Mikopo Chefuchefu
JF-Expert Member
- May 15, 2017
- 3,373
- 6,756
Mheshimiwa Rais, ikikupendeza uwashauri vijana waachane na madesa, wasome vitabu!
Sijawahi ona wanafunzi wavivu wa kusoma vitabu kama wanafunzi wa vyuo vikuu.
Wao kazi yao kubwa ni kusoma madesa (zile notes zinazotolewa na wakufunzi), kupiga group discussion basi. Kazi ndio inakuwa imeishia hapo.
Mwalimu akija kutoa mitihani definitely atabase kwenye yale madesa yake hivyo kuwawezesha wanafunzi wengi kufaulu vizuri tu. Lakini kiuhalisia hili huwafanya wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kuwa weupee vichwani.
Yani ukikutana nao hata kwenye interveiw, wanapita tu kwa kuwa kampuni inahitaji watumishi, na wengi wako ivyo hivyo.
Hili hufanya taifa liwe na wataalam wengi vilaza ambao hawawezi kufikiria nje ya box.
Mimi nilipokuwa nasoma chuo, sikufanikiwa kupata GPA kubwa, lakini niliweka bidii ya kuitumia vizuri library ya chuo na hii imenisaidia sana kuweza kuwa deep kwenye fani yangu kiasi kwamba nikiomba kazi, huwa siulizwagi vyeti na huu ni mwaka wa nane sijawahi kurudi kuchukua cheti ili niweze kupata ajira.
Yani kuna graduates wengine unakutana nao unashindwa kuamini kama kweli mtu alimaliza chuo kikuu, angalau mpaka alete cheti. Wengi ni weupe sana.
Library mpya ikitumika vizuri, angalau itawawezesha wanafunzi wengi kuwa na content kwenye vichwa vyao.