Mheshimiwa Mbunge wa Arumeru Mashariki ni mgonjwa!

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,926
31,169
Wakuu si jambo jema kumtabiria kifo binadamu mwenzako ila wakati mwingine lazima tuwe realistic kidogo.Mbunge wa Arumeru Mashariki Jeremiah Solomon Sumari wakati wowote anaweza kuungana na ndugu,jamaa na marafiki waliotangulia mbele ya haki.Mheshimiwa Sumari pamoja na kuwa na elimu ndogo sana ya form four aliukwaa unaibu waziri wa fedha kwakuwa mtoto wake kamwoa mtoto wa Laigwanani mkuu Afrika Mashariki Elowasa.Taarifa za uhakika toka kwa ndugu wa karibu Mheshimiwa Sumari hali ya afya yake imezidi kudorora sana.Chama cha Magamba tayari kimeshaanza mchakato wa kumpata mtu wa kurithi mikoba yake.Jimbo la Arumeru Mashariki uenda likawa jimbo la kwanza kufanya uchaguzi muda mfupi ujao.
 
Du...Mkuu, naamini unamaanisha unachoongea!
Kadiri ya mwezi wa January mwaka huu nilipewa habari na jamaa wa karibu sana na familia hizi aishiye huko King'ori, akisema kuwa hali ya huyu mkuu ni mbaya na inakatisha tamaa!...Kwa habari ya kuumwa kwake sina shaka na hilo, lakini tunachomwombea leo hii ni Afya tele!
 
... Taarifa za uhakika toka kwa ndugu wa karibu Mheshimiwa Sumari hali ya afya yake imezidi kudorora sana.Chama cha Magamba tayari kimeshaanza mchakato wa kumpata mtu wa kurithi mikoba yake.Jimbo la Arumeru Mashariki uenda likawa jimbo la kwanza kufanya uchaguzi muda mfupi ujao.
Yaani hawa jamaa ni hatarui sana... wanaacha kushughulikia kumtibia wao wanaanza kjutafuta mtu wa kumrithi... yaani wameshamkatia hukumu ya kifo tayari. Kweli dunia imekwisha
 
Ila alikuwa mtu mzuri sana enz za uwaziri wake hakukumbwa na kashfa za kifisadi tuzidishe maombi wapendwa
 
Yaani hawa jamaa ni hatarui sana... wanaacha kushughulikia kumtibia wao wanaanza kjutafuta mtu wa kumrithi... yaani wameshamkatia hukumu ya kifo tayari. Kweli dunia imekwisha
tuliotoka familiya za kichifu hatushituki kabula chifufu hajafa huandaliwa mapema mlithi vitu kama hivyo nivielelezo tosha tz inaendeswa kichifu baba anaondoka anabadilswa mtoto mjukuu naye anaandaliwa usishangae ni bongo tz
 
huo ni uchuro! Mungu ndio pekee ajuae ni lini avume. Hakuna kisichowezekana mbele ya Mungu. Tuzidi kumwombea
Mtoa mada kanisikitisha sana, ni ubinadamu kuwapa moyo ndugu na jamaa zake ili wawe na subra na uvumilivu wakati huu mgumu.
Tabia ya kufikiria kugawana vya mgonjwa kabla hajafa si ya kiafrika.
 
Chadema tulilikosakosa jimbo lile sasa nafasi nyingine maana alitangazwa mshindi ni wa chadema gafla wakabadili...
 
Mtoa mada kanisikitisha sana, ni ubinadamu kuwapa moyo ndugu na jamaa zake ili wawe na subra na uvumilivu wakati huu mgumu.
Tabia ya kufikiria kugawana vya mgonjwa kabla hajafa si ya kiafrika.
vipo sana na kama havipo basi vimeanza...lol
 
Mungu amrejeshee afya yake ili aungane nasi kwenye majukumu ya ujenzi wa Taifa letu
 
Kama bwana Yesu alimfufua Lazaro aliyekuwa amekufa kwa siku tatu, naamini ataweza kumponyesha Mh.Sumari. Kwa mungu hakuna kinachoshindikana. Hakuna anayejua siku wala saa ya yeye au mtu mwingine kufa.
 
Angekuwa babako ungetoa mada kishabiki hivi? Acha uchawi wewe. Nakuambia unaweza kupigwa na mshangao pale utakapojikuta unatangulia akhera kabla ya huyo Sumari. Mambo ya kishabiki kamwe hayachanganywi na utu, Mungu hapendi huu ujinga MITHALI 5:32. Bush pamoja na chuki yake kwa Osama lakini alimtumia salamu za rambirambi aliposikia kifo chake.
 
Back
Top Bottom