Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lekanjobe Kubinika, Dec 23, 2009.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwenzenu napata taabu kidogo, sijui jinsi gani Mheshimiwa huyu ashawishiwe na kukubali ombi hili. Natamani sana John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama sio sasa kwa sababu za taratibu za CCM, basi zamu inayofuata.

  Vyovyote iwavyo, naamini huyu bwana anafaa kila kona uwanjani anapocheza siasa. Hata PhD aliyoipata majuzi inaongezea chachandu tu, kwamba hatababaishwa na vyeti vya udaktari wa kupewa zawadi tu, maana anayo real one.

  Sina uhusiano naye kabisa huyu mtu na wala sijawahi kukaa naye au kuonana karibu, lakini vitu vyake mwisho bwana. Naamini atachagua timu ya washauri inayofanana naye. Hata kama anayo mapungu yake kama binadamu, the good outways the bad, wakati mwingine analazimika kufanya vitu vingine kwa kuwatii wakubwa zake, lakini akishika rungu mwenyewe nashawishika (sidanganyiki) kwamba ataifaa Tanzania ya sasa.

  Leka
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  utasababisha jk abadilishe hata baraza la mawaziri ili amtoe. Nyamaza, let time solve and bring him to power. You know everyone loves Pombe because the old chap is a realist not idealist.
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  na-kusupport 10,000% i.e 1000 times! We need him if not people of his caliber! He has an iron fist plus heart to mould this nation to higher heights!
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sikio la kufa......

  Amandla..........
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bro, tuko pamoja...Lau kama watanzania wote wangekuwa na akili kama zako na zangu, wangestusupport!....Namwelewa sana JPM, na anafaa sana kwa nafasi hiyo, na ana uchungu na nchi hii!..Mungu Ibariki Tanzania!
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tatizo lake ni MSUKUMA!
   
 7. T

  Tata JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2009
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Najua JPM ni mchapakazi mzuri zaidi ya mawaziri wengine wengi kama siyo wote, ni mfuatiliaji mzuri wa watu wa chini yake, ana uwezo wa kujieleza, kujenga hoja na kizisimamia hata pale hoja hizo zinapokuwa na upinzani wa dhahiri - mfano ni uuzwaji wa nyumba za serikali.

  Tatizo langu na huyu jamaa ni moja tu si msikilizaji mzuri na anaweza kuwa "dictator" mzuri sana hasa pale mitazamo na misimamo yake itakapokuwa kinyume na maslahi ya nchi - refer uuzwaji wa nyumba na ubadilishwaji wa ramani ya barabara kuu kupitia wilayani kwao. Wakati wa uuzwaji wa nyuma za serikali JPM alikuwa na majibu ya kejeli - kama ya bosi wake Mkapa - kwa wale wote waliokuwa wanahoji busara ya zoezi lile. Ni aina ya mtu ambaye anapenda kutumia hoja za nguvu badala ya nguvu ya hoja pale anapokabiliwa na wapinzani makini wanaohoji busara za maamuzi na matamshi yake.

  Tatizo letu Tanzania ni la kimfumo zaidi kuliko kiongozi mmoja mmoja. Tuna mfumo ambao hauna vidhibiti mwendo kwa kiongozi mkuu kabisa wa nchi na wateule wake hasa pale wanapoamua kushirikiana kuifilisi nchi. Ninashawishika kuamini kuwa hata kama utamweka JPM kama mfumo ni huu huu wa kuwa na imperial president hakuna jambo la maana atakalofanya zaidi ya kujitwalia chake mapema. JPM katika mfumo wetu wa sasa hana tofauti na Benjamin William Mkapa.

  Katika mfumo wa sasa nadhani JPM anaweza kuwa mtendaji mzuri akiwa waziri mkuu na apewe mamlaka kamili ya kuwasimamia na kuwawajibisha mawaziri wote.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Msitake kumfanya mkwere abadili baraza la mawaziri.

  All in all, atakuwa better 100 times kuliko muungwana.
   
 9. w

  wasp JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Always I've been impressed by the work done in any Ministry where Dr. John Pombe Magufuli has been a Minister. The guy is focus and wants Tanzania to move ahead. However, his personal hatred towards the opposition political parties makes me sick. Now if he becomes President or PM of the Republic with the swipping state powers in his hands would he not turn into a dictator? I'm yet to be convinced otherwise.
   
 10. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  The Champ is good...kwa kweli...ila sasa huwa anakimbia mpaka anapitiliza home..Ila I hope akipata uwaziri mkuu atafanya vizuri zaidi badala ya urais....
   
 11. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nafikiri kwa jinsi hali ya nchi ilivyo hivi sasa, tunahitaji sana kiongozi ambaye ni dictator, but udictator wa kuwataka watu wafanye kazi, wa kuwakamata na kuwafunga mafisadi na mwingine wa kufanana na huo. Vinginevyo tutabaki masikini hadi kufa. Nchi yetu hivi sasa si ya kuongozwa na Rais anayetabasamu tu hata anapotaka kuadress sensitive issue katika nchi.Tunahitaji mtu wa mabavu, Mkapa aliiweza vizuri nchi kasoro tu alishawishika kuiba. Ile uongozi wake ulikuwa excellent na matokeo yalionekana baada ya muda mfupi.
   
 12. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  If wishes were horses, beggers would be riding! Hata hivyo nakubaliana na mjumbe Tata hapo juu.
   
 13. GY

  GY JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Augustino Lyatonga Mrema alikuwa kama huyu bwana, kasoro tu yeye hakuwa na PHD. Alipoutaka uraisi tu, akaishia hapa alipo leo hii

  Magufuli can better be appreciated for what he has so far done, and should not be honoured for what he can do in the future, bacause that will spoil his excelent perfomance so far!

  I will vote for Pinda, for the honour of Mwalimu!
   
 14. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama tungekuwa tunachagua mtu kwa maslahi ya taifa na si ushabiki wa kundi fulani, Katika walishika madaraka makubwa kama uwaziri Magufuli anafaa kuwa rais kwa maslahi ya nchi na watanzania
   
 15. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  I agree with you beyond reasonable doubt!!!Jamaa ni mkali wa kusimamia sheria no one else!!
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wachina wana usemi; uwe mwangalifu unachoombea maana unaweza kukipata!

  amandla.....
   
 17. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pinda ni bora mara mia kuliko Pombe. Bahati mbaya sana Pombe tunafahamiana kiasi cha kutosha. Hatufai kwa ngazi ya Urais.
   
 18. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #18
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa kwa kweli ni mzuri hasa kwa wakati huu amabo nchi inajiogoza yenyewe, sijui kama kuna Viongozi wa nchi hapa, kama siko sahihi naomba mnielewe nipo sahihi.

  Tanzania ya sasa inataka kiongozi kama magufuli, full dictator wa vitendo na wala siyo kuonea watu, akisema amesema.
   
 19. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JPM ni mtendaji mzuri sana,kama watanzania wangeungana kweli huyu ni kifaa haswa hata umtupe wapi lazima afanye wonder.
  Ube Jk akimaliza tumpe nae tuone wapi atakupeleka,nahisi kama kwenye maziwa na asali????
   
 20. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe ndugu una akili sana.wazo lako ni 100++ naliunga mkono.
   
Loading...