Miaka 60 ya Uhuru: Kwanini Katiba Mpya?

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Habari Tanzania!

Naomba kuuliza wapenda nchi eti kwa muda wote huo wa umri wa nchi miaka 60 ndio tutake KATIBA MPYA?

Kwanini kwa miaka yote 60 eti ninyi mnawaza maendeleo tu yasiyo kikomo au kuakisi mahitaji?

Kwanini hawa wapenda siasa na waishio ndani yao wanapenda kuaminisha UMMA yakuwa mawazo yao ni sahihi kuliko wengine?

Kwanini Kilimo muwe mnalopoka eti ni UTI WA MGONGO wa Tanzania na kwenye KATIBA ya sasa na hiyo MPYA hakuna anayekumbusha!?

ONYO
Penda kuweka ufahamu huu " kila mtu na amuhesabie mwenzie kuwa ni bora kuliko yeye; hakika utapa ukitakacho au ukitarajiacho kutokana na mahitaji au umuhimu"

Asante
 
AKILI ulizotumia kuuliza sasa ulipaswa zitumike kuuliza Wakati Mchakato wa kukusanya Maoni naTume ya Warioba ulipoanza.
Pili Katiba Mpya sio Mchakato wa Sasa imekuwa inadaiwa Siku nyingi kumbuka MTIKILA aliidai.

Tatu Katiba iliyopo hiyo ya Miaka 60 imeshindwa kutuletea Maendeleo mpaka sasa hata kujenga Matundu ya Vyoo Tunahangaika kutokana na Ubovu wa Katiba kwani inatoa Mwanya kwa Fedha ambazo ni KODI kuchezewa na Watawala na pia Watawala kuichezea Katiba bila kuwajibishwa.

Pia Katiba iliyopo haitendi Haki kwa Vyama vya Siasa vingine kwani bado ni ya Chama kimoja.Kuna Uchafu mwingi kwenye KATIBA ILIYOPO.
 
Back
Top Bottom