Miaka 50 ya utawala CCM ime expire | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya utawala CCM ime expire

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mjukuu2009, Sep 8, 2010.

 1. m

  mjukuu2009 Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Bei ya mkate yapunguzwa Msumbiji


  [​IMG]Msumbiji


  Msumbiji itabadilisha ongezeko la bei ya mikate iliyosababisha kuibuka kwa ghasia wiki iliyopita.
  Tangazo la kubadilisha sera zimetolewa na waziri wa mipango, Aiuba Cuereneia, ambaye amesema pia kwamba nchi hiyo itarejesha baadhi ya ruzuku ya umeme na maji.
  Ongezeko la bei ya vyakula na bidhaa nyingine zilisababisha maandamano ya siku tatu.
  Serikali ilisema zaidi ya watu 400 walikamatwa wakati wa maandamano hayo, iliyosababisha watu 13 kufariki dunia.
  Taarifa ya waziri ilisema kwamba serikali " itaendelea kuuza mkate kwa bei ya awali huku wakipanga ruzuku."
  Awali serikali ya Msumbiji ilisema ongezeko la bei "haibadiliki".
  Kuweka bei ndogo ya bidhaa nchini humo ni ngumu kwani kiwango kikubwa cha chakula chao hutoka nchi za nje.
  Taifa hilo lililopo kusini mashariki mwa bara la Afrika linazalisha asilimia 30 tu ya ngano inayohitaji.
  Ongezeko kubwa la bei ya vyakula lilisababishwa kwa upande mmoja na thamani ya pesa ya Msumbiji dhidi ya randi ya Afrika Kusini, ambapo wachambuzi wanasema bidhaa kutoka nje zinazidi kuwa ghali.
  Pamoja na hayo, bei ya ngano imeongezeka kufuatia ukame nchini Urusi, muuzaji mkuu wa ngano duniani.
  BBC Swahili - Habari - Bei ya mkate yapunguzwa Msumbiji


  Angalizo;
  Kwanini sisi watanzania atuonyeshi kushituka kila siku bei ya mafuta,soda,beer,ngano vinapanda lakini sisi wala atujigusi hivi sisi tumelogwa au tuna matatizo ya akili?
  kama wenzetu mkate unapanda sisi je kila kitu kinapanda tumeka kimya utafikiri atuvitumi hivyo vitu,kama tumeshindwa basi tuondoe huu utawala wa majambazi.
  Tumeluwa tukiongozwa na majambazi kwa miaka 50 kila kitu kinazidi kuwa juu tokea nimezaliwa sasa miaka 30 sijawai kusikia bei ya kitu ikishuka apa Tanzania,tumpe kura Dk.Slaa angalau tushuhudie bei ya vitu muhimu ikishuka kwa wengi wetu itakuwa ni neema kubwa.Miaka 50 ya utawala ccm imesha expire tumpe Dk.Slaa ilitu renew nchi yetu jamani tupate tanzania mpya yenye mtazamo mpya ccm haiwezi imesha shindwa kwa miaka 50 kwaiyo ata wakipewa madaraka awataweza tena,nasikitika sana ninaposoma na kuambiwa uchumi wetu ulikuwa sawa na Singapore miaka ya 60,70 sasa hivi ata Rwanda waliopigana miaka mingi wanatushinda aibu gani hii.
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Na utakuta bei ya mkate msumbiji ni robo ya bei ya mkate bongo
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  tubadilike sote...........tuseme sasa basi.....ccm imetuchosha...........tunataka tuondoke kutoka hapa tulipo......tumekaa kwenye tope la ccm kwa muda mrefu sana...........hata wan ccm wenyewe ndani yake wamechoka sana ukiongoe nao ...wanasema chama chetu kimewapa umasikini mkubwa watu wetu usiokuwa wa lazima yaani wa kujitakia..........
   
 4. J

  Jafar JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naona tumelogwa.
   
 5. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli,SERA za CCM ni nzuri sana,tatizo ni jinsi ya kutekeleza hizo sera.
  Ni bora sasa ccm wakaridhika kuachia majukumu ya kuendesha nchi kwa kizazi kingine yenyewe ikakaa pembeni kwa kipindi angalau kimoja,ishuhudie mabadiliko ya Kisiasa,kiuchumu,Kijamii-michezo,kilimo,mifugo,madini nk nk....
  Hapo ndipo itakapojua kwamba Tanzania kuna mali na mali inakimbizwa nje na wajasiriamali wachache wa asili ya huko nje.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Let us make it a reality come October 31 2010.
   
 7. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Basi kila unapoamka sali hivi:

  Ee J.K. uliyetufilisi, jina lako ni Usanii mtupu,
  Utakalo lifanyike Bagamoyo tu,
  Utupe leo mamilioni yetu ya EPA.
  Uwapeleke Mahakamani mafisadi, uwalipe waalimu na wastaafu
  malipo yao
  Uwasamehe wafungwa wote kama ulivyowasamehe Lowasa,
  Karamagi, Msabaha na Vijisenti.
  Usitutie katika mikataba feki
  Utuondolee mafisadi wote,
  Kwa ufisadi ni fani yako na uwongo na utapeli hata milele.

