Mhubiri wa kiislamu, mpenzi wa jinsia moja

Status
Not open for further replies.

DOMA

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
944
365
160608130316_gay_mullah_640x360_bbc_nocredit.jpg

Mhubiri mmoja wa Kiislamu ambaye ni mpenzi wa jinsia moja nchini Iran amelazimika kutorokea nchini Uturuki kufuatia tishio kwa maisha yake.

Taha ni mhubiri wa dini ya kiislamu.

Aliyetorokea nchi jirani ya Uturuki akihofia maisha yake katika jamhuri ya kiislamu ya Iran.

'Sheikh'' Taha alikuwa akiwaoza wapenzi wa jinsia moja kisiri siri lakini shauku na uvumi ukaenea kuhusiana na hali yake.

Walimu wenzake wa kidini ''Walihoji kwanini Sheikh na mwalimu wa dini anahusiana na watu waliokufuru dini yake ya Islam kwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja ?''

Wengine walitaka kumuangamiza kwa kumtizama kuwa ''mchafu''

''Walitishia kuniangamiza .'' anasema Taha

Japo Uturuki ni taifa lenye idadi kubwa ya waislamu, utawala wake hauna uhasama wala sera zinazowadhalilisha wapenzi wa jinsia moja

Na sasa Taha anafurahia uhuru wake mpya huko Uturuki na hata hujipamba na kuzuru vilabu vya wapenzi wa jinsia moja katika mji mkuu wa Uturuki Instabul.

Akiwa huko uhamishoni, Mullah Taha angali anaendesha shughuli zake.

Mkimbizi mwenza kutoka Iran Ramtin, pia ni mpenzi wa jinsia moja.

Anataka Tawa amuoze kwa mchumba wake kisiri.

''Kabla ya leo nilikuwa najua kuwa mullah ni baadhi ya wale watu wanaotuchukia sana na ambao hawatupendi kamwe''

'Waliongoza sallah ya kutuangamiza'.

''Lakini sasa wanaswali katika harusi zetu'.

Chanzo:BBC Swahili
 
Mbona kuna baadhi ya wahubiri wa Kikristo wanajihusisha na tabia hizi chafu - mfano: Marehemu Askofu Banana wa Zimbabwe!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom