Jumong S
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 7,377
- 10,641
Mara ya kwanza kwenda Kigoma baada ya miaka mingi, ilikuwa mwaka 2009 January kwa bus nikipitia Kahama-Kibondo mpaka Kigoma mjini. It was a terrible journey kuanzia Nyakanazi to Kibondo na maeneo ya Kasulu. Mvua ilikuwa inanyesha na zile barabara utadhani tairi zilikuwa zinachimba makaburi. Nilifika Kigoma usiku nikiwa hoi. Kila nilipokumbuka namna abiria tulivyoshushwa garini na kusukuma basi huku tukitumia makoleo na majembe sikutamani kupita njia ile tena. Nashukuru mazoezi ya JKT yalinisaidia kuhimili suruba zile.
Baada ya project yangu Kigoma, niliamua kurudi Morogoro kwa treni na nilikata tiketi mapema. Kilichonishangaza, siku ya safari nakumbuka ilikuwa Jumapili train ilijaa na siti yangu ilikatiwa watu 3. Train ilijaa sana na uJKT wangu nilisalenda nilipofika Dodoma nikaamua kushuka, next day nilipanda Shabiby to Dar.
Kigoma niliiona ina potentials nyingi sana, watu wake wanapiga kazi sana na biashara imechangamka vizuri. Watu wanalima si mchezo. Wasomi wapo wa kutosha lakini nashangaa kwa nini hapana raisi aliyepakumbuka walau kwa barabara ya rami kuiunganisha na mikoa mingine. Sijui wasomi wake nao hawajitambui na kukumbuka kwao??!
Sina hakika kama reli hii mpya ya standard gauge inawahusu Kigoma, au inachepukia Mwanza tu.
Mh. Magufuli, ikumbuke Kigoma. Kule kuna watanzania pia walipa kodi. Kule kwetu barabara ikikwanguka tu, watu wa serikali huja kwa kasi kutengeneza. Ila mikoa mingine imewekwa kapuni.
Leo nataja Kigoma, ila ipo na mingine. Maintain equality ktk maendeleo.
Kila la kheri ktk ujenzi wa taifa.