Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,510
- 4,224
Inasikitisha sana kuona jinsi shirika hili linavyoendeshwa.Miaka 60 ya uhuru lakini bado umeme ni wa shida hapa nchini.
Mbaya zaidi hakuna anayewajibika au kuwajibishwa. Waziri mhusika ndiyo kwanza anatumia chopper kukagua vyanzo vya maji na kusema Tanzania nzima hakuna Crane ya kuweza kubeba tani 80 na kutangaza mgao wa siku zaidi ya 10 akiahidi kumaliza kero za umeme jambo ambalo tumeshuhudia kuwa ni uongo, Lakini cha kushangaza bado yupo ofisini.
Umeme umekuwa ukikatika hovyo kwa kisingizio cha dharura. Hivi TANESCO wanaelewa maana ya neno 'dharura'?
Walau miaka michache iliyopita hapakuwa na makatizo Makali ya umeme kiasi hiki. Ina maana vyanzo vya umeme hapo nyuma vilikuwa tofauti na sasa?
Tuliaminishwa mgao mkubwa uliopita siku za karibuni utakuwa mwisho Lakini inasikitisha kuona kila mara umeme bado unakatika kwa sababu zisizoisha.
Sijui lini Tutafika.