Miaka 60 ya uhuru, bado tunaning'iniza watoto kwenye miti kuwapima uzito

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,018
144,377
Hii habari nimesoma twitter, habari inayosema watoto wadogo wanapimwa uzito kwa kuning'inizwa kwenye mti huko wilayni Tarime mkoa wa Mara(kuna picha ikionyesha tukio hilo).

Hakika nimeshangazwa sana na hii habari, ila inaelekea hali hii ni ya kawaida tu kwa baadhi ya maeneo ya nchi yetu huku tukiwa na takribani miaka 60 ya kujitawala.

Jamani vitu vingine tuone aibu kwani haiwezekani viongozi watembee na mashangingi huku watoto wetu wananing'nizwa kwenye miti kama viroba miaka 60 baada ya uhuru na watu tunaridhika tu.

Alieturoga watanzania hakika alikuwa fundi.

Habari husika hii hapa chini na inapatikana pia JamiiForums twitter account :

TARIME: WATOTO WANING'INIZWA MTINI KUPIMWA UZITO, WAJAWAZITO WALAZWA CHINI

- Wananchi wa Nyagisya wamesema wanafanya hivyo kwa kuwa Kijiji hakina Zahanati

- Wizara ya Afya imesema inafuatilia kwanini Uongozi haujatumia Majengo ya Serikali

Soma - Taarifa kwa Umma: Zahanati ya Mtama mkoani Mara kutoa huduma ya vipimo kwa wajawazito mezani na watoto chini ya mti

#Afya https://t.co/IdLLhkQliK
 
Kawahadithie baba zenu mabeberu, halafu watawatia moyo kwakutoa tamko la kuweka vizuizi vya watanzania kuwa wamezuiliwa wasiende kununua vitumbua kwa mabeberu, ilihapo ufipani mfarijikee.
 
wanaharakati fulani wakawa wanapigania uhuru wa kuongea
.

mtu hana hospital ya maana unamwambia habari za kuongea ongea,anaishia kukuangalia tu.
 
Kama Tarime bado wanatahiriana kwa mapanga unashangaa nini kupimana uzito kwa kuning'inizana kwenye miti?
 
Kwan wanatakiwa kupimwaje tofauti na kuning'inizwa kwenye kile kidude Cha kupimia pale hospital?
 
Mgawanyiko wa kimaendeleo hauko sawa lazim. Semeh flan kutoendelea Zaid kuliko kwingine hvy Basi unapozungumzia neno maendeleo nineno pana san mkuu tusijaji vitu juu juuu
 
Waning'inizwe tu, kwani shida nini? Mzae tu, elimu bure. Nchi ya viwanda na uchumi wa kati. Sisi ni matajiri, msitusumbue humu.
 
Tunajenga kwanza Vyumba vya Madarasa
 
Halafu kuna mwehu anatamba kajenga vituo vya afya 380..vipo wapi..?? Mbona Tarime watoto wanapimwa nje kwenye miti
 
Dah...sijaelewa mkuu....tatizo ni kupimwa kwa kuning'inizwa...au kuning'inizwa kwenye mti?
 
Hio njia ya kuning'izwa ni nzuri kabisa haina shida yoyote hata DSM wanatumia kuning'iniza sasa sijui shida iko kwenye kuning'iniza au kuweka huo mzani kwenye mti. Maana habari haina picha binafsi nimeshindwa kuelewa shida iko wapi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…