Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli something is wrong here!

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli something is wrong here!

Ngoja afanye anachodhani ni sahihi kwa sababu hatuna sheria ya kutaka ulazima wa kwenda. Akienda muwakilishi ni Sawa na yeye kwenda.
Pili sidhani kama ni kweli huwa hapendi maana ameudhulia misiba kadhaa kama aonavyo yeye sio tutakavyo. Leo akisema aende yeye Kila msiba na majanga au Ajali hakuna iliyobora zaidi ya nyingine hivyo basi kwa uzembe huu mabarabarani nusu ya Muda wake utaishia kwenye misiba. Sioni kama suala hilo linauhusiano wowote na kabila la mtu Bali ni utashi na maamuzi ya muhusika. Kuleta hoja za kikabila karne hii ni udhaifu
Je akifa Waziri mkuu atatuma mwakilishi msibani? Au ndio tunawekwa kwenye matabaka?
 
Kuhudhuria msiba sio kipimo cha utu!!
wewe mwenyewe uko kwenye keyboard na haujaenda msibani.

Na kwa usahihi kabisa misiba ya waliofariki itafanyika leo na kesho maeneo mbalimbali nchini...unategemea rais atajigawaje?

Ambaye hajawahi kufiwa na mtoto tena wa rika la miaka 12-14 ndio atabaki kuchonga sana.


Mkuu;
Na wewe unaona umesema kweli?? Haya, tukuulize; Mantiki ya kwenda kuiweka miili ile pale uwanjani na viongozi kwenda pale, kwako ni kusherehekea?? Mbona hujiulizi kwa nini hawakutoa ruhusa tu kuwa kila mzazi aende kujichukulia marehemu wake akazike kwani hatuna viongozi wa kwenda kuhudhuria kila msiba??
Naomba nikueleweshe kuwa, mazishi yalikuwa leo, kesho ni kufukia tu. Pale waliwekwa kuagwa na viongozi wetu kwa niaba ya kila mtanzania. Kesho ni sehemu ya familia husika, leo ilikuwa ni Kitaifa.
Simung'unyi maneno; Rais, angekuwa amewafariji Watz wote yeye kama baba yetu aliyepo leo, angelifika, hata kwa dakika 10 tu. Aseme, Nimeacha shughuli zote kwa ajili ya hili tukio la kusikitisha mno. TUNGEMUELEWA.
 
Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli kusema ukweli na wala hili nisikufiche kama wengine wanavyokuchekea kukuambia ukweli kuwa hata kama unatonyesha jitahada zako na kwakweli nyingi tu tunaanza kuziona na tunakushukuru kwa hilo ILA unatupa Kazi ngumu na kubwa mno ya ' kukutea ' humu mitaani na hata mitandaoni juu ya hii tabia yako ambayo sasa naanza kujiuliza ni ya Wasukuma kweli hawa hawa ninaowajua au labda mwenzetu Wewe ni Mwana Diaspora wa Taifa jingine ambalo halina utu huu wa Kitanzania uliozoeleka?

Katika utamaduni wa Kiafrika ni SIFA mbaya sana tena kwa Kiongozi kabisa wa nchi ( HEAD OF STATE / PRESIDENT ) kukacha kabisa kwenda kuhudhuria ' Misiba ' ambayo yawezekana hata hao waliokufa 99% walikupigia Kura au pengine hata Wazazi wao walihakikisha leo Wewe uwe hapo ulipo.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Mimi GENTAMYCINE itabidi tu univumilie kwani huwa sina tabia ya kumficha Mtu hata kama ni Rafiki yangu au ni Kipenzi changu na hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyoniumba na sitokuja kubadilika hadi naingia Kaburini na nitasema ukweli pale panapostahili na nitakosoa mara moja kama hivi pale ninapoona pana tatizo kwani sikuumbwa kuwa ' Mnafiki ' kama wengi wanaokuzunguka.

Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli hivi una ' matatizo ' gani na Misiba au Maiti? Mbona Mimi nimeishi miaka mitatu ( 3 ) na ' Wananzengo ' wa Kisukuma kule Nyegezi, Luchelele, Nsumba, Malimbe, Mkolani na Buhongwa lakini tulikuwa ' tunajumuika ' nao sana Misibani na hata Mazishini? Hii picha unayotuonyesha Watanzania sasa unataka tukueleweje Mheshimiwa?

Hukwenda Kagera Watu tukajipinda humu kukutetea labda kwa kuhisi kuwa ungejishtukia na kubadilika ikawa vile vile tukasema ' poa ' mara tena ' Wapiganaji ' wako Askari wa Police waliuwawa ' Kinyama ' mno kule Kibiti kama kawaida hukwenda na kama jadi yetu Wanaume tukaja humu tena ' kutiririka ' kwa kukutetea lakini mioyo yetu inatusuta ila tumeshazoea kujikaza ' kisabuni ' kwa kujua labda moyo wako ungajawa na ' aibu ' na ungabadilika kumbe ndiyo kama vile tulikuwa tunapaka ' Upepo ' rangi.

Sasa kali katika yote Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli hili la juzi tu ' masikini ya Mungu ' Taifa limepoteza Wapendwa wetu kabisa tena wakiwa bado wadogo na wana Ndoto za kuja kuwa Watu fulani wa muhimu katika Taifa hili huku kuna wengine pia huwezi jua walikuwa wanataka kuja kuwa ' watiririkaji ' kama GENTAMYCINE lakini safari yao ikafikia tamati katika Mlima wa Rhotie Marera kwa kufariki dunia pamoja na Walimu wao na Dereva wa lile Basi.

Huku ' watetezi ' wako ' tukisikilizia ' kwa mbali kuona labda safari hii ' mshipa ' wako wa ' aibu ' utakunjuka kwa ' kutukuka ' na utahudhuria Msiba ghafla tunaona Press Release kutoka IKULU ya kutoa rambirambi zako na baadae tena tunatangaziwa kuwa Wewe hutokwenda ila utawakilishwa na Makamu wako wa Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Hatukatai kuwa uwepo wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pale Sheikh Amri Abeid Kaluta ni jambo jema ila nadhani uwepo wake pale ' ungenoga ' kama si ' kupendeza ' mno endapo Wewe Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ungekuwa haupo nchini Tanzania ila kumbe umemtuma Yeye ( Makamu wa Rais ) halafu Wewe ' umeunyuti ' zako tu hapo IKULU ya Magogoni na ratiba zako za hapa na pale.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli leo kwa mara ya Kwanza kabisa naungana na maneno yako unayopenda kuyasema kila mara kuwa nakunukuu " Watanzani mniombee " na yawezekana kumbe sisi Watanzania tukawa hatujui huwa unamaanisha nini ila GENTAMYCINE leo nimegundua kuwa yawezekana unaposema tukuombee labda unataka Watanzania tumwambie Mwenyezi Mungu aweze kuukunjua huo moyo wako mgumu, akujaze upendo uliotukuka na pengine aweze kukuondolea Kisirani chako au Chuki zako au Pepo la ukatili ukatili ambalo labda mwenzetu ' umeshalichungulia ' mahala na ukaona kuwa linakuijia na si ajabu tayari limeshaweka makazi ya kudumu katika roho yako kama siyo moyo wako.

Nimalizie tu kwa kusema kuwa Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli unatupa wakati mgumu sana wa ' kukutetea ' kwa matendo ya ajabu kama pia si ya kustaajabisha unayoyafanya. Hivi kabisa huna hata ' uchungu ' na hawa Watoto? Je ukiachillia mbali Wewe kuwa Rais wetu lakini na Wewe si ni Mzazi pia au? Basi hata ' ungetuzuga ' tu Watanzania kwa kumtuma pia Mkeo Mama yetu Janet Magufuli aandamane na Makamu wa Rais kwenda Arusha lakini hata Yeye pia hajaenda.

Hivi kwa mtindo huu hizi kauli ambazo sasa zinaanza ' kutiririka ' kuwa yawezekana haya matukio labda mwenzetu huwa unayajua kupitia ' African Traditional Science / Ndumbaism ' wakisema kuwa huenda mwenzetu unatoa ' sadaka ' unadhani zitakuwa na mashaka? Hivi na Wewe ungekuwa ' unajichanganya ' Misibani ' umbea ' huu wa sisi ' Waswahili ' kuwa unafanya ' shiriki ' ungeanza kushika kasi na hata kuanza kuaminika na wengi?

Nakuruhusu unichukie kama utapenda au kujisikia kufanya hivyo ILA nakuomba tu haya ambayo huwa nakuandikia uwe unayachukua na kuyafanyia Kazi kwani kwa ' Zawadi ' ya Kipekee kabisa ambayo nimepewa na Mwenyezi Mungu yawezekana Mimi pamoja na Wana JamiiForums wote humu tukawa ni ' Tochi ' yako nzuri ya kukusaidia utuongoze vyema ila bahati mbaya sana mwenzetu hii ' Tochi ' unaichukia na unaidharau sana.

Nawapeni pole zangu za dhati sana Wafiwa wote, Uongozi mzima wa Shule ya Lucky Vicent na Walimu wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wana Arusha wote na Watanzania kwa ujumla kwa Msiba huu mkubwa na mzito sana na kikubwa sote tuungane na tuwaombee maziko na makazi mema huko katika Nyumba zao za Milele hawa Wapendwa wetu. Tuliwapenda ila Mwenyezi Mungu kawapenda zaidi na Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amen.
Kawaida head of state huzika head of state mwenzake jifunze kutoka kwa malkia! Misiba kama hii ana wa kutuma. Kwa hili JK alilete ukakasi
 
Huyu mtu ana roho kama ya shetani.roho mbayaa.
 
Nitakua wa mwisho kumlaumu katika hili.
Uraisi nafikiri si kuamua kila unachotaka.

Huenda alitamani kwenda ila taasisi ikaona hapaswi kwenda, huwezi jua.

Ila labda kama itatokea akatoa maneno tatanishi kama bk.....hapo sasa ndio tunaweza kutia neno.
 
Angeenda pia
tungesikia hana kazi ya kufanya.

wapumzike kwa Amani wadogo zetu & Pole ziwafikie wafiwa wote.
Wawe na imani katika kipindi hiki kigumu
na yumkini wangesema kwani kila msiba ama janga lazima tu yeye ndio aende hakuna wasaidizi wake.
 
kwanza tu nikupe pole kuwa wewe si jasiri ni muoga sana na hizo sifa ulianza kueleza kwenye hii makala haunazo embu leo toa maoni yako kwakutumia ID isiyo mficho yaani weka namba yako ya simu ili utumiwe meseji kuwa ujumbe wako umefika pili usitake kumpangia mh raisi majukumu kumbuka raisi ni taasisi hivyo akiwakilishwa na makamu wake ni sawa na yeye kuwa yupo pale .yaani makamu kama mwenyewe hayupo pale basi ndiye mkuu.i hope umeelewa.kwa kuanzia hapo.

Nilishaacha ' kujibizana ' na ' Hopeless Creatures ' zamani sana.
 
Mwingine huyu.....kha!
Pole tujifunze kupoke tusiyoyapenda! Isiwe ni tatizo la ushabiki kama simba na yanga! Tambwe akiwa simba kwa wanasimba ni kifaa ila kwa wanayanga ni malizozo. Akihamia yanga I amua vice versa.
 
Kwani kasahau maneno ya Lema? Kwani hajitaki? Na pia Raisi angesikia kichefuchefu kumuona Lema. Bora hajaenda.

Ila mleta Mada kichwani hayupo Sawa kiakili tena kitambo tu kagombana kwa matusi karibu nusu ya wana jf ni wa kumpuuza tu... ndio waandishi makajanja aliyoisema Mwakyembe. Pia mwambieni a edit maneno yake vichapizi vingi mno.
 
Wachangiaji wote hapo juu mnaonyesha mna leta siasa kwenye mambo ya msingi. Raisi ni mkuu wa nchi hivyo safari zake zote zinahitaji maandalizi ndo maana akawa na washauri. Safari za mkuu yeyote wa nchi ni lazima zizingatie usalama wake tofauti na nyinyi mnaokurupuka bila hata kunawa uso. So msimlinganishe Raisi na mtu mwingine yeyote na safari zake zote zipo kwenye ratiba. Acheni lawama ambazo wala haziwasaidii lolote. Angekuwa hajali hata salaam asingetuma.
Aiseee kumbe hata safari za majanga mbalimbali ziko kwenye ratiba yakeee
 
Ile ya Kagera na Askari 8 akaopt kwenda kufungua hostel, pale ndipo nilipoondoa neno utu katika fikra za mkulu. Kwa hii ya Arusha hata sikutaka kufikiria.
 
Napenda kuwapongeza na kuwashukuru washauri wa rais kwa kutumia weledi wao kwa kumshauri asihudhurie msiba wa Leo wa watoto wetu sheikh abeid karume. Kwasababu jamaa angetuongezea majonzi na simanzi kwa kauli zake mbofumbofu.

Moyo ulikuwa unadunda labda ataibuka ghafla lahaula haikuwa hivyo.

Sasa kwa huo weledi hawa washauri waliotumia pia wamshauri Sizonje utawala bora na kuinua uchumi wa nchi.

RAMBIRAMBI ZIWAFIKIE WALENGWA
 
Back
Top Bottom