Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli something is wrong here!

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli something is wrong here!

Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli kusema ukweli na wala hili nisikufiche kama wengine wanavyokuchekea kukuambia ukweli kuwa hata kama unatonyesha jitahada zako na kwakweli nyingi tu tunaanza kuziona na tunakushukuru kwa hilo ILA unatupa Kazi ngumu na kubwa mno ya ' kukutea ' humu mitaani na hata mitandaoni juu ya hii tabia yako ambayo sasa naanza kujiuliza ni ya Wasukuma kweli hawa hawa ninaowajua au labda mwenzetu Wewe ni Mwana Diaspora wa Taifa jingine ambalo halina utu huu wa Kitanzania uliozoeleka?

Katika utamaduni wa Kiafrika ni SIFA mbaya sana tena kwa Kiongozi kabisa wa nchi ( HEAD OF STATE / PRESIDENT ) kukacha kabisa kwenda kuhudhuria ' Misiba ' ambayo yawezekana hata hao waliokufa 99% walikupigia Kura au pengine hata Wazazi wao walihakikisha leo Wewe uwe hapo ulipo.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Mimi GENTAMYCINE itabidi tu univumilie kwani huwa sina tabia ya kumficha Mtu hata kama ni Rafiki yangu au ni Kipenzi changu na hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyoniumba na sitokuja kubadilika hadi naingia Kaburini na nitasema ukweli pale panapostahili na nitakosoa mara moja kama hivi pale ninapoona pana tatizo kwani sikuumbwa kuwa ' Mnafiki ' kama wengi wanaokuzunguka.

Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli hivi una ' matatizo ' gani na Misiba au Maiti? Mbona Mimi nimeishi miaka mitatu ( 3 ) na ' Wananzengo ' wa Kisukuma kule Nyegezi, Luchelele, Nsumba, Malimbe, Mkolani na Buhongwa lakini tulikuwa ' tunajumuika ' nao sana Misibani na hata Mazishini? Hii picha unayotuonyesha Watanzania sasa unataka tukueleweje Mheshimiwa?

Hukwenda Kagera Watu tukajipinda humu kukutetea labda kwa kuhisi kuwa ungejishtukia na kubadilika ikawa vile vile tukasema ' poa ' mara tena ' Wapiganaji ' wako Askari wa Police waliuwawa ' Kinyama ' mno kule Kibiti kama kawaida hukwenda na kama jadi yetu Wanaume tukaja humu tena ' kutiririka ' kwa kukutetea lakini mioyo yetu inatusuta ila tumeshazoea kujikaza ' kisabuni ' kwa kujua labda moyo wako ungajawa na ' aibu ' na ungabadilika kumbe ndiyo kama vile tulikuwa tunapaka ' Upepo ' rangi.

Sasa kali katika yote Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli hili la juzi tu ' masikini ya Mungu ' Taifa limepoteza Wapendwa wetu kabisa tena wakiwa bado wadogo na wana Ndoto za kuja kuwa Watu fulani wa muhimu katika Taifa hili huku kuna wengine pia huwezi jua walikuwa wanataka kuja kuwa ' watiririkaji ' kama GENTAMYCINE lakini safari yao ikafikia tamati katika Mlima wa Rhotie Marera kwa kufariki dunia pamoja na Walimu wao na Dereva wa lile Basi.

Huku ' watetezi ' wako ' tukisikilizia ' kwa mbali kuona labda safari hii ' mshipa ' wako wa ' aibu ' utakunjuka kwa ' kutukuka ' na utahudhuria Msiba ghafla tunaona Press Release kutoka IKULU ya kutoa rambirambi zako na baadae tena tunatangaziwa kuwa Wewe hutokwenda ila utawakilishwa na Makamu wako wa Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Hatukatai kuwa uwepo wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pale Sheikh Amri Abeid Kaluta ni jambo jema ila nadhani uwepo wake pale ' ungenoga ' kama si ' kupendeza ' mno endapo Wewe Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ungekuwa haupo nchini Tanzania ila kumbe umemtuma Yeye ( Makamu wa Rais ) halafu Wewe ' umeunyuti ' zako tu hapo IKULU ya Magogoni na ratiba zako za hapa na pale.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli leo kwa mara ya Kwanza kabisa naungana na maneno yako unayopenda kuyasema kila mara kuwa nakunukuu " Watanzani mniombee " na yawezekana kumbe sisi Watanzania tukawa hatujui huwa unamaanisha nini ila GENTAMYCINE leo nimegundua kuwa yawezekana unaposema tukuombee labda unataka Watanzania tumwambie Mwenyezi Mungu aweze kuukunjua huo moyo wako mgumu, akujaze upendo uliotukuka na pengine aweze kukuondolea Kisirani chako au Chuki zako au Pepo la ukatili ukatili ambalo labda mwenzetu ' umeshalichungulia ' mahala na ukaona kuwa linakuijia na si ajabu tayari limeshaweka makazi ya kudumu katika roho yako kama siyo moyo wako.

