Miaka 11 tangu ya kifo cha nguli wa HIP-HOP: Father Nelly

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,648
75,729
Mwaka 2006 tarehe kama ya leo ilikuwa ya majonzi saana kwa wanafamilia na wapenzi wa utamaduni wa hip-hop na mziki wake jijini arusha, Tanzania na dunia kwa ujumla.

Father nelly au Nelson Chrizostom Buchard alikuwa muasisis wa kundi la x-plastaz lililokuwa na memba 6 akiwemo yeye. He was a real emcee. Kuondoka kwake lilikuwa pengo kubwa kwa utamaduni wa hiphop. Katika uhai wake Yeye na kundi lake waliweza kufanya mziki wa hiphop wenye ladha ya kiafrika kwa kuchanganya tamaduni za kimasai na kimeru ndani yake. Sikiliza Ushata utaelewa.


Nelly alichomwa visu 9 sehemu tofautitofauti za mwili na jirani yake aliyekuwa anaitwa moses yohana kilevo ikiwa ni mwendelezo wa ugomvi kati yake na yeye. Mauti yalimpata alipokimbizwa hospitalini pasipo kupata nafuu yeyote na hivyo kupelekea kuaga dunia.

Moja ya wimbo alioufanya father nelly enzi za uhai wake na picha zake.

ef80b99405fafbab3a61b374daa6b416.jpg




Baada ya kukithiri kwa matukio ya madaga na bisu Arusha..JCB kutoka kundi la WATENGWA jijini Arusha mwaka 2008 alianzisha kampeni ya kupinga dagaz/bisu/visu ikiwa ni moja ya njia ya kumwenzi father na kutokomeza mauaji ya kinyama arusha. Walifanikiwa kurekodi wimbo huu ulioleta mapinduzi makubwa A-city.


RIP FATHER ULIACHA PENGO KUBWA KWENYE UTAMADUNI WA HIPHOP NA MZIKI WAKE.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom