Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli something is wrong here!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
60,422
120,747
Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli kusema ukweli na wala hili nisikufiche kama wengine wanavyokuchekea kukuambia ukweli kuwa hata kama unatonyesha jitahada zako na kwakweli nyingi tu tunaanza kuziona na tunakushukuru kwa hilo ILA unatupa Kazi ngumu na kubwa mno ya ' kukutea ' humu mitaani na hata mitandaoni juu ya hii tabia yako ambayo sasa naanza kujiuliza ni ya Wasukuma kweli hawa hawa ninaowajua au labda mwenzetu Wewe ni Mwana Diaspora wa Taifa jingine ambalo halina utu huu wa Kitanzania uliozoeleka?

Katika utamaduni wa Kiafrika ni SIFA mbaya sana tena kwa Kiongozi kabisa wa nchi ( HEAD OF STATE / PRESIDENT ) kukacha kabisa kwenda kuhudhuria ' Misiba ' ambayo yawezekana hata hao waliokufa 99% walikupigia Kura au pengine hata Wazazi wao walihakikisha leo Wewe uwe hapo ulipo.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Mimi GENTAMYCINE itabidi tu univumilie kwani huwa sina tabia ya kumficha Mtu hata kama ni Rafiki yangu au ni Kipenzi changu na hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyoniumba na sitokuja kubadilika hadi naingia Kaburini na nitasema ukweli pale panapostahili na nitakosoa mara moja kama hivi pale ninapoona pana tatizo kwani sikuumbwa kuwa ' Mnafiki ' kama wengi wanaokuzunguka.

Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli hivi una ' matatizo ' gani na Misiba au Maiti? Mbona Mimi nimeishi miaka mitatu ( 3 ) na ' Wananzengo ' wa Kisukuma kule Nyegezi, Luchelele, Nsumba, Malimbe, Mkolani na Buhongwa lakini tulikuwa ' tunajumuika ' nao sana Misibani na hata Mazishini? Hii picha unayotuonyesha Watanzania sasa unataka tukueleweje Mheshimiwa?

Hukwenda Kagera Watu tukajipinda humu kukutetea labda kwa kuhisi kuwa ungejishtukia na kubadilika ikawa vile vile tukasema ' poa ' mara tena ' Wapiganaji ' wako Askari wa Police waliuwawa ' Kinyama ' mno kule Kibiti kama kawaida hukwenda na kama jadi yetu Wanaume tukaja humu tena ' kutiririka ' kwa kukutetea lakini mioyo yetu inatusuta ila tumeshazoea kujikaza ' kisabuni ' kwa kujua labda moyo wako ungajawa na ' aibu ' na ungabadilika kumbe ndiyo kama vile tulikuwa tunapaka ' Upepo ' rangi.

Sasa kali katika yote Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli hili la juzi tu ' masikini ya Mungu ' Taifa limepoteza Wapendwa wetu kabisa tena wakiwa bado wadogo na wana Ndoto za kuja kuwa Watu fulani wa muhimu katika Taifa hili huku kuna wengine pia huwezi jua walikuwa wanataka kuja kuwa ' watiririkaji ' kama GENTAMYCINE lakini safari yao ikafikia tamati katika Mlima wa Rhotie Marera kwa kufariki dunia pamoja na Walimu wao na Dereva wa lile Basi.

Huku ' watetezi ' wako ' tukisikilizia ' kwa mbali kuona labda safari hii ' mshipa ' wako wa ' aibu ' utakunjuka kwa ' kutukuka ' na utahudhuria Msiba ghafla tunaona Press Release kutoka IKULU ya kutoa rambirambi zako na baadae tena tunatangaziwa kuwa Wewe hutokwenda ila utawakilishwa na Makamu wako wa Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Hatukatai kuwa uwepo wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pale Sheikh Amri Abeid Kaluta ni jambo jema ila nadhani uwepo wake pale ' ungenoga ' kama si ' kupendeza ' mno endapo Wewe Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ungekuwa haupo nchini Tanzania ila kumbe umemtuma Yeye ( Makamu wa Rais ) halafu Wewe ' umeunyuti ' zako tu hapo IKULU ya Magogoni na ratiba zako za hapa na pale.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli leo kwa mara ya Kwanza kabisa naungana na maneno yako unayopenda kuyasema kila mara kuwa nakunukuu " Watanzani mniombee " na yawezekana kumbe sisi Watanzania tukawa hatujui huwa unamaanisha nini ila GENTAMYCINE leo nimegundua kuwa yawezekana unaposema tukuombee labda unataka Watanzania tumwambie Mwenyezi Mungu aweze kuukunjua huo moyo wako mgumu, akujaze upendo uliotukuka na pengine aweze kukuondolea Kisirani chako au Chuki zako au Pepo la ukatili ukatili ambalo labda mwenzetu ' umeshalichungulia ' mahala na ukaona kuwa linakuijia na si ajabu tayari limeshaweka makazi ya kudumu katika roho yako kama siyo moyo wako.

