Miaka 39 sina mke wala mtoto. Je, hii ni kawaida?

stephenga

Member
Sep 15, 2022
38
146
Natamani kujua kama hii ni kawaida au mimi ni mtu ajabu. Nakaribia miaka 39 na sina mke wala mtu naetegemea awe mke wangu. Sina mtoto japo ninauwezo wa kuzalisha vizuri sababu nilishawai wapa mimba wanawake watatu tofauti tukazichomoa.

Japo bado sina mke lakini naamini sana kwenye ndoa na kuzaa watoto wangu wote na mama mmoja ndani ya ndoa. Ndio maana sijakubali kuzaa na mtu pia naogopa mtoto kulelewa na mama wa kambo coz nna experience mbaya ya mama wa kambo.

Kitu kinachonifanya niulize sababu kila anaeniuliza kuhusu family yangu nikimwambia sina mke wala mtoto anashangaa sana. Kiasi inanifanya nijione mtu ambaye nimepotea au niko very wrong.

Kifupi mimi sio mtu sana wa mapenzi na nikiwa na mwanamke uwa anakuwa huyo huyo so nikistukia mwanamke sio mwaminifu ananikifu hapo hapo na simtaki tena hii imefanya nimekuwa sikai na wanawake.

Kingine mie ni disminder napenda simple life hata wanawake wangu naowapenda ni wale kama machakalamu fulani unakuta ana vikuku bleach kichwani tattoo Yani mpaka kuna muda uwa najiona kama sipo sawa maana washikaji wanasema huyu sio mke tafuta mke na mimi demu akiwa decent sana hatukai japo mimi ni mpole saana ila sipendi mwanamke yule decent kavaa vitenge sijui kajizungushia mtandio kavaa mosimo. Nimekuwa mtu najitafuta kila siku sijipati.

Sasa nisaidieni nipo sawa sawa au kuna kitu namiss na nifanyeje nibadilike??? Maana naona nitaazeeka sina familia.
 
Natamani kujua kama hii ni kawaida au mimi ni mtu ajabu. Nakaribia miaka 39 na sina mke wala mtu naetegemea awe mke wangu. Sina mtoto japo ninauwezo wa kuzalisha vizuri sababu nilishawai wapa mimba wanawake watatu tofauti tukazichomoa.

ole saana ila sipendi mwanamke yule decent kavaa vitenge sijui kajizungushia mtandio kavaa mosimo. Nimekuwa mtu najitafuta kila siku sijipati. Sasa nisaidieni nipo sawa sawa au kuna kitu namiss na nifanyeje nibadilike??? Maana naona nitaazeeka sina familia.
Life begins at 40
 
• Kuwa Mcha Mungu kiimani na kivitendo maana Mungu huwa hapokei maombi ya mdhambi ( si Mnafki).

"YOHANA 9:31."

• Mchagua sana nazi hupata koroma, kila jambo kwa kiasi.

• Usikate tamaa ungali hai ila tunza sana afya maana afya ni uhai..

• Tabia ndiyo Mke si urembo, hata lover boys huoa Ke wa kawaida sana kimwonekano ila vichwani huwa wana hekima na maarifa tele.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mahusiano unayo ila muda wa kuoa ndo haujafika..... Kwani kinacho kufanya usio nini haswa? Siku
Mpaka leo uwa sina sababu ya msingi nakuwa naona nnaempenda ni msumbufu naogopa atanizingua kwenye ndoa na wale naona kabisa huyu ni mke kwa tamaduni zetu nakuwa sina mapenzi nae ya kweli.
 
• Kuwa Mcha Mungu kiimani na kivitendo maana Mungu huwa hapokei maombi ya mdhambi ( si Mnafki).

"YOHANA 9:31."

• Mchagua sana nazi hupata koroma, kila jambo kwa kiasi.

• Usikate tamaa ungali hai ila tunza sana afya maana afya ni uhai..

• Tabia ndiyo Mke si urembo, hata lover boys huoa Ke za kawaida sana kimwonekano ila vichwani huwa vina hekima na maarifa.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Asante nimekuelewa.
 
Back
Top Bottom