Nimalizie tu kwa kusema kuwa Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli unatupa wakati mgumu sana wa ' kukutetea ' kwa matendo ya ajabu kama pia si ya kustaajabisha unayoyafanya. Hivi kabisa huna hata ' uchungu ' na hawa Watoto? Je ukiachillia mbali Wewe kuwa Rais wetu lakini na Wewe si ni Mzazi pia au? Basi hata ' ungetuzuga ' tu Watanzania kwa kumtuma pia Mkeo Mama yetu Janet Magufuli aandamane na Makamu wa Rais kwenda Arusha lakini hata Yeye pia hajaenda.

Hivi kwa mtindo huu hizi kauli ambazo sasa zinaanza ' kutiririka ' kuwa yawezekana haya matukio labda mwenzetu huwa unayajua kupitia ' African Traditional Science / Ndumbaism ' wakisema kuwa huenda mwenzetu unatoa ' sadaka ' unadhani zitakuwa na mashaka? Hivi na Wewe ungekuwa ' unajichanganya ' Misibani ' umbea ' huu wa sisi ' Waswahili ' kuwa unafanya ' shiriki ' ungeanza kushika kasi na hata kuanza kuaminika na wengi?

Nakuruhusu unichukie kama utapenda au kujisikia kufanya hivyo ILA nakuomba tu haya ambayo huwa nakuandikia uwe unayachukua na kuyafanyia Kazi kwani kwa ' Zawadi ' ya Kipekee kabisa ambayo nimepewa na Mwenyezi Mungu yawezekana Mimi pamoja na Wana JamiiForums wote humu tukawa ni ' Tochi ' yako nzuri ya kukusaidia utuongoze vyema ila bahati mbaya sana mwenzetu hii ' Tochi ' unaichukia na unaidharau sana.

Nawapeni pole zangu za dhati sana Wafiwa wote, Uongozi mzima wa Shule ya Lucky Vicent na Walimu wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wana Arusha wote na Watanzania kwa ujumla kwa Msiba huu mkubwa na mzito sana na kikubwa sote tuungane na tuwaombee maziko na makazi mema huko katika Nyumba zao za Milele hawa Wapendwa wetu. Tuliwapenda ila Mwenyezi Mungu kawapenda zaidi na Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amen.
Jaman wapendwa fumbeni macho na tuombe
 
hahahaha Nyani Ngabu ona huku....

Hahaaaa what do you expect from wale wanyama....

Alipokamatwa Ney wa Mitego walilia na kumlaumu rais.

Rais alipoingilia/aliposhauri kuwa huyo dogo aachiwe napo wakalalamika eti anaingilia mamlaka yasiyo yake.

Hahahaaa....sasa sijui walitaka Ney aendelee kunyea debe?

Hata hawaeleweki hawa watu.
 
Angekuwepo angesema ile ajali haikuletwa na serikali Kwa hiyo chapeni kazi tu.
Huyu Rais wangu bana huwa ni kiboko.
Ungesikia: wakati naomba kura nilisema nitaleta ajalii? Nilisema nitaleta?. bora hukuja aise angeongea pumba pale chuga angepigwa hata mawe, sio kagera pale mtu anaongea shudu halafu anashangiliwa. Pale ukiongea shudu tu, utapata unacho stahili.
 
