Miaka 49 ya magwanda haya tafakari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 49 ya magwanda haya tafakari!

Discussion in 'Jamii Photos' started by Hofstede, Dec 9, 2010.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Joseph ambaye ni mgonjwa amekutwa ameanguka barabarani baada ya kuzidiwa alipokuwa akitoka hospitali. Utamuona kuwa japo amekosa usafiri na mtu wa kumuangalia bado ameanguka akiwa amevaa nguo za kijana akiashiria dole gumba.
  untitled3.JPG

  Huduma za afya ni tatizo kubwa kwa watanzania wengi na huenda alivaa magwanda haya akifiria kuwa kutakuwa na favour fulani. Ila pia huenda magwanda hayo kwake yalikuwa ni muafaka katika kushine kwa yatakuwa bado mapya baada ya uchaguzi kuisha mwezi mmoja uliopita. Tufanye kazi sasa katika kuboresha huduma za afya na maisha ya watanzania vinginevyo nina hakika huyu bwana Joseph 2015 atakuwa amebadilika na kuwanyima kura waliompatia magwanda haya mwaka huu.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ugonjwa hauna chama......ZINDUKA!
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakubalina na wewe kwa 100% ila huduma bora za afya ni sera zinazosimamiwa na vyama. Mfano huduma za dharura kama gari la wagonjwa na huduma ya kwanza pindi mtu kama huyu akianguka basi mara moja First Aid squad wanakuwa wamefika. Pili huyo amenguka njiani kwa kuwa hana pesa ya kukodia taxi ambayo ingemfikisha nyumbani salama. Haya yote yanapaswa kuwa sera za vyama na serikali zinazojadi huduma kwa raia wake zinakuwa na wasiwasi pindi mambo kama haya yakitokea.
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Taarifa imenisikitisha mno.
  Sasa aliambiwa na waliompa hayo magwanda kuwa popote atakapoyavaa hatopata shida kama hiyo iliyomkuta!
  Maskini wee!
   
 5. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mimi napata hisia alias Joseph ametoka kusherehekea ushindi mahali fulani na mitungi ya bure imemzidi!
   
 6. Muro

  Muro Senior Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo mgonjwa huyo ni mlevi chunguza kwa makini hiyo picha utagundua
   
Loading...