PRESIDENTIAL MEMOIR: Rais Magufuli, baada ya kustaafu, ukipenda kuandika kitabu kama mzee Mkapa, tumia lugha ya wazalendo ya Kiswahili

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari zenu JamiiForums.

Ninaomba kuanza kwa kunukuu maneno ya Balozi Mkuu wa lugha ya Kiswahili Mh. J.P Magufuli alipokuwa kwenye hafla moja jijini Dodoma. Mheshimiwa Rais alisema hivi “Nimefanya PHD bado wanasema sijui Kiingereza, na nikakaa mwaka mzima Uingereza, sijui nilikuwa nazungumza Kisukuma kule!, wakasema sijui Kiingereza, niliamua kuzungumza Kiswahili na kuki-promote kwasababu ni lugha iliyoachwa na Baba wa Taifa"

aaaaaaaaaaaasdsdeeeeeeeeedfrfwwwwwww.jpg


Picha hapo juu ni Mh. Rais Dk. JP Magufuli akiwa na Waziri wa mashauri ya kigeni Prof. Kabudi wakikabidhi vitabu vya kiswahili kwa Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kusini Mh. Ramaphosa katika harakati ya kuhakikisha lugha hii tamu inakuwa na kuenea kwa haraka zaidi nje ya mipaka ya Tanzania na Afrika ya Mashariki.

Kitabu cha Kiingereza cha Mzee Mkapa: My Life, My Purpose: A Tanzanian President Remembers
Mheshimiwa, hayati Benjamin William Mkapa ndiye aliyekuwa rais wa tatu wa Tanzania, aliyechaguliwa chini ya mfumo wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini. Kitabu chake kinafafanua kumbukumbu zake kutokea utotoni, wakati bado akiwa rais, na kuendelea kwake kujihusisha (hata baada ya kustaafu) kwenye masuala ya kimataifa yahusuyo maendeleo na upatanishi wa amani.

images (12).jpg

Kitabu hiki kinavutia sana kwa wasomaji wanaopenda kujua kuhusiana na, kadhia aliyoipitia mwafrika katika kipindi cha ukoloni hususan eneo zima la Afrika Mashariki na mapambano ya uhuru na harakati za ukombozi wa nchi kadhaa za kusini mwa Afrika.

Mheshimiwa Mkapa ameandika pia kuhusu utoto wake, kukomaa kwake kisiasa, mabadiliko ya kimfumo/kiutawala na kisiasa nchini Tanzania, na vile vile machafuko ya kisiasa katika nchi jirani.

Kitabu hiki kimejaa maoni yake juu ya uongozi na ushauri kwa viongozi wanaochipukia kama dada yangu mama D. Baada ya Mwalimu Julius Nyerere, ni vitabu vichache sana vimeandikwa na viongozi wakuu wa Tanzania juu ya mageuzi ya nchi; kwa kweli bila kuwa mnafiki vitabu vingi vinavyosomwa hapa nchini vimeandikwa na wageni kuliko watanzania, kwa hivyo kitabu cha Mh. Mkapa ni mfano bora wa kuigwa.

I Can, I Must, I Will written by Dr. Reginald Mengi
=====

images (14).jpg


OMBI LANGU: Itapendeza sana kama Rais Magufuli ataandika kitabu cha maisha yake kwa kutumia lugha ya wazalendo ya KISWAHILI.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Bora aandike kwa lugha yake pendwa ya Kisukuma. Sisi wengine hatutakinunua maana tunamjua hapendi kukosolewa, so hawezi kujikosoa kama Marehemu Mkapa alivyojikosoa kwenye kitabu chake, yeye huwa anapatia huwa hakosei hata pale anapokosea wazi wazi, na pia si mkweli wakati mwingine (Refer ahadi alizowahi kutoa na hakuzitimiza).
 
Nyama za kazi gani tena? Mbona yeye ni balozi mzuri wa Kiswahili na anaipenda lugha mama ya taifa...

Sio kweli, huwa haongei kiswahili fasaha maana hupenda kuchanganya na maneno ya kiingereza. Ukweli ni kuwa hawezi kuongea kiingereza kwa ufasaha, ndio maana anaongea kiswahili, na hata hicho kiswahili anakichafua kwa kuweka maneno ya kiingereza mengi ili kukoga watu kuwa ni msomi.
 
Sio kweli, huwa haongei kiswahili fasaha maana hupenda kuchanganya na maneno ya kiingereza. Ukweli ni kuwa hawezi kuongea kiingereza kwa ufasaha, ndio maana anaongea kiswahili, na hata hicho kiswahili anakichafua kwa kuweka maneno ya kiingereza mengi ili kukoga watu kuwa ni msomi.
Kumbe kuongea kiingereza ni ishara ya usomi?
 
Nitaandika kwa niaba yake nina wazo hilo pia.Sema sijapata connection na Jk pia. Nitamaliza na cha Mizengo pinda mtoto wa mkulima.
 
Back
Top Bottom