Endelea kuisoma namba, umeonyesha jinsi unabyomuwazia kila sekunde. VIZURI
Napenda kuwapongeza na kuwashukuru washauri wa rais kwa kutumia weledi wao kwa kumshauri asihudhurie msiba wa Leo wa watoto wetu sheikh abeid karume. Kwasababu jamaa angetuongezea majonzi na simanzi kwa kauli zake mbofumbofu.

Moyo ulikuwa unadunda labda ataibuka ghafla lahaula haikuwa hivyo.

Sasa kwa huo weledi hawa washauri waliotumia pia wamshauri Sizonje utawala bora na kuinua uchumi wa nchi.

RAMBIRAMBI ZIWAFIKIE WALENGWA
mh!!
 
Napenda kuwapongeza na kuwashukuru washauri wa rais kwa kutumia weledi wao kwa kumshauri asihudhurie msiba wa Leo wa watoto wetu sheikh abeid karume. Kwasababu jamaa angetuongezea majonzi na simanzi kwa kauli zake mbofumbofu.

Moyo ulikuwa unadunda labda ataibuka ghafla lahaula haikuwa hivyo.

Sasa kwa huo weledi hawa washauri waliotumia pia wamshauri Sizonje utawala bora na kuinua uchumi wa nchi.

RAMBIRAMBI ZIWAFIKIE WALENGWA

Mimi nimeona ID yako nikajua Rais ameruhusu watu tupate Fao la Kujitoa.....Anyway.....yote mema!
 
Napenda kuwapongeza na kuwashukuru washauri wa rais kwa kutumia weledi wao kwa kumshauri asihudhurie msiba wa Leo wa watoto wetu sheikh abeid karume. Kwasababu jamaa angetuongezea majonzi na simanzi kwa kauli zake mbofumbofu.

Moyo ulikuwa unadunda labda ataibuka ghafla lahaula haikuwa hivyo.

Sasa kwa huo weledi hawa washauri waliotumia pia wamshauri Sizonje utawala bora na kuinua uchumi wa nchi.

RAMBIRAMBI ZIWAFIKIE WALENGWA
We mpuuzi mmoja. Watu kama nyie mkatafute nchi yenu mwondoke tanzania yetu mnatuletea mikosi tu
 
Napenda kuwapongeza na kuwashukuru washauri wa rais kwa kutumia weledi wao kwa kumshauri asihudhurie msiba wa Leo wa watoto wetu sheikh abeid karume. Kwasababu jamaa angetuongezea majonzi na simanzi kwa kauli zake mbofumbofu.

Moyo ulikuwa unadunda labda ataibuka ghafla lahaula haikuwa hivyo.

Sasa kwa huo weledi hawa washauri waliotumia pia wamshauri Sizonje utawala bora na kuinua uchumi wa nchi.

RAMBIRAMBI ZIWAFIKIE WALENGWA
Nahic wewe ulikuwa mpigaji ndiyo maana upo kwenye kundi la kutokubali kuambiwa ukweli.
 
Acha tujifariji kwa hilo kwani jamaa sio konfota ini chifu hata kidogo....baba jeuri watoto wakimwona uvungu unawahusu
Hasara tupu watoto wakidigitali hawapendi kuelewa ukweli, maana hao wanajifanya wanajua kila kitu.
Na ndiyo maana wanaona wanaonewa kwa kila jambo kwa sababu ya akili mgando.
 
Hoja za wana JF umezishindwa maana faster unakimbilia matusi kama hujafunzwa na wazazi wako na watu wa dini.. utakuwa Unalaana wewe si bure... wengi tumekupuuza sasa unarukia kwa Raisi soon utapotezwa trust me ukiendelea na upuuzi wako... wewe unajua sababu za raisi kitokwenda? Ati mtetezi wa raisi mtandaoni unaandika huku umebana pua. .. humu watu wanatoa Stress tu Raisi hafutilii kimaanani. Acha Kucheza na Taasisi ya Uraisi msione nchi inaenda tu vyombo vinafanya kazi... sina haja ya kukuonya tena.
Lazima wewe mgonjwa ila hujijui tu
 
Wamekufa watu wangapi kabla ya hawa, kusikitika kiubinadamu ni sawa lazima tuumie, ila hili la kusema jamaa anakwepa misiba mi sawaelewi. Kwani uwepo wake ungepunguzaje majonzi?
 
Back
Top Bottom