Mhitimu wa degree ya sheria auza mihogo baada ya kukosa ajira

good girl bravoooo
Anahitaji kupongezwa sana kwa kuona fursa na kuitumia.

Watanzania kelele kila siku.Chukulia bishara ya kuchoma chips kuku iko kila kona Tanzanaia ukiangalia unaweza sema huoni fursa.Lakini wenzetu wazungu mfano KFC wakagundua kuwa Tanzania kuna fursa kubwa ya kuuza biashara ya chips kuku sababu wanaofanya hiyo biashara haiko kwenye viwango vya kumvutia mtu wa kipato cha kati na cha juu kuzila.Wakaja na hoteli za chips kuku tu lakini za HIGH QUALITY kama wawekezaji na wanauza kama nini.Mtanzania waweza kuta anapiga yowe hamna fursa na utaletaje mwekezaji auze chips kuku? Huyo analipa kodi serikalini kubwa tu na anatoa ajira kibao na anaajiri hadi wasomi wa madgrii kibao wakati huyo mwingine kodi tu kupata ya halmashauri hadi ngumi zitembee amwagiwe chips ndipo alipe.

Huyu dada kaona fursa kaichukua chap chap hongera zake.
 
Dhaaa aiseee huyu jamaa Nairobi anauza expensive had mungu hapend
 
Amechukua wazo dogo na akalifanya kwa umaridadi Kama kachumbari iliyo bora , usafi na package nzuri ....

Kwa kuongeza huko thamani ya bidhaa yake bila shaka atapata pesa nzuri ya kumuwezesha kutanua mtaji wake .....

Somo kwa wale wote wanaodhani kuwa kilichopo katikati ya mapaja ndicho utajiri kuliko akili...

Nimeupenda ujasiri wake
 
Mkuu kwani kuhitimu degree ya sheria ndyo tayari unakuwa mwanasheria? Any way huenda ana malengo anatafuta fedha akasome school of Law
 
Ujue wewe jamaa/ dada leo nimekutana na posts zako kutoka kwenye uzi wa kanali kuingia chamani na huu uzi naona kama ukiamua hua unaandika vizuri tu, siku nyingine sijui nini hua kinakukumba unaandika upupu si mchezo.
 
Ukiona degree holder anauza mihogo, mitumba, chips, urembo ama anapiga ukonda basi ujue elimu yetu imepanda thamani kama Euro, na nchi ya viwanda iko mikononi.
 
Na sisi tukiacha kulalamika na maneno mengi tutafika mbali tatizo maneno bila vitendo;hasa vijana na mastori ya kijinga bila kutazama kesho zetu;akili zifunguke
 
Tukiachana na maswala ya kuuza mihogo na degree, nilichokigundua huyu mtotoz neema ni mzuri sana
-dimpoz
-ngozi nzuri
-sura yake
-shingo na lips
**Nangoja ageuke, mleta mada hauna picha zaidi tafadhali.
 
hongera sana neema(mhitimu wa shahada ya sheria) kwa kukata shauri na kuamua kujiajiri.

nina hakika,huyu dada aki-apply nidhamu ya usomi wake na ubunifu ktk biashara, atafika mbali ktk hii project yake ya kuuza mihogo.

kwa east afrika,yawezekana ni Tz pekee ambako ndio tunaanza kupata vijana wasomi walioamua kujiajiri kwa kuanza na biashara za kawaida baada ya kukosa ajira rasmi.

rafiki yangu mmoja jijini nairobi kenya,ana bsc in bio chemistry toka Kenyatta university.

baada ya kusota mda mrefu bila kupata ajira,aliamua kuendeleza talent yake ya kupiga drum instruments kwa kufanya mazoezi kila siku.

leo ninapo tuma post hii,he has became one of the best drummer in kenya...amekuwa akikodishwa kupiga drum ktk matamasha makubwa ya mziki nchini kenya.

MK254
 
Hiyo pia ni mojawapo ya ajira siyo lazima awe serikalini, alisoma ili kupata maarifa na Sheria itamsaidia kuepuka na manyanyaso ya wagambo Wa Jiji na manispaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…