Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli something is wrong here!

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli something is wrong here!

Angeenda pia
tungesikia hana kazi ya kufanya.

wapumzike kwa Amani wadogo zetu & Pole ziwafikie wafiwa wote.
Wawe na imani katika kipindi hiki kigumu
Kwa hiyo wote wanaoenda kwenye misiba hawana kazi za kufanya? Duuuuu hapo umechemka vibaya.
 
Tanzania tuna watu wa ajabu sana kazi kutafuta kasoro feki kila kukicha! Kumbuka Uraisi ni taasisi ,ni ofisi, na ndo maana ana wasaidizi wengi ili wamsaidie katika ujenzi wa taifa , na taaisisi hiyo tayari ilikuwepo pale msibani. tatizo ulitaka kuona kipara cha JPM upate la kuandika, bora amebaki huko dar! wazushi hamuachi kuandika upupu!

Kwanza nafuahi sana kwa kuweza kulitumia neno langu nililoliingiza humu la ' Upupu ' na sasa naona baadhi yenu mnalitumia kama ambavyo mmeshazoea kuyatumia yale mengine ya Popoma, Ngumbaru na hili la Kutukuka. Hiyo ndiyo ' impact ' ya GENTAMYCINE ambapo huwa naanzisha na wengine mtake msitake lazima tu mtavutiwa kunifuata na kuniiga na ndiyo mwisho wa siku nasema GENTAMYCINE ama hakika ni ' Talented and Charismatic '.

Kuhusu ' mada ' Kuu kwahiyo Mkuu kwakuwa Urais ni Taasisi basi kila ' Msiba ' tu ukitokea ndiyo awe ' anaingia mitini ? ' Hivi unajielewa au kujitambua Wewe kweli Kichwani mwako? Unajua umuhimu wa yale yaliyotokea Kagera, Kibiti na hili la juzi tu la Rhotie Marera Mkoani Arusha?

Kama unafanya Kazi hapo IKULU au umeajiriwa mahala popote pale ' waliokuajiri ' waandike tu wana ' Mtumishi ' hewa kwani ujengaji wako wa hoja umeonyesha kabisa jinsi ulivyo ' mtupu ' kabisa katika huo Mbichwa wako mkubwa kama Tairi za Magari ya Migodini.
 
Mi nadhani mh JPM anajaribu kurudisha hadhi ya urais pale ikulu, ikulu ilishafikia hadhi ya kituo cha daladala hata mateja walikua wanaenda kupiga selfie na chata. Hata kwa wakatoliki cardinal, askofu,papa ni watu adimu kuonekana makanisani.

Ukituma post moja tu inatosha swine, kwani unatuchosha kurudia rudia kusoma kitu kile kile halafu kibaya zaidi ni ' Upupu ' mtupu.
 
mwacheni huwezi jua amepatwa na nini? ni mtu mzima yule anajua anachokifanya mbona kagera alienda baadaye kusalimia labda ana moyo mwepesi analia zake ndani, kumuona rais analia nje aibu nayo...mwacheni akipata nguvu atakuja kutoa pole.
Nadhani watu makini wameshauri asiende, labda walihisi ataropoka maneno kama yale aliyotoa Mbele ya watu wenye huzuni kwa maafa ya tetemeko pale Kagera. Hebu fikiria umefiwa alafu unasubiri neno la faraja mara mkuu wa nchi anakupa habari za ngono, katerero nakadhalika, ndiyo maana huwa anaomba sana aombewe na naamini maombi yanafika kwa Mungu vinginevyo siku ile angeweza kupigwa mawe
 
Katika utamaduni wa Kiafrika ni SIFA mbaya sana tena kwa Kiongozi kabisa wa nchi ( HEAD OF STATE / PRESIDENT ) kukacha kabisa kwenda kuhudhuria ' Misiba ' ambayo yawezekana hata hao waliokufa 99% walikupigia Kura au pengine hata Wazazi wao walihakikisha leo Wewe uwe hapo ulipo
dhana yako inachagizwa na mazoea ya Kikwete. Serikali inatarajiwa ku deliver entitlements kwa wananchi. Kuhudhuria misiba siyo sehemu ya wajibu au delivery mechanism ya entitlements hizo, ila kisayansi, masuala ya kuhudhiria misiba, ngoma, miziki au hata kushiriki sherehe za kimila tunaita low politics ambzao Rais anaweza kushiriki iwapo kukiwa na lazima ya ku-fill gap kutokana na kushindwa entitlements delivery katuka high politics. Magufuli is right, and nevertheless, the Government was well represented thereat.
 
Mbona mwalimu nyerere alikuwa hahudhurii mnataka kuanzisha tabia gani.mwakamu wa rais ndio moja ya kazi zake.
Jamani anazingua mbona kwa Christina lissu alienda
Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli kusema ukweli na wala hili nisikufiche kama wengine wanavyokuchekea kukuambia ukweli kuwa hata kama unatonyesha jitahada zako na kwakweli nyingi tu tunaanza kuziona na tunakushukuru kwa hilo ILA unatupa Kazi ngumu na kubwa mno ya ' kukutea ' humu mitaani na hata mitandaoni juu ya hii tabia yako ambayo sasa naanza kujiuliza ni ya Wasukuma kweli hawa hawa ninaowajua au labda mwenzetu Wewe ni Mwana Diaspora wa Taifa jingine ambalo halina utu huu wa Kitanzania uliozoeleka?