Nimalizie tu kwa kusema kuwa Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli unatupa wakati mgumu sana wa ' kukutetea ' kwa matendo ya ajabu kama pia si ya kustaajabisha unayoyafanya. Hivi kabisa huna hata ' uchungu ' na hawa Watoto? Je ukiachillia mbali Wewe kuwa Rais wetu lakini na Wewe si ni Mzazi pia au? Basi hata ' ungetuzuga ' tu Watanzania kwa kumtuma pia Mkeo Mama yetu Janet Magufuli aandamane na Makamu wa Rais kwenda Arusha lakini hata Yeye pia hajaenda.

Hivi kwa mtindo huu hizi kauli ambazo sasa zinaanza ' kutiririka ' kuwa yawezekana haya matukio labda mwenzetu huwa unayajua kupitia ' African Traditional Science / Ndumbaism ' wakisema kuwa huenda mwenzetu unatoa ' sadaka ' unadhani zitakuwa na mashaka? Hivi na Wewe ungekuwa ' unajichanganya ' Misibani ' umbea ' huu wa sisi ' Waswahili ' kuwa unafanya ' shiriki ' ungeanza kushika kasi na hata kuanza kuaminika na wengi?

Nakuruhusu unichukie kama utapenda au kujisikia kufanya hivyo ILA nakuomba tu haya ambayo huwa nakuandikia uwe unayachukua na kuyafanyia Kazi kwani kwa ' Zawadi ' ya Kipekee kabisa ambayo nimepewa na Mwenyezi Mungu yawezekana Mimi pamoja na Wana JamiiForums wote humu tukawa ni ' Tochi ' yako nzuri ya kukusaidia utuongoze vyema ila bahati mbaya sana mwenzetu hii ' Tochi ' unaichukia na unaidharau sana.

Nawapeni pole zangu za dhati sana Wafiwa wote, Uongozi mzima wa Shule ya Lucky Vicent na Walimu wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wana Arusha wote na Watanzania kwa ujumla kwa Msiba huu mkubwa na mzito sana na kikubwa sote tuungane na tuwaombee maziko na makazi mema huko katika Nyumba zao za Milele hawa Wapendwa wetu. Tuliwapenda ila Mwenyezi Mungu kawapenda zaidi na Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amen.
 
Mbona mwalimu nyerere alikuwa hahudhurii mnataka kuanzisha tabia gani.mwakamu wa rais ndio moja ya kazi zake.
 
Ngoja afanye anachodhani ni sahihi kwa sababu hatuna sheria ya kutaka ulazima wa kwenda. Akienda muwakilishi ni Sawa na yeye kwenda.
Pili sidhani kama ni kweli huwa hapendi maana ameudhulia misiba kadhaa kama aonavyo yeye sio tutakavyo. Leo akisema aende yeye Kila msiba na majanga au Ajali hakuna iliyobora zaidi ya nyingine hivyo basi kwa uzembe huu mabarabarani nusu ya Muda wake utaishia kwenye misiba. Sioni kama suala hilo linauhusiano wowote na kabila la mtu Bali ni utashi na maamuzi ya muhusika. Kuleta hoja za kikabila karne hii ni udhaifu
 
Huenda ni mizimu ilompa urais ulimkatalia kuudhuria misiba ya kitaifa, make haiwezekani hadi rais wa Kenya asikitike na kutoa pole kwa watanzania, wakati Rais wa nchi haishie kumpa gambo pole, utafikiri gambo nae kafiwa, inasikitisha sana, labda kuna siri anaijua kuhusu hii misiba.

Tetemeko bukoba aliishia kuwakejeli wahanga hadi kupelekea kuwadhulumu rambirambi zao, askari hata hakutikisika, na hili aliona gambo ndo kaathirika kuliko hata hawa viongozi wa kesho na familia zao, ni aibu kuwa na kiongozi wa namna hii.
 
Kuhudhuria msiba sio kipimo cha utu!!
wewe mwenyewe uko kwenye keyboard na haujaenda msibani.

Na kwa usahihi kabisa misiba ya waliofariki itafanyika leo na kesho maeneo mbalimbali nchini...unategemea rais atajigawaje?

Ambaye hajawahi kufiwa na mtoto tena wa rika la miaka 12-14 ndio atabaki kuchonga sana.
 
mwacheni huwezi jua amepatwa na nini? ni mtu mzima yule anajua anachokifanya mbona kagera alienda baadaye kusalimia labda ana moyo mwepesi analia zake ndani, kumuona rais analia nje aibu nayo...mwacheni akipata nguvu atakuja kutoa pole.
Acha kumtetea ata kama angelia kuna mtu ambae angemshangaa analia nini......... Tuliekuwa tunamshangaa bashite alilia kanisani baada ya kuambiwa atoe vyeti ila ule ni msiba akilia hakuna wa kumshangaa.
 
Hivi nyinyi watu mbona hamkaukiwi maneno na visa...?
Mh JPM nikuombe baba piga kazi maana kuna msemo wangu
huwa napenda kusema hivi" IF THEY DONT APPRECIATE U'R PRESENCE LET THEM APPRECIATE U'R ABSENCE" . hivyo wewe chapa kazi kwa kwenda mbele
maana wabongo hawaishiwi drama kila siku.
 
K
Si huwa anaenda mingine jamani!! Kule alienda sababu watu walee walikuwepo. Sasa huku akaona akienda na kusema ni sababu ilee aliyoitia moshi itakuwa mbaya.ama nakumbuka vizuri alienda kwenye msiba wa Dr. Didas masaburi.
 
Back
Top Bottom