  AMINA.
   
 8. D

  Dopas JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sijui tumelaaniwa? Sijui ni ujinga? Utashangaa tunalalamika hali duni, lakini wakijitokeza hao mafisadi kuomba kura tunawapigia makofi. IMETOSHA. Tuwaelimishe watanzania. Badala ya makofi ni kuzomea hao wezi wa mali ya umma. Tusisibiri waingie tena Ikulu kisha tuandamane. Enough is enough
   
 9. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unaamka kwenu Tandale kwa mfuga mbwa na kazi unafanya mburahati.you don't know even a single border of your country.
  tembelea majirani zetu uone bei za vitu katika nchi hizo kisha fanya conversion kwenda kwenye Tsh ndio utajua gharama ya maisha hapa TZ ilivyo chini. nina wasiwasi na wataka mabadiliko kama mnajua mnaka mabadiliko ya nini
   
 10. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145

  Watanzania hatujalogwa ila ni wazito kujua baya na zuri

  _______________________________________________
  Wakatae waepuke wanaokudanganya,
  Ni wajinga wakupoteza wewe
  Ila wewe ukatae kutokumchagua Dr. Slaa
  Waambie wenzako CHADEMA ndio Mkomboz
  i!
   
 11. LAMPARD

  LAMPARD Member

  #11
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CHAMA CHA MAPINDUZI, ccm itaendelea kudumu kudumu zaidi , ni tofauti na vyama vingine kabisa ambavyo vinapitapita leo mitaani vikiomba kura, ni ukweli usio pingika kwamba vyama hivi vya mlengo wa kushoto hawana sera ambazo wenyeakili wakizisoma zinaweza zikawaingia, sera za wenzetu ni danganya toto kwa maana ya ELIMU BURE, AFYA BURE , SERIKALI YA TANGANYIKA , UFISADI, na mengine mengi ambayo wanayoyajua wao.

  wanaposema suala la elimu bure , mimi siwaelewi kabisa maana shabaha yao ya kusema elimu iwe bure sijui wanaitoa wapi labda kwa faida ya wale wasiojua haya mambo ya vyama vingi yalipoletwa na hao wanaitwa mabwana wakubwa yalikuja na misururu ya mambo mengine kama watu wachangie katika elimu, afya, mfumo wa vyama vingi uanzishwe, mashirika yasiyojiweza yabinafsishwe, haya yalikuwa ni matakwa ya wakubwa IMF NA WORLD BANK, sasa sisi kama waTanzania na waafrika kwa ujumla tulikaa nao kwa pamoja na kukubaliana ili mambo hayo hapo juu na mengine yaende kwa kufuata kanuni za nchi husika.

  sasa hawa wanaosema elimu bure sijui wanamkakati gani na nchi yetu maana Tanzania kama Jamuhuri ya muungano ni mwanachama wa mashirika hayo hapo juu, sasa wenzetu wanaotaka elimu bure wanataka kutuambia watajitoa huko......? sasa wakijitoa huko tutakuwa mgeni wa nani sisi waTanzania hili sio suala la kubeza hata kidogo au kulifanyia mzaha....mkiamini hivyo itakuja kutugharimu vibaya ndio maana mimi hawa CHADEMA nawaona ni wababaishaji tu, hili la elimu hata nchi kama Marekani wanachangia si hapa kwetu tu ndio maana Rais wao Obama katika kitabu chake cha Audacity of Hope Anaelezea jinsi wamarekani wanavyotaabika usiku na mchana kuhakikisha wanapata kipato kitakacho wafanya wawalipie watoto wao ada za shule na yeye ameingia madarakani na kuliboresha zaidi sio kwamba wasilipe kabisa hapana.

  Kadhalika suala la afya duniani kote watu wanachangia ,pia kuna na health care Insurance sembuse linchi kubwa kama Tanzania unaposema afya bure inabidi tukutizame mara mbili au tatu coz it may be ur brain is working unclockwise sorry 4 sying that but dat's is the reality my friends.

  Wapinzani katika Tanzania ya leo wanazungumzia SERIKALI YA TANGANYIKA , katika yote hili ndio limenikera sana maana laiti hata mwalimu angekuwepo hai leo suala hili bado angeendelea kulipigia kelele CHADEMA wanataka kuigawa nchi hii ambayo imejizolea heshima kubwa duniani kwa utulivu iliyokuwa nayo, wasisahau miaka ile ya1991,1992 1993,1994, ndani ya CCM kulikuwa na wapuuzi wakilitaka hili lakini kwa uimara wa Mwalimu Nyerere waligonga mwamba na likafa kabisa leo wenzetu hawa wa chadema wanalifanya kama mtaji wa kuombea kura naamini kabisa wameishiwa sera sasa wanataka kutulaghai wananchi......., nawaambia watanzania HATUDANGANYIKI.

  CCM chama kikubwa chama dume,dume la mbegu kitaendelea kutawala nchi hii zidi na zaidi

  LAMPARD.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  JAFAR unajua kama aliyeturoga angekuwa HAI ingekuwa afadhari ila naona aliyetuloga ameshakufa
   
Loading...