Katika utamaduni wa Kiafrika ni SIFA mbaya sana tena kwa Kiongozi kabisa wa nchi ( HEAD OF STATE / PRESIDENT ) kukacha kabisa kwenda kuhudhuria ' Misiba ' ambayo yawezekana hata hao waliokufa 99% walikupigia Kura au pengine hata Wazazi wao walihakikisha leo Wewe uwe hapo ulipo.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Mimi GENTAMYCINE itabidi tu univumilie kwani huwa sina tabia ya kumficha Mtu hata kama ni Rafiki yangu au ni Kipenzi changu na hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyoniumba na sitokuja kubadilika hadi naingia Kaburini na nitasema ukweli pale panapostahili na nitakosoa mara moja kama hivi pale ninapoona pana tatizo kwani sikuumbwa kuwa ' Mnafiki ' kama wengi wanaokuzunguka.

Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli hivi una ' matatizo ' gani na Misiba au Maiti? Mbona Mimi nimeishi miaka mitatu ( 3 ) na ' Wananzengo ' wa Kisukuma kule Nyegezi, Luchelele, Nsumba, Malimbe, Mkolani na Buhongwa lakini tulikuwa ' tunajumuika ' nao sana Misibani na hata Mazishini? Hii picha unayotuonyesha Watanzania sasa unataka tukueleweje Mheshimiwa?

Hukwenda Kagera Watu tukajipinda humu kukutetea labda kwa kuhisi kuwa ungejishtukia na kubadilika ikawa vile vile tukasema ' poa ' mara tena ' Wapiganaji ' wako Askari wa Police waliuwawa ' Kinyama ' mno kule Kibiti kama kawaida hukwenda na kama jadi yetu Wanaume tukaja humu tena ' kutiririka ' kwa kukutetea lakini mioyo yetu inatusuta ila tumeshazoea kujikaza ' kisabuni ' kwa kujua labda moyo wako ungajawa na ' aibu ' na ungabadilika kumbe ndiyo kama vile tulikuwa tunapaka ' Upepo ' rangi.

Sasa kali katika yote Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli hili la juzi tu ' masikini ya Mungu ' Taifa limepoteza Wapendwa wetu kabisa tena wakiwa bado wadogo na wana Ndoto za kuja kuwa Watu fulani wa muhimu katika Taifa hili huku kuna wengine pia huwezi jua walikuwa wanataka kuja kuwa ' watiririkaji ' kama GENTAMYCINE lakini safari yao ikafikia tamati katika Mlima wa Rhotie Marera kwa kufariki dunia pamoja na Walimu wao na Dereva wa lile Basi.

Huku ' watetezi ' wako ' tukisikilizia ' kwa mbali kuona labda safari hii ' mshipa ' wako wa ' aibu ' utakunjuka kwa ' kutukuka ' na utahudhuria Msiba ghafla tunaona Press Release kutoka IKULU ya kutoa rambirambi zako na baadae tena tunatangaziwa kuwa Wewe hutokwenda ila utawakilishwa na Makamu wako wa Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Hatukatai kuwa uwepo wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pale Sheikh Amri Abeid Kaluta ni jambo jema ila nadhani uwepo wake pale ' ungenoga ' kama si ' kupendeza ' mno endapo Wewe Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ungekuwa haupo nchini Tanzania ila kumbe umemtuma Yeye ( Makamu wa Rais ) halafu Wewe ' umeunyuti ' zako tu hapo IKULU ya Magogoni na ratiba zako za hapa na pale.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli leo kwa mara ya Kwanza kabisa naungana na maneno yako unayopenda kuyasema kila mara kuwa nakunukuu " Watanzani mniombee " na yawezekana kumbe sisi Watanzania tukawa hatujui huwa unamaanisha nini ila GENTAMYCINE leo nimegundua kuwa yawezekana unaposema tukuombee labda unataka Watanzania tumwambie Mwenyezi Mungu aweze kuukunjua huo moyo wako mgumu, akujaze upendo uliotukuka na pengine aweze kukuondolea Kisirani chako au Chuki zako au Pepo la ukatili ukatili ambalo labda mwenzetu ' umeshalichungulia ' mahala na ukaona kuwa linakuijia na si ajabu tayari limeshaweka makazi ya kudumu katika roho yako kama siyo moyo wako.

Nimalizie tu kwa kusema kuwa Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli unatupa wakati mgumu sana wa ' kukutetea ' kwa matendo ya ajabu kama pia si ya kustaajabisha unayoyafanya. Hivi kabisa huna hata ' uchungu ' na hawa Watoto? Je ukiachillia mbali Wewe kuwa Rais wetu lakini na Wewe si ni Mzazi pia au? Basi hata ' ungetuzuga ' tu Watanzania kwa kumtuma pia Mkeo Mama yetu Janet Magufuli aandamane na Makamu wa Rais kwenda Arusha lakini hata Yeye pia hajaenda.

