Mheshimiwa Ngeleja; Sweden kuna kashfa ya nishati yetu

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja leo anawasilisha bajeti ya wizara yake huku kashfa ya nishati yetu ikiwa ni moja ya ajenda ya shirika la Misaada la Kimataifa la Action Aid lenye tawi lake nchini Sweden.

Shirika hili linaishinikiza Serikali ya Sweden kuacha kufadhili kwa kuyapa mitaji ya kuwekeza makampuni yenye kukwepa kodi kama ilivyo kwa kampuni ya Pan African Energy.

Kampuni hii Pan African Energy iliyosajiliwa kwenye visiwa viwili; Mauritius na Jersey inavuna gesi ya Songosongo huku ikiwa imeingia mkataba wa miaka 25 na TANESCO kupitia Shirika la Nishati ina Madini la Taifa TPDC. Ni mkataba wenye kuifanya kampuni hiyo kutokulipa kodi ya faida ya mapato wanayopata kutokana na mauzo ya umeme unaotokana na gesi asilia wanayovuna Songo Songo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu, tangu Pan African Energy waanze kuvuna gesi asilia kule Songo Songo mwaka 2004, kampuni hiyo imevuna faida ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 60. Nusu ya faida hiyo ilipatikana mwaka 2009 na kampuni hiyo ilitarajiwa kuongeza uzalishaji. Hivyo, kuvuna zaidi gesi yetu asilia ya Songosongo.

Mpaka kufikia sasa, Pan African Energy imefanikiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 40. Hiki ni kiasi cha fedha kinachotosha kusomesha watoto wa Kitanzania 175,000 ( Laki moja na sabin ina tano elfu) kwa mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid.

Kwa kifupi tu, ripoti hii inadhihirisha namna ufisadi unavyochangia kutuacha Watanzania tukiwa katika hali ya giza linalotokana na mgawo wa umeme. Tukiwa katika hali ya uzalishaji duni kutokana na uhaba wa nishati ya umeme. Ufisadi umetuletea giza na umasikini.

Kampuni hii ya Pan African Energy inanufaika na ’mkataba wa kifisadi’ usiotanguliza maslahi ya taifa.
Ni wakati sasa wa Waheshimimiwa wabunge wetu ’ kumweka kikaangoni’ Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja ili atoe maelezo ya kina juu ya kashfa hii ya Pan African Energy. Na atwambie, ni hatua gani zitachukuliwa na lini kwa wote waliochangia kutufikisha kwenye kashfa hii. Hivyo basi, waliochangia kutufikisha katika giza hili tunalolishuhudia sasa kwa kukosa nishati hii muhimu kwa maana ya umeme.

Kama Mheshimiwa Waziri atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha, basi, aombwe akae pembeni kupisha Watanzania wengine wenye uwezo wa kushika Wizara hiyo nyeti kwa taifa.

Nawasilisha.

Maggid
Knivsta, Sweden
Ijumaa, Julai 15, 2011
( Unaweza kusoma ripoti ya Action Aid kwenye; Hjälp ett fadderbarn | ActionAid)

Ndugu zangu,

Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja leo anawasilisha bajeti ya wizara yake huku kashfa ya nishati yetu ikiwa ni moja ya ajenda ya shirika la Misaada la Kimataifa la Action Aid lenye tawi lake nchini Sweden.

Shirika hili linaishinikiza Serikali ya Sweden kuacha kufadhili kwa kuyapa mitaji ya kuwekeza makampuni yenye kukwepa kodi kama ilivyo kwa kampuni ya Pan African Energy.

Kampuni hii Pan African Energy iliyosajiliwa kwenye visiwa viwili; Mauritius na Jersey inavuna gesi ya Songosongo huku ikiwa imeingia mkataba wa miaka 25 na TANESCO kupitia Shirika la Nishati ina Madini la Taifa TPDC. Ni mkataba wenye kuifanya kampuni hiyo kutokulipa kodi ya faida ya mapato wanayopata kutokana na mauzo ya umeme unaotokana na gesi asilia wanayovuna Songo Songo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu, tangu Pan African Energy waanze kuvuna gesi asilia kule Songo Songo mwaka 2004, kampuni hiyo imevuna faida ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 60. Nusu ya faida hiyo ilipatikana mwaka 2009 na kampuni hiyo ilitarajiwa kuongeza uzalishaji. Hivyo, kuvuna zaidi gesi yetu asilia ya Songosongo.

Mpaka kufikia sasa, Pan African Energy imefanikiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 40. Hiki ni kiasi cha fedha kinachotosha kusomesha watoto wa Kitanzania 175,000 ( Laki moja na sabin ina tano elfu) kwa mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid.

Kwa kifupi tu, ripoti hii inadhihirisha namna ufisadi unavyochangia kutuacha Watanzania tukiwa katika hali ya giza linalotokana na mgawo wa umeme. Tukiwa katika hali ya uzalishaji duni kutokana na uhaba wa nishati ya umeme. Ufisadi umetuletea giza na umasikini.

Kampuni hii ya Pan African Energy inanufaika na 'mkataba wa kifisadi' usiotanguliza maslahi ya taifa.
Ni wakati sasa wa Waheshimimiwa wabunge wetu ' kumweka kikaangoni' Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja ili atoe maelezo ya kina juu ya kashfa hii ya Pan African Energy. Na atwambie, ni hatua gani zitachukuliwa na lini kwa wote waliochangia kutufikisha kwenye kashfa hii. Hivyo basi, waliochangia kutufikisha katika giza hili tunalolishuhudia sasa kwa kukosa nishati hii muhimu kwa maana ya umeme.

wacha porojo hizo Mjengwa hizo ndiyo hasara za wewe na wana CCM wenzako, kwanini lakini hutaki kuachana na CCM? wanakulipa sana nini?
 
Maggid,

Kwanza hiyo ndio faida ya kuichagua CCM vumilia moshi wa kiwandani upate Ujira. Pili usifikiri Ngeleja hajui Bali tamaa za viongozi na wasaidizi wao ndio zinazopelekea katika upuuzi kama huo. Action Aid wangelichunguza na offshore accounts za viongozi wahusika ndio ungelifahamu CCM ni janga la Taifa.
 
Kunamsemo wa kibantu unasema "Nigo ombuli ukashililaga hibega" (" Mzigo wa miwa wa mpumbavu huishia begani kwake" ) Msemo huu unalenga mfanyabiashara wa miwa ambaye ni mpumbavu, watu(has watoto) wakishajua aliyebeba miwa ni mpumbavu, huwa wanaenda na kuchomoa muwa mmoja mmoja wanaenda zao yeye anabaki kuduwaaa tu mpaka miwa yote inamwishia.

Msemo huu unafanana kabisa na uvunaji wa rasilimali za Tanzania unaoendelea sasa kiholela! Kila mtu ameshajua sisi ni wapumbavu anakuja anaongea na viongozi wapumbavu wanapewa kitu kidogo wanaachia wavunaji wanaendelea!

Huu upumbavu wetu sijui utaisha lini, nadhani mwisho unakaribia lakini tutakuwa tumebakiwa na mali kidogo sana nyingi zitakuwa zimeshaondoka.

Nadhani vizazi vitakavyokuja vitanyonga wazee wao waliohusika na haya!
 
Faida kwenye biashara huwa ina-attract kodi kubwa sana sehemu zote duniani. Nchi maskini huwa zinajitahidi kuvutia mitaji kwa kutoa vivutio mbali mbali faida ikiwa ni mojawapo. Jambo la kusikitisha tu ni kuwa vivutio vya namna hiyo sehemu nyingine duniani haviwekwi kwenye sekta ambazo faida ziko nje nje kama kwenye Madini, Mafuta na Gas kwa sababu maeneo haya yanajulikana kuwa faida huwa ni lazima. Halafu mara nyingi mafuta na madini mengine kama Dhahabu, Almas, Platinum ni maeneo ambayo inajulikana kabisa muwekezaji atakuwepo kwa kipindi kadhaa. Kwa hiyo kuweka vivutio kwenye faida haisaidii chochote kwani madini yakiisha tu muwekezaji hufungasha virago vyake.

Pengine tatizo kubwa zaidi liko kwenye hii sera ya kutoa vivutio kwa wawekezaji. Tujaribu kuwa pragmatic zaidi badala ya ulalamishi usio isha. Pale TIC wana vivutio mbali mbali ambavyo vinatokana na sera yetu ya kuvutia vitega uchumi. Sera hiyo imeandaliwa na nani na inasema nini? Ikiwa sera inaruhusu kuwapa vivutio kama hivyo suluhisho sahihi ni kuipitia sera hiyo upya na kuirekebisha kwanza. Nina uhakika tutaendelea kulizwa katika maeneo mengine kwa sababu tunalalamika tu badala ya kuliangalia tatizo lenyewe.

