Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar: Rais Mohamed Shein, awasamehe Wanafunzi 12 wa vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba

Drjacka92

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
445
522
IMG-20180112-WA0000.jpg


MY TAKE:

Natumai Kumekucha salama.

Kuwaelewa wazanzibar wanachomaanisha wakiongea ni kwa Msaada wa Mungu tu.

Kufuatia Sherehe za mapinduzi huko Zanzibar, mh. Shein amewapa msamaha baadhi Ya WANAFUNZI ambao walikuwa bado wameendelea Na mafunzo Kwenye vyuo mbalimbali.

Sasa kila nikitafakari Naona ukakasi hivi, Yani amewasamehe Wanafunzi??. Kwa haraka nikaelewa labda wanamaanisha wafungwa, Na ivyo vinavyosemekana vyuo labda Ndio Magereza.

Sasa nimeona nije hapa labda wazanzibar wenyewe watatuelekeza vizuri wanachomaanisha.

Naomba kuwasilisha.

Habari zaidi soma=>LIVE - Yanayojiri Uwanja wa Aman, Zanzibar: Sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 
Ndio maana wanasisitizwa elimu hawa watu, haya maneno yanachanganya.
- Wanafunzi
- Vyuo vya Mafunzo
- Wafungwa
- Msamaha
 
Back
Top Bottom