Mheshimiwa Mbunge wa Arumeru Mashariki ni mgonjwa!

Angekuwa babako ungetoa mada kishabiki hivi? Acha uchawi wewe. Nakuambia unaweza kupigwa na mshangao pale utakapojikuta unatangulia akhera kabla ya huyo Sumari. Mambo ya kishabiki kamwe hayachanganywi na utu, Mungu hapendi huu ujinga MITHALI 5:32. Bush pamoja na chuki yake kwa Osama lakini alimtumia salamu za rambirambi aliposikia kifo chake.
Kuna magojwa hata hospitalini wana kukataa wanasema mrudisheni nyumbani maana yake ukafie nyumbani...hivyo usiwe mkali mkuu kama gonjwa lake ni kati ya hayo basi acha watu wajidai akina Yahaya Jr...Pole mkuu
 
kama anaumwa sana angeachia kitu maana hiyo nayo ni stress na kuongeza matatizo kifya

maana kwa jinsi nilivyosoma ni kama anaumwa kwa muda mrefu sasa
 
Dah mnanichekesha kwa hiyo Kamanda SLAA ni emergency kwa nafasi ya ubunge mahali popote Tz.mpinzani wake alikuwa nani kwani?
 
Wakuu si jambo jema kumtabiria kifo binadamu mwenzako ila wakati mwingine lazima tuwe realistic kidogo.Mbunge wa Arumeru Mashariki Jeremiah Solomon Sumari wakati wowote anaweza kuungana na ndugu,jamaa na marafiki waliotangulia mbele ya haki.Mheshimiwa Sumari pamoja na kuwa na elimundogo sana ya form four aliukwaa unaibu waziri wa fedha kwakuwa mtoto wake kamwoa mtoto wa Laigwanani mkuu Afrika Mashariki Elowasa.

Taarifa za uhakika toka kwa ndugu wa karibu Mheshimiwa Sumari hali ya afya yake imezidi kudorora sana.Chama cha Magamba tayari kimeshaanza mchakato wa kumpata mtu wa kurithi mikoba yake.Jimbo la Arumeru Mashariki uenda likawa jimbo la kwanza kufanya uchaguzi muda mfupi ujao.

Na wewe ndugu yangu uwe unaweka janvini mambo yanayoeleweka. Acha masuala ya unazi wa kisiasa linapokuja suala la kuishi au kifo. Aliyekuambia kuumwa sana mara zote kunapelekea kifo ni nani? Kwani haujawaona au kusikia watu wamelazwa ICU kwa siku kibao, na bado wakapona na wale ambao hawakugusa ICU wakaishia kufariki?

Anaweza kupona kwa mkono wa Mungu, na kama Mungu wako unayemwabudu ni yule ambaye hawezi kurejesha uhai na afya ndani ya mtu usituletee emotions zako hapa janvini. Kwamba CCM wameanza kuandaa mtu wa kumrithi ni njia tu ya siasa za maji taka! Acha upuuzi huu kutaka kutusadikisha kwa CCM wamefikia hatua hiyo kwamba mtu anapoumwa tu kwa muda mrefu tayari wanaanza kutafuta re-placement!

Kwa taarifa yako, hata kama unajiona umejaa misuri na kifua chako na unaafya njema sana wakati huu, unaweza kufariki hata ndani ya sekunde chache baada ya kusoma ujumbe huu. Sikuombei ufe sasa, lakini uwe makini unapoandika jambo kwa vile linakufunua jinsi gani ulivyo mweupe moyoni mwako.

Tazama maisha ya mwanadamu yalivyoainishwa ktk Biblia Takatifu:

a.Ni kama majani yapendezayo na mara jua kali likipiga hutoweka mara, (Zaburi 90:5, 6; Yakobo. 1:10; 1 Petro 1:24).

b.Ni kama mvuke, (Yakobo. 4:14).

c.Ni kama pumzi moja, (Ayubu 7:7).

d.Ni kama moshi upoteleao angani, (Zaburi 102:3).
 
Pole kwa mheshimiwa Silili chami japo ni gamba ila huwa simwombei kifo binadamu yeyote. katika human rights article namba 1 & 2 zinazungumzia haki ya mtu kuishi hata kama ni mbaya namna gani hivyo ndivyo katiba nyingi hasa za nchi za kidemokrasia zinavyoamini na kuainisha ktka katiba zao pia. Binafsi ninakuombea upone na ndugu na jamaa ni lazima wadumu katika sala kuomba urudishiwe afya na siha njema. Mungu akubariki sana
 
Huyu anaitwa Jeremiah Sumari, sasa hizo habari za Sililii Chami sijui umezitoa wapi? Au na yeye unamchuria?
 
Angekuwa babako ungetoa mada kishabiki hivi? Acha uchawi wewe. Nakuambia unaweza kupigwa na mshangao pale utakapojikuta unatangulia akhera kabla ya huyo Sumari. Mambo ya kishabiki kamwe hayachanganywi na utu, Mungu hapendi huu ujinga MITHALI 5:32. Bush pamoja na chuki yake kwa Osama lakini alimtumia salamu za rambirambi aliposikia kifo chake.
MKUU SIJAKUELEWA,BUSH ALIMTUMIA OSAMA SALAM ZA RAMBI RAMBI? anyway NAMTAKIA NH. APONE KWA JINA LA YESU KRISTO.AMEN!
 
Duh! inashitua, kwani anaumwa nn ambacho hawezi kupona?

Wakuu ili kudhibiti the wandering minds zisifike kusikostahili, huyu mkuu niliwahi kusikia alikutwa na brain cancer soon after the 2010 elections.
Mwenyezi mungu ampunguzie maumivu na ampe nafuu Solomon Sumari.
 
Alwatan,

Kama habari hizo ni za kweli namwombea Mheshimiwa apone haraka. Pia pole kwa familia kwa kuuguza especially watoto wake. Wito kwa wanabodi, ni lazima ifike sehemu tuweke tofauti zetu za siasa pembeni na tujali uanadamu wa mtu...
 
Jamani ubinadamu wetu tumeuweka wapi? Hata kama tunachukia Chama au siasa zake na vipi kuhusu yeye binafsi kama binadamu? TUUNGANE KUMWOMBEA APATE AFYA NJEMA NA AREJEE KAZINI KUIJENGA NCHI YAKE!
Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu nimeomba, Amen!
 
Pole mh.sumari! Najua utapata nafuu. Nakuomba kama waweza jiuzulu ubunge upunguze tension ya ubongo.
 
Aaaaaah!! Hivi haiwezekani kuanzisha thredi ya wagonjwa wawe wanajadiliwa huko bana!!!!! Hapa tunataka siasa, tena siasa safi. Mapenzi ya Mungu yatimie lakini....
 
Back
Top Bottom