Of course ku-politicize kila kitu kunafanya iwe ngumu kushughulikia baadhi ya mambo. Ni kweli serikali ya CCM ni problem; lakini bado iko madarakani kwa miaka mingine minne ijayo na inabidi tutafute jinsi ya kuisaidia nchi bila kuleta matatizo. Njia hiyo ni kuainisha maeneo yenye matatizo ili yafanyiwe kazi angalau hata kwa shinikizo.

Hizi sera nyingi unakuta zilidondoshwa tu na watu wa World Bank halafu viongozi wetu wakazipokea kama zilivyo bila kuchambua na kurekebisha kasoro zitokanazo na hao walioleta sera hizo kutoelewa mazingira halisi ya nchi hii. Sera hizo ndiyo zimeruhusu kutolewa kwa vivutio bila kuangalia hali halisi ya nchi! Kwa nchi yenye tax base ndogo kama Tanzania, halafu unatoa vivutio vya kodi kwenye faida katika sekta kama madini na mafuta (amako faida inajulikana lazima ipatikane tena kubwa), unategemea serikali ipate mapato kutoka wapi? Ingetolewa vivutio kwenye sekta endelevu kama kilimo cha kibiashara, sawa, lakini kwenye madini ni big no. Of course tutakimbilia kwenye conclusion kuwa kuna ufisadi ndani yake, lakini maeneo mengine hakuna hata ufisadi bali ubovu wa sera zinazotumika.
 
"Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja leo anawasilisha bajeti ya wizara yake huku kashfa ya nishati yetu ikiwa ni moja ya ajenda ya shirika la Misaada la Kimataifa la Action Aid lenye tawi lake nchini Sweden. Shirika hili linaishinikiza Serikali ya Sweden kuacha kufadhili kwa kuyapa mitaji ya kuwekeza makampuni yenye kukwepa kodi kama ilivyo kwa kampuni ya Pan African Energy.

Kampuni hii Pan African Energy iliyosajiliwa kwenye visiwa viwili; Mauritius na Jersey inavuna gesi ya Songosongo huku ikiwa imeingia mkataba wa miaka 25 na TANESCO kupitia Shirika la Nishati ina Madini la Taifa TPDC. Ni mkataba wenye kuifanya kampuni hiyo kutokulipa kodi ya faida ya mapato wanayopata kutokana na mauzo ya umeme unaotokana na gesi asilia wanayovuna Songo Songo.
.."

Mkuu shukrani kwa taarifa uliyoileta hapa jamvini, hakika inazidi kutuongezea hasira na uelewa juu ya namna Serikali yetu ilivyodhamiria kutufukarisha. Yalisemwa sana ya Rada watu wakaziba masikio sasa tumeambiwa fadha ile ina uwezo wa kununua vitabu milioni 4.4 kwa shule za msingi, vitabu 192,000 kwa walimu wa shule za msingi, nyumba za walimu 1196, na vyoo 200,000 kwenye shule za msingi.

Sasa hii ni fedha ya RADA tu! Kibaya zaidi hakuna siku ambayo serikali iliamua kulivalia njuga suala hilo mpaka tuliposaidiwa na Serikali ya Uingereza kupitia kitengo cha SFO. leo hakuna anayezungumzia Pan African zaidi ya kuliomba Bunge liidhinishe suala la kununua mitambo chakavu! Sijui tunangoja na ACTION AID watusaidie katika hili! Hii nchi inakwenda wapi? Na wabunge wachache hasa wale wa upinzani wanapokuwa firm on issues za namna hii, Unatumika UTATU USIOKUWA MTAKATIFU- (wabunge wa CCM, Kiti cha Speaker, na Serikali). This is pathetic

Ndugu yangu MAJJID, naamini ndani ya CCM kuna watu ambao uzalendo wao na msimamo wao unazingatia maslah ya nchi, ninaimani nawe ni mmoja wao. Kwa kuwa nawe ni sehemu ya CCM, nadhani ungekuwa na mchango mkubwa kama ungeamua kuanza kuwaamsha hawa wabunge wa CCM kwenye vikao vyenu ili waanze kuacha ushabiki na waangalie maslahi ya nchi, na isiwe kwa makala kwani ni imani yangu kuwa hawasomi.

Wakiendelea na Misimamo yao UMMA utaamua cha kufanya
 
Ndugu zangu,

Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja leo anawasilisha bajeti ya wizara yake huku kashfa ya nishati yetu ikiwa ni moja ya ajenda ya shirika la Misaada la Kimataifa la Action Aid lenye tawi lake nchini Sweden.

Shirika hili linaishinikiza Serikali ya Sweden kuacha kufadhili kwa kuyapa mitaji ya kuwekeza makampuni yenye kukwepa kodi kama ilivyo kwa kampuni ya Pan African Energy.

Kampuni hii Pan African Energy iliyosajiliwa kwenye visiwa viwili; Mauritius na Jersey inavuna gesi ya Songosongo huku ikiwa imeingia mkataba wa miaka 25 na TANESCO kupitia Shirika la Nishati ina Madini la Taifa TPDC. Ni mkataba wenye kuifanya kampuni hiyo kutokulipa kodi ya faida ya mapato wanayopata kutokana na mauzo ya umeme unaotokana na gesi asilia wanayovuna Songo Songo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu, tangu Pan African Energy waanze kuvuna gesi asilia kule Songo Songo mwaka 2004, kampuni hiyo imevuna faida ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 60. Nusu ya faida hiyo ilipatikana mwaka 2009 na kampuni hiyo ilitarajiwa kuongeza uzalishaji. Hivyo, kuvuna zaidi gesi yetu asilia ya Songosongo.

Mpaka kufikia sasa, Pan African Energy imefanikiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 40. Hiki ni kiasi cha fedha kinachotosha kusomesha watoto wa Kitanzania 175,000 ( Laki moja na sabin ina tano elfu) kwa mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid.

Kwa kifupi tu, ripoti hii inadhihirisha namna ufisadi unavyochangia kutuacha Watanzania tukiwa katika hali ya giza linalotokana na mgawo wa umeme. Tukiwa katika hali ya uzalishaji duni kutokana na uhaba wa nishati ya umeme. Ufisadi umetuletea giza na umasikini.

Kampuni hii ya Pan African Energy inanufaika na 'mkataba wa kifisadi' usiotanguliza maslahi ya taifa.
Ni wakati sasa wa Waheshimimiwa wabunge wetu ' kumweka kikaangoni' Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja ili atoe maelezo ya kina juu ya kashfa hii ya Pan African Energy. Na atwambie, ni hatua gani zitachukuliwa na lini kwa wote waliochangia kutufikisha kwenye kashfa hii. Hivyo basi, waliochangia kutufikisha katika giza hili tunalolishuhudia sasa kwa kukosa nishati hii muhimu kwa maana ya umeme.

Kama Mheshimiwa Waziri atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha, basi, aombwe akae pembeni kupisha Watanzania wengine wenye uwezo wa kushika Wizara hiyo nyeti kwa taifa.

Nawasilisha.

Maggid
Knivsta, Sweden
Ijumaa, Julai 15, 2011
( Unaweza kusoma ripoti ya Action Aid kwenye; Hjälp ett fadderbarn | ActionAid)

Sina uhakika na hili la ukwepaji wa kodi lakini kitu kimoja nakijua ni kwamba bila ya juhudi za hiyo kampuni ya Pan African Ernergy ya kupandisha uzalishaji wa gesi nchi ingekuwa kwenye giza tororo kwa sasa. Hii kampuni ndio iliyofanya juhudi kuilazimisha Songas ikubali mtambo wa kusafisha gesi wa songosongo uongeze uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya wateja, i.e TANESCO.
Hili la kukwepa kodi kama lipo ni kosa kubwa japo nijuavyo kampuni hii hulipa kodi zake ipasvyo na TPDC ndio wasimamizi wakuu wa hii kampuni.
 
Yaani ufisadi kila mahali mpaka kizungu zungu,ngeleja hana muda wa kutafuta uuvumbuzi,starehe atamwachia nani?
 
siku tutakapo jua kuwa tumemaliza raslimali za nchi hii, ndipo tutakapojua ujinga ni mzigo. Tumekalia haya haya tu.
2m.JPG
 
Sina uhakika na hili la ukwepaji wa kodi lakini kitu kimoja nakijua ni kwamba bila ya juhudi za hiyo kampuni ya Pan African Ernergy ya kupandisha uzalishaji wa gesi nchi ingekuwa kwenye giza tororo kwa sasa. Hii kampuni ndio iliyofanya juhudi kuilazimisha Songas ikubali mtambo wa kusafisha gesi wa songosongo uongeze uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya wateja, i.e TANESCO.
Hili la kukwepa kodi kama lipo ni kosa kubwa japo nijuavyo kampuni hii hulipa kodi zake ipasvyo na TPDC ndio wasimamizi wakuu wa hii kampuni.

