Miaka 11 ya ushauri uliofanyiwa kazi, Najisifia, Hutaki Acha!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Miaka 11 iliyopita niliandika makala mitandaoni nikipendekeza Ikulu ya Dar es Salaam ihamishwe mahali ilipo Magogoni jijini Dar es Salaam, nilipendekeza wazo la Mwalimu Nyerere kuhamishia ikulu Dodoma lizingatiwe na kama hilo litakwama basi Ikulu inaweza kubakia Dar lakini ijengwe pembeni ya mji Kigamboni Kisawe II kule.

Hoja kubwa nilizojenga zilikuwa ni za kiusalama zaidi, Niliamini hoja za Mwalimu Nyerere juu ya Kuhamia Dodoma zilikuwa za Kisiasa na zilikosa nguvu baada ya Muungano wa TANU na Afro Shiraz Party uliozaa CCM 1977 ambapo Wajumbe wa CCM toka Zanzibar walikataa hoja ya kuhamia Dodoma kwakujenga hoja kuwa ni mbali kwao. Na pia Vita vya Kagera vilichangia pakubwa agenda ya kuhamia Dodoma kufa. Izingatiwe kuwa Rais Nyerere alikuwa ameleta wataalamu kutoka Nigeria wakadizaini mji mpya wa Kiserikali Dodoma 1973 wakachora ramani ya mji huo na Ikulu itakavyokuwa.

Unaweza kuisoma makala hiyo hapa Ikulu ya Dar ihamishwe ndani ya miezi 18 kuanzia 01/01/2015

Baada ya Magufuli kuingia madarakani, Mwezi December 2015 enzi hizo naandikia katika Gazeti la Mwanahalisi, niliandika makala hiyo kama ukumbusho na msisitizo kwa serikali mpya juu ya hoja yangu ya kutaka Ikulu ihamishwe. Na mwaka 2016 makala hiyo nikaiweka katika Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kwa urefu zaidi na mapana yote, nikichambua, kunyumbua na kupembua kila kona ya Ikulu ya Magogoni na kwa nini Ikulu hiyo ihame mahali ilipo.

Mwaka 2016 huohuo katika moja ya ziara ya Rais Magufuli akitokea Mwanza, alizungumza juu ya kusudio la kuhamisha Ikulu, akatoa hoja za kiusalama ambazo ziliendana kabisa na hoja zangu, na kwa sehemu kubwa japo hakukitaja Kitabu husika kwa jina, Magufuli alijibu kile kilichoandikwa na kitabu cha Ujasusi, Alikuwa amekinadi vizuri kitabu hicho.

Leo yametokea ikulu ya Dodoma imekamilika kwa 100%. Hii ndio ikulu kubwa zaidi barani Afrika kwa sasa, na iliyojengwa na wazawa kwa 100/%. Binafsi sihitaji kusifiwa bali wewe nunua kitabu cha Ujasusi usome kwa undani zaidi, utakuwa umeniinua, sifa zingine najisifia mwenyewe!

Kwaundani zaidi, Soma KITABU cha Ujasusi kwa Ofa Maalumu.

Watu 5 @ mtu atapata Kitabu cha "UJASUSI" kwa 30,000/= Badala ya 80,000

Lpia kwa:

Tigo Pesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
(Yericko Nyerere)

Tuma majina yako na ulipo

Kwa Dar ni free delivery

Nje ya Dar nauli ni 8,000/=

IMG_20230815_181539_337.jpg
 
View attachment 2718282
Imekamilika sawa, mbona Kila uchwao dar?
 
Back
Top Bottom