mahojiano na Elisa Muhingo na Mathias Byabato, Bukoba, anasema wakati huo ilikuwa ni nadra na vigumu mtu yoyote kutaka kugombea nafasi hiyo kwa kuwa wananchi wengi walidhani kuwa hapakuwepo mtu mwingine zaidi ya Mwalimu Nyerere ambaye angeweza kuwa Rais wa nchi.
Alizaliwa tarehe 14 juni mwaka 1929 katika kijiji cha Katendaguro na kusoma shule ya msingi ya Rukurungo na baadae alipelekwa katika jumba la Mugorola lililokuwa Bunge la jadi ambapo hapo alikaa humo akilelewa na wazee ikiwa ni pamoja na kufundishwa maadili, utii, na uwajibikaji.
Mwaka 1948 alichaguliwa kujiunga na shule ya Serikali Ihungo iliyopo Bukoba kwa masomo ya Sekondari ambapo baada ya kuhitimu aliajiriwa katika idara ya mahesabu katika Wilaya ya Buhaya.
Rwizandekwe aliamua kujisomea mwenyewe masomo ya sheria na alipofanya mtihani wa Chuo cha Kibete cha nchini Uganda alifaulu vizuri na baada ya kupata cheti aliajiriwa katika sekta mbalimbali serikalini ambapo juni 1 mwaka 1959 aliteuliwa kuwa Hakimu wa Mahakama ya Rufaa ya Buhaya.
Mwaka 1960 alichaguliwa kama mtumishi bora kutoka Halmashauri ya Buhaya kwenda kuhudhuria semina ya sheria za Afrika nchini Uganda ambapo kupitia huko alichaguliwa pia kuhudhuria masomo ya shahada ya sheria za mila za Afrika katika Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza.......