Mi-doctor (PhD) na mi-Professor ya Bongo siielewi!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mi-doctor (PhD) na mi-Professor ya Bongo siielewi!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanamayu, May 24, 2012.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Jana katika kipindi cha Jirani cha Redio Tumaini alialikwa mkurungenzi mtendaji wa ESRF ambaye ni PhD holder nafikiri kwenye maeneo ya sayansi ya jamii. Alitoa mfano mmoja mpaka mimi mwenyewe nikashangaa. Ilikuwa hivi: msikilizaji kauliza hivi ni kwa nini tunaambiwa uchumi unakua lakini bado watanzania ni masikini. Dr. akasema kuwa kipimo cha uchumi kukua kinatokana na viashiria au matokeo kama kujengwa kwa barabara na ukuaji huu wa uchumi unatusaidia bila sisi kujua mpaka kufanya tathmini.

  Akatoa mfano kwamba zamani barabara ya Dodoma - Singida haikuwa na lami hivyo ilimlazimu msafiri kulala njiani kwenye hotel ambayo alilipa 15,000/-; baada ya kuwekwa lami msafiri huyo halali tena hotel ile na ku-save 15,000/- hivyo hayo ndio matunda ya kukua kwa uchumi ila mwananchi lazima ayatafiti. Mshangao wangu unakuja na swali je, yule mwenye hotel inakuwaje? Si anakuwa amepoteza 15,000/? Je, ukuaji wa uchumi unaumiza wengine? Je, poverty itaondoka kweli? Mwenye hotel atapeleka kweli watoto wake shule bila shida?

  Ukiangali hata mi-professor yetu ni balaa kwa kuchanganya mambo!

  Hivi kuna tofauti kati ya professor wa Tanzania na UK au USA? Kama zipo ni zipi? Na maanisha u-professor wa ku-publish na sio title ya kufundisha chuo kikuu.
   
 2. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Kwetu sisi shule ni kusoma kwa ajili ya kujibu mitihani ili tupate cheti cha kutusaidia kupata ajira!
   
 3. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 836
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  -Sijaelewa, inamaana unahisi jibu la huyo mkurugenzi halikuwa sahihi na unataka kumkosoa ama?
   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Kuna prof. ana ka-grocary na kaeneo ka kuchemshia supu mtaani kwetu. Mmda mwingi prof huyu yupo hapo kazini kwake. Sasa jiulize kazi za ubunifu zenye tija kwa jamii pana na maendeleo endelevu zitatengenezwa na kina nani? Darasa saba? Wallah tulikotoka karibu, tunakokwenda ni mbali!!
  .
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Ndio nahisi hivyo. Na kama ndivyo economic theory inasema hivyo basi inabidi itazamwe upya. Je, wewe unaona yuko sahihi? Kama ndio usahihi wake ukoje?
   
 6. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  LIKE! Wewe ni great thinker, unaangalia jambo tofauti na mazoea ya kawaida!
   
Loading...