Hivi kwa mtindo huu hizi kauli ambazo sasa zinaanza ' kutiririka ' kuwa yawezekana haya matukio labda mwenzetu huwa unayajua kupitia ' African Traditional Science / Ndumbaism ' wakisema kuwa huenda mwenzetu unatoa ' sadaka ' unadhani zitakuwa na mashaka? Hivi na Wewe ungekuwa ' unajichanganya ' Misibani ' umbea ' huu wa sisi ' Waswahili ' kuwa unafanya ' shiriki ' ungeanza kushika kasi na hata kuanza kuaminika na wengi?

Nakuruhusu unichukie kama utapenda au kujisikia kufanya hivyo ILA nakuomba tu haya ambayo huwa nakuandikia uwe unayachukua na kuyafanyia Kazi kwani kwa ' Zawadi ' ya Kipekee kabisa ambayo nimepewa na Mwenyezi Mungu yawezekana Mimi pamoja na Wana JamiiForums wote humu tukawa ni ' Tochi ' yako nzuri ya kukusaidia utuongoze vyema ila bahati mbaya sana mwenzetu hii ' Tochi ' unaichukia na unaidharau sana.

Nawapeni pole zangu za dhati sana Wafiwa wote, Uongozi mzima wa Shule ya Lucky Vicent na Walimu wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wana Arusha wote na Watanzania kwa ujumla kwa Msiba huu mkubwa na mzito sana na kikubwa sote tuungane na tuwaombee maziko na makazi mema huko katika Nyumba zao za Milele hawa Wapendwa wetu. Tuliwapenda ila Mwenyezi Mungu kawapenda zaidi na Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amen.
 
MIMI NILISHANGAA SANA SIKU ILE WALE POLICE NANE WALIVYOAGWA, JAMMA ALIKUA HAPA HAPA DAR NA ALIENDA KUFUNGUA HOSTELI, KUPIGA PICHA NA KUCHEKA NA WATU WA BONGO MOVIE NA BASHITE. HIVI HOSTELI SI ZINGE NGOJA HATA KESHO YAKE AU SIKU NYINGINE? something is wrong!!!!!!!!
 
Naona watiririkaji wanaanza kunyosha mikono.Hakuna siri duniani.Chanzo kitajulikana tu.
 
Nimekuwa nikimfuatilia sana mleta mada, mara ajiite mnyarwanda wa gitale, mzanaki wa mara, aliitetea ccm enzi zile za uchaguzi ni balaa, lakini hivi karibuni ukifatilia mada zake utagundua kuwa anasoma number tena za Kirumi sasa hivi, teuzi zimepita kushoto, tulia mkuu magu atakukumbuka tu usihofu.
Siku urais utakapo patikana bila kuchakachua matokeo ndio hadhi ya urais utakapo rudi,

"mtanifanya nini sasa maana yupo juu ya sheria atakuwa rais tena kwa njia yoyote ile mpaka muda wake uishe taka usitake."
 
Kwa hiyo
Jamani anazingua mbona kwa Christina lissu alienda
haendi kwenye misiba ya kitaifa bali ya watu binafsi? Kwamba kwa Christina Lisu na Masaburi alienda,why not Kagera,kwa Polisi na sasa kwa watoto wa Arusha? Atakuwa anajua sababu zake bila shaka.
 
Acheni kumuandama mheshiniwa rais bana na chokochoko zenu hizo.
Rais hana shida yoyote kama ni midiba mbona ana hudhuria vizuri tu.
Alihudhuria msiba wa Didas Masaburi pia akaenda Chato kuhudhururia msiba wa yule Mzee jirani yake kuke chato.
Inategemea hawa wengine mnaowaongelea nini wana ukaribu gani naye.
 
Angeenda pia
tungesikia hana kazi ya kufanya.

wapumzike kwa Amani wadogo zetu & Pole ziwafikie wafiwa wote.
Wawe na imani katika kipindi hiki kigumu
He is not only a commander in chief but also a comforter in chief ungelijua hilo usingetoa huo upuuzi wako
 
Siku urais utakapo patikana bila kuchakachua matokeo ndio hadhi ya urais utakapo rudi,

"mtanifanya nini sasa maana yupo juu ya sheria atakuwa rais tena kwa njia yoyote ile mpaka muda wake uishe taka usitake."
ndio walewale kwani wanaoshindwa nao wameshindwa kuchakchua au wamechakachus vibaya.hizo akili za zezeta
 
Shame on you, not me. Maisha yanipige mimi jamaa angu, wewe ndio yamekupiga mpaka unaongea shudu tu ili ulipwa.

Ha ha ha haaaaa

Kumbe unanilipa wewe embu jirudishie haraka ulipoziweka.
 
Back
Top Bottom