Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

Huyu hafai kabisa, ana hasira isio na mpango, ni mtenda kazi mzuri lakini gazabu zake ndo zinamponza, ameitia hasara ya mabilioni serikali kwa haraka zake za kwenda kuvunja mali ya mdosi mwanza, sasa serikali ndo inalipa. Huyu apewe waziri mkuu lakini uraisi hauwezi huyu. kwa upande mwingine ni mwanakijiji na Jina POMBE ni noma sana.
 
Lakini ukikompea na huyu mzee wa kukena basi bora hata pombe.
 
Majumuisho ya haraka haraka, nagundua haya yafuatayo:
Wachangiaji wote wanakubali kwamba JPM ni kifaa cha kazi nzuri. Reservations ni:
  1. Mmoja kasema anafaa isipokuwa tatizo ni msukuma (sio mkara kama Ng'walimu alivyosema)
  2. Mwingine kasema ni dictator (sio wote wanaafiki hilo)
  3. Ana hasira (sasa amchekee mharibifu?)
  4. Mbabe na hoja ya nguvu (Wabongo wanapenda kubembelezwa - inalipa hiyo?)
  5. Jina lake la Pombe ni nuksi (Hivi unajua maana ya jina lako? Labda ni nuksi zaidi?) Mbona Mkapa mlisema kaleta ukapa kwa sababu ya jina lake?
  6. Anafaa uwaziri mkuu (Wangi wanakubali kama alternative safi - Lakini wakati Obama anaambiwa apewe unaibu Rais alisema yeye hagombei unaibu ila urais ili atumike vema)
Mmh! Haya endelea

Leka
 
I would like to suggest to the President that it high time that Dr. John Pombe Magufuli is transferred to the Ministry of Education to put to rest the following nagging issues at the ministry in question:

- Exam likages at NECTA
- Primary schools massive failures in mathematics and English language
- Holders of fake bachelor, masters degrees and PhDs
- Genuine unpaid teachers' allowances and salaries
- unfinished ward secondary schools buildings
- re-introduction of adult education in rural areas
 
Tatizo letu Tanzania ni la kimfumo zaidi kuliko kiongozi mmoja mmoja. Tuna mfumo ambao hauna vidhibiti mwendo kwa kiongozi mkuu kabisa wa nchi na wateule wake hasa pale wanapoamua kushirikiana kuifilisi nchi. .

Mkuu hapo ndipo nasisimama huu mfumo (system) ndo unatutafuna taratibu.
 
Pinda ni bora mara mia kuliko Pombe. Bahati mbaya sana Pombe tunafahamiana kiasi cha kutosha. Hatufai kwa ngazi ya Urais.

kwa nini usiseme kwa nini unaona Pinda ni bora kuliko Magufuli? na nai anayefaa kwa urais ukiacha Pinda na Magufulli

Nimepata sana shida kusoma post yako imebidi niulize kulingana na post yako

Pinda unayemsema ni huyu waziri mkuu wa sasa wa Tanzania? au kuna mwingine
 
Kama tungekuwa tunachagua mtu kwa maslahi ya taifa na si ushabiki wa kundi fulani, Katika walishika madaraka makubwa kama uwaziri Magufuli anafaa kuwa rais kwa maslahi ya nchi na watanzania

Mkuu Kicheruka.
Ninakuunga mkono kwa 100%
 
wanaomkataa Magufuli hawana sababu ya msingi, ila ni ule kutukuza utanzania haswaa!
 
Toeni sababu za msingi za kumpigia debe zaidi ya uchapa kazi. Nini hasa alichofanikisha katika uongozi wake kinachowapa imani.

Amandla.......
 
bora yeye with outhoritarian character but honest kuliko kuwa na lowassa ambaye ni dictator plus mwizi! unaju tatizo la zile nyumba ilikuwa utekelezaji wako ufisadi ulijipenyeza lakini nia ilikuwa nzuri yaani kujenga mpya sasa alivyokuja huyu wa kubembea mpango ukafa
 
The Champ is good...kwa kweli...ila sasa huwa anakimbia mpaka anapitiliza home..Ila I hope akipata uwaziri mkuu atafanya vizuri zaidi badala ya urais....
..Buswelu huyu jamaa ni kweli akiwa ndio mkuu wa kaya kiukweli kabisa huu ujinga ambao muugwana anaufumbia macho lazima atafanya kweli. Hayo masuala ya kukimbia sana mpaka anapitiliza home ni mambo yanarekebishika kabisa.Mbona hata muungwana alipokuja kwa mara ya kwanza alikuwa namna gani vipi?? I really support JPM kuwa mkuu wa kaya. Hawa wengine wote ni wajasiriamali tu!!!
 
Pinda mbabaishaji, kila siku anang'ang'ania viwanja vya Nyamagana km vile hajui sheria! wamemlisha bumba!
 
Toeni sababu za msingi za kumpigia debe zaidi ya uchapa kazi. Nini hasa alichofanikisha katika uongozi wake kinachowapa imani.

Amandla.......

TZ hatuangalii hayo. Kama ingekuwa hivyo basi marais waliotangulia including this one wasingekuwa marais. Ushaambiwa huko TZ bora rais na si rais bora.

TZ tuna vigezo vyetu, kama huyu mwenzetu (AHM), tunamtaka kiongozi Msafi (BWM), kiongozi anauzika (JMK). This is not Europe or America, this is TZ bwana!!!!!

Safari hii tunamtaka "mchapa kazi" period!!
 
Toeni sababu za msingi za kumpigia debe zaidi ya uchapa kazi. Nini hasa alichofanikisha katika uongozi wake kinachowapa imani.

Amandla.......
background ya jkikwete na Pmagufuli ni nani kafanya mambo makubwa tanzania na tumeyashuhudia.
Bora Magufuli,mafuli for presidency
 
Tufafanulie kuwa "msukuma" kuna dosari gani, ni vyema wana JF tukaelewa sababu ya kimsingi!

Kwani huyu bwana ni Msukuma??? I doubt!!!!!!! Nafikiri jamaa kakosea kwa vile alikuwa headmaster sengerema kwa muda mrefu!!!!!!
 
Mbona mnashindwa kutoa sababu? Kama ni ufanya kazi tu mbona Lowassa alikuwa ni mchapa kazi asiye mfano? Toeni sababu na mafanikio ya huyu bwana!

Siasa za ushabiki ndizo zilizotufikisha hapa. Kama mnataka kuziendelea basi msimlalamikie mliemchagua kwa kishindo!


Amandla.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…