Mheshimiwa Rais fanya ziara kwenye magereza ya mikoani

Uhuru Cape

Member
Nov 1, 2016
48
124
Rais tunakuomba ufanye ziara magereza ya mikoani ujionee matatizo sugu ya askari wako wa magereza;

-Askari wengi wa mikoani awana vitambulisho vya kazi kulingana na vyeo vyao na wengine kama depo namba 26, 27 na 28 hawana kabisa.

-Miladi mingi ya magereza ni kwa ajili ya RPO na wakuu wa magereza.

-Kalakana nyingi zinazotengeneza furniture ni kwa ajili ya kupamba nyumba za maafisa na askari wa vyeo vya chini na raia unapotaka kuchonga gharama yake bora uende mtaani mana ni mara 3 ya mtaani mfano kiwanda cha furniture gereza kuu uyui tabora.

-Askari anapofanya kosa kinyume na sheria ya kazi anapata adhabu sasa moja ya adhabu anakatwa % ya mshaara wake na kupewa account ya kuingiza hiyo pesa ukioji inaenda wapi unaambiwa mfuko wa kamishna sasa ifatilie hiyo mana inafanya wakuu wa gereza kutoa adhabu hiyo ovyo ovyo ili aonekane anamwingizia kamishna kipato na aweze kuendele kubaki na gereza.

Wakuu wengi wa vitengo huwekwa bila vigezo na ndo mana uzalishaji unashuka kila siku.
 
Kuwa kwenye jeshi hili unahitaji uwe na roho ngumu sana, sheria nyingi ni za kikoloni na ni kandamizi kwa askari wa chini.
 
Back
Top Bottom