Tafadhali sana soma habari nzima uielewe baada ya hapo ndipo uchangie. Utetezi mwingine mnaouleta huwa unatia kinyaa sana!!!! Phew
 
Kaka just now now now, tumetoka kusema huwa hawasomi maelezo hao, jumpin on issues and "naunga mkono asilimia mya"! thats their fate.

Wakati wao wakuikimbia nchi unakaribia!
 
Yanaitaijika mapinduzi ya kweli ya fikra. Tunapaswa kujitambua sisi ni kina nani, tumetoka wapi, tunakwenda pai. nini tunachotakiwa kufanya kwa vizazi vyetu na vijavyo.......

Vinginevyo tutaendelea kutoa kila utajiri wetu kwa hawa jamaa.
 
Sina uhakika na hili la ukwepaji wa kodi lakini kitu kimoja nakijua ni kwamba bila ya juhudi za hiyo kampuni ya Pan African Ernergy ya kupandisha uzalishaji wa gesi nchi ingekuwa kwenye giza tororo kwa sasa. Hii kampuni ndio iliyofanya juhudi kuilazimisha Songas ikubali mtambo wa kusafisha gesi wa songosongo uongeze uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya wateja, i.e TANESCO.
Hili la kukwepa kodi kama lipo ni kosa kubwa japo nijuavyo kampuni hii hulipa kodi zake ipasvyo na TPDC ndio wasimamizi wakuu wa hii kampuni.

Hizi ndiyo pumba pumba pumba kabisa..... tuna safari ndefu.............
 
Acha kutia chumvi bro. Swedish Kroner milioni 65 ni sawa na dola milioni 10 hivi na siyo dola milioni 40.

Svenskt bistånd till skatteparadis

Svenskt bistånd till skatteparadis
Det svenska biståndsorganet Swedfund har investerat svenska biståndspengar i företag som medvetet undviker att betala skatt i Tanzania, där företaget är verksamt.

En studie av ActionAid visar att en av Swedfunds investeringar har resulterat i företaget PanAfrica Energy, som utvinner och säljer fossilgas i Tanzania, och som har fört ut stora skattefria vinster ur landet till skatteparadis. Konsekvensen är att Tanzania inte får in skatt för de vinster landets fossilgas genererar. PanAfrica Energy har undkommit skatter för totalt 65 miljoner i Tanzania sedan 2004. För65 miljoner hade 175 000 flickor kunnat gå i skola i Tanzania. Fallet med PanAfrica Energy är bara en del av ett mycket större problem.

Swedfunds uppdrag är att främja en långsiktigt hållbar utveckling genom att investera i företag i utvecklingsländer. På sin hemsida framhåller Swedfund särskilt att dessa investeringar är viktiga för att de genererar skatteintäkter i länderna.

Regeringen har på flera sätt förändrat förutsättningarna för biståndet. En tydlig inriktning är att kanalisera allt mer bistånd genom näringslivet. Regeringen anser att näringslivet har en viktig roll att spela för att skapa ekonomisk tillväxt och arbetstillfällen samt ge länder större skatteintäkter att bygga grundläggande välfärd för.
 
Les Mer,
Ahsante sana. Uko sahihi. Hapo nilighafirika katika haraka ya kuandika. Badala ya kugawa kwa 6.5 nikazidisha. Sijawahi kupata ' A' ya hisabati shuleni! Poleni kwa usumbufu. All in all, ni fedha nyingi kwa Watanzania na zingeweza kusomesha watoto 175, 000 kwa mwaka mmoja.
Maggid
 
wacha porojo hizo Mjengwa hizo ndiyo hasara za wewe na wana CCM wenzako, kwanini lakini hutaki kuachana na CCM? wanakulipa sana nini?

