Miaka 10 bila Tanzania Institute Hospital, niliyoyasikia, kuyaona na kusimuliwa na miaka 9 bila gwiji wa moyo nchini Dr. Masau

Hii ishu ya Dr Masau iliibua mjadala mkubwa sana miaka ya nyuma, wegine wakimtuhumu kuwa hakuwa na uzoefu na vigezo vya kuwa daktari bingwa wa maradhi ya moyo, na hatimaye kusababisha vifo vya wagonjwa wengi sana.
Ilikuwa jambo la propaganda zaidi mkuu badala ya ukweli wenyewe,labda upungufu wa wataalamu ambalo hata serikalini ni janga tena kubwa tofauti na hospital binafsi. Kuhusu utaalamu na ubobezi wake, alihitimishwa huko china na Marekani ktk taasisi ya moyo yaani Texas heart institute hospital (THI) alikubalika sana na ndio taasisi ya kwanza kuja nchini kumtafuta baada ya kuvuna sifa Kede Kede huko china. Haikuishia hapo, alikuwa ni mwafrika wa kwanza nchini Ujerumani kuhudumu au kufanya kazi ktk taasisi ya moyo nchini humo. So utaalamu wake ilikubalika duniani kote na ndio maana alisaidiwa kila alichohitaji.
 
Kiufupi katika nchi hii, habari ya 10% inatawala sana na usipokaa na wahusika wenye nguvu na nafasi fulani,utapigwa kwa kuzungukwa mpaka kieleweke mfano THI pia ilikuwa inanyonywa malipo yake na NHIF mathalani 200m zilioneshwa zimelipwa wakati walikuwa wamelipa 40m kati ya 240 zilizokuwa zinadaiwa na Taasisi,hiyo ilitokana na Dr.Masau kutokubali mambo yao ya hovyo kuhujumu nchi kwa kujiongezea malipo yasiyo stahili kama zilivyokuwa baadhi ya taasisi au hospitali zilizokuwa zikilipwa hadi 800m mpaka 1billion kwa mwezi. 10% ni shida na ni ugonjwa mkubwa sana unaolitafuna taifa letu kihuni huni tu.
Daa so sad.

Swali; ukijiona una uadirifu na kutaka kuijenga nchi yako, ufanye nini kuepuka madhira na hadha kama hizi?.
 
Hii ishu ya Dr Masau iliibua mjadala mkubwa sana miaka ya nyuma, wegine wakimtuhumu kuwa hakuwa na uzoefu na vigezo vya kuwa daktari bingwa wa maradhi ya moyo, na hatimaye kusababisha vifo vya wagonjwa wengi sana.

Ni kweli haya yalikuwepo, lakini hizi ni figisu za ngozi nyeusi. Mambo haya yalianzia mbali sana.

Unasema mtu hana vigezo, lakini Texas Heart Institute ikaona ana vigezo na wakahitaji kubaki na mhusika. Ina maana hawa walikubali kushirikiana na incompetent personal ambaye alisoma na kufanya mazoezi kwa vitendo kwao na sehemu ya kazi yake akiwa ameifanya huko?. Ila baadhi ya watu wa MNH ambayo haikuwa na cardiac institute by then ndo wakaona hajui kitu?

In summary:
1: Mambo yalianzia tangu MNH na aintofahamu malipo ya pango kwenye nyumba ya Dr. Masau wakati anasoma, alikuwa amepanga pale Magomeni.

2: Dr. Masau aliporudi ali-introduce idea ya heart institute pale MNH, mkurugenzi wa MNH by then akamwambia akimpa nafasi pale, basi yeye mtoa nafasi ndo awe mkurugenzi na wakashindwana.

3: Dr. Masau, alienda KCMC vs BUGANDO bado mambo yalikuwa magumu.

4: Mwisho alikuja kupata nafasi TMJ, alilipa pango, lakini alikaa muda mrefu akipigwa kalenda kuondoa vifaa bandarini. Mpaka muda wa pango aliolipa uliisha.

5: Pango liliisha pale TMJ, akapata nyumba pale nyuma ya Feza school (Mikocheni), ndio kazi ikaanza baadaye sana. Kwa biinde sana.

6: THI ilitakiwa kuwa expanded na kuimarishwa zaidi, institute za Wajerumani na Marekani wakataka commitment ya serikali wagonjwa kupelekwa pale badala ya India. Wenye mamlaka baada ya kupewa programme, wakakimbia nayo India kusaka hospitali nyingine zinazoweza kufanya huku wakipata 10%.

7: Lilipokuja la ramani kukosewa na msigano wake ndo basi tena, waungwana wakatembelea humohumo.

8: Dr. Masau pamoja na kuumwa, msongo wa mawazo ni sehemu ya vitu vili-accelerate kuondoka kwake mapema. Alipambana na nguvu kubwa hasi, but most of his time smiling kama hakuna kitu kinamsonga.

Nakumbuka katika mazungumzo, aliwahi ku-refer professor mmoja toka Kenya. Alimwambia,"Waafrika ni kama viumbe kaa kwenye ndoo, mmoja anaweza kupanda mpaka juu kwenye chombo walichofungiwa akitaka kutoka, lakini wenzake wakamshika na kumdondosha ndani tena."

Apumzike kwa amani. Walioshiriki walipwe kwa kadri yao pia.

Itoshe kusema ilikuwa purely figisu za ngozi nyeusi kutokutaka waliopiga hatua zaidi kutambulika na kukosa/kutokupewa10%. Bila kujali shida za jamii husika, hawa ndo walikuwa wakieneza sumu kila alikojaribu kupata ushirikiano toka kwa wenye mamlaka.
 
Uhuni tuu, wivu na akili mbovu vilitumika kumfungia Dr Massau, nchi kubwa inahitaji Hospital nyingi tuu za moyo maana hata kule THI kupata nafasi kutibiwa inawezakuchukua muda mrefu sana
 
Back
Top Bottom