Ndugu yangu Kiwalanikwagude,

Asante kwa maoni yako.
Fikra zangu umeziita porojo. Ni uhuru wako wa kujieleza. Nami niseme, kuwa maelezo yako ni UONGO mtupu usio na chembe ya ukweli. Labda huoni haya kuandika ya uongo kwa vile umejificha kwenye jina la mtandaoni. Na huna hata chembe ya uthibitisho wowote kwa uandikacho. Ndio maana nauita uzushi na uongo.
Wikiendi Njema.
Maggid
 
Ndugu zangu,

Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja leo anawasilisha bajeti ya wizara yake huku kashfa ya nishati yetu ikiwa ni moja ya ajenda ya shirika la Misaada la Kimataifa la Action Aid lenye tawi lake nchini Sweden.

Shirika hili linaishinikiza Serikali ya Sweden kuacha kufadhili kwa kuyapa mitaji ya kuwekeza makampuni yenye kukwepa kodi kama ilivyo kwa kampuni ya Pan African Energy.

Kampuni hii Pan African Energy iliyosajiliwa kwenye visiwa viwili; Mauritius na Jersey inavuna gesi ya Songosongo huku ikiwa imeingia mkataba wa miaka 25 na TANESCO kupitia Shirika la Nishati ina Madini la Taifa TPDC. Ni mkataba wenye kuifanya kampuni hiyo kutokulipa kodi ya faida ya mapato wanayopata kutokana na mauzo ya umeme unaotokana na gesi asilia wanayovuna Songo Songo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu, tangu Pan African Energy waanze kuvuna gesi asilia kule Songo Songo mwaka 2004, kampuni hiyo imevuna faida ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 60. Nusu ya faida hiyo ilipatikana mwaka 2009 na kampuni hiyo ilitarajiwa kuongeza uzalishaji. Hivyo, kuvuna zaidi gesi yetu asilia ya Songosongo.

Mpaka kufikia sasa, Pan African Energy imefanikiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 40. Hiki ni kiasi cha fedha kinachotosha kusomesha watoto wa Kitanzania 175,000 ( Laki moja na sabin ina tano elfu) kwa mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid.

Kwa kifupi tu, ripoti hii inadhihirisha namna ufisadi unavyochangia kutuacha Watanzania tukiwa katika hali ya giza linalotokana na mgawo wa umeme. Tukiwa katika hali ya uzalishaji duni kutokana na uhaba wa nishati ya umeme. Ufisadi umetuletea giza na umasikini.

Kampuni hii ya Pan African Energy inanufaika na 'mkataba wa kifisadi' usiotanguliza maslahi ya taifa.
Ni wakati sasa wa Waheshimimiwa wabunge wetu ' kumweka kikaangoni' Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja ili atoe maelezo ya kina juu ya kashfa hii ya Pan African Energy. Na atwambie, ni hatua gani zitachukuliwa na lini kwa wote waliochangia kutufikisha kwenye kashfa hii. Hivyo basi, waliochangia kutufikisha katika giza hili tunalolishuhudia sasa kwa kukosa nishati hii muhimu kwa maana ya umeme.

Kama Mheshimiwa Waziri atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha, basi, aombwe akae pembeni kupisha Watanzania wengine wenye uwezo wa kushika Wizara hiyo nyeti kwa taifa.

Nawasilisha.

Maggid
Knivsta, Sweden
Ijumaa, Julai 15, 2011
( Unaweza kusoma ripoti ya Action Aid kwenye; Hjälp ett fadderbarn | ActionAid)

Jamani nipigeni mawe tena!

Hii habari imeandikwa kiubabaishaji sana. TPDC sio shirika la Nishati na Madini! Mkataba huo unoasemwa wa kiifisadi nani aliuona? Kwa nini usiuweke hapa tukauptia?
Mimi sina maslahi yeyote na hiyo kampuni lakini, kitu kimoja najua, Watz wachache sana wanajua uendeshaji wa mafuta na gesi unakuwaje. Kuna standard za industry hii, na nijuavyo TPDC wana the best PSA model ever! Hii yote ni kwamba kwa kuwa kwenye madini tuliliwa, basi imekua hata jani likikugusa utadhani nyoka.
Honestly, bila juhudi za hiyo kampuni kujitahidi kulazimisha kuongeza uzalishaji wa gesi kwa wingi ili mitambo ya TANESCO na SONGAS ipate kuzalisha umeme, nchi ingekuwa kwenye giza tororo mida hii. Hizi facts watu wengi hawazijui, wanakaa kuwa wakali kwa wale ambao tunajaribu kuwaeleza mambo yalivyo. Najua nitashambuliwa na kuitwa kibaraka...lakini mjue signature yangu na nickname yangu zinamaanisha yaliyopo moyoni mwangu.
 
Back
Top Bottom