Mhe. Wassira anapokua msemaji wa CHADEMA...

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,888
1,347
“Chadema nao wana makundi na ndiyo maana walitofautiana na marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA)… nao wana matatizo katika uongozi,” alisema Wassira na kuongeza:

“Mbowe, Zitto na hata Dk Slaa nao wana makundi ndiyo maana Zitto alipotangaza kutaka kugombea urais alionywa, tena mmoja ya waliofanya hivyo ni muasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei.”

Wassira alisema hata Shibuda hivi karibuni ameibuka na kuzungumza yake, lakini chama hicho kimeshindwa kumfukuza.
Alisema ndani ya CCM kuna makundi na kwamba, matatizo yanayojadilika huku akijigamba kuwa chama kikubwa kama hicho hakiwezi kukosa matatizo.

Kuhusu siasa za majukwaani, Wassira alisema CHADEMA wanaeneza propaganda ili Watanzania wakiamini chama hicho kuwa kitachukua nchi mwaka 2015.

“Haya ni majigambo tu, mimi ni mzoefu na nimeanza siasa tangu utotoni, hizi ni siasa ambazo unaweza kuzifananisha na uganga wa kienyeji,” alisema Wassira.

Haya ndio mazungumzo ya Mh.wakati wa dk 45 ITV hapa mi najiuliza kwamba huyu jamaa amekua msemaji wa CHADEMA sasa kama ndio hivyo avue gamba nae avae gwanda.

Jiulize kwamba ni kwanini chama ambacho kimeweza kutawala kama sio kuongoza kwa muda wote huo hakiwezi kuongea moja kwa moja mpaka in comparizon to CHADEMA ukianza kufanya mlinganisho wa vyama kama CHADEMA ina maana kwamba CHADEMA tunawatisha na ndio maana lazima watutaje, wajilinganishe na mambo kama hayo na hii M4C ni mwisho wa gamba
 
yule mzee aisee,kwisha habaru yake, nilimsikiliza siku ile yaani hana llolote,ila hali ndo ishakuwa ivyo,inabidi tu wakubali maana hakiuwa hata na cha kueleza kuhusu chama chake,alicheza danadana balaaaaaa,
 
CCM ni chenye wanachama wenye vipaji vingi:walopokaji kama huyo mzee,wanafiki kama Nape mara tumewapa muda wajivue magamba,du hadi wakavaa mengine baraza la mawaziri likabadilishwa,ccm kuna maafisa matusi kama kina Lusinde,kazi kweli kweli.Jambo la kumshukuru Mumgu ni kwamba pia kuna wenye vipaji vizuri kama Magufuli,Mwandosya na Mwakyembe kidooogo! KWA ule msemo wa wengi wape basi WOTE NI MAGAMBA
 
Hivi wassira naye bado ni mtu wa kutiliwa maanani?
Nadhani hata uwezo wake wa kufikiri na kutathmini siasa umekwisha kabisa, kwahiyo akilala ,akiamka anaiona Chadema ikichukua uongozi wa nchi, sasa analazimika kuongea lolote linalomjia kichwani bila kutafakari.

Juzi tu amezomewa sana na wananchi wa jimboni kwake bunda, sasa kwanini asirukwe na akili? hiki kimbunga cha M4C kinawatisha nyinyiem na hivyo wanajikuta wanajiropokea tu bila kujua wanaongea nini.
 
Nasikia kuna kampuni linataka limwajiri kwenye kliniki yao kwaajili ya kunyamazisha watoto pindi wanapolia kwani mtoto akiambiwa mzee wa gombe huyo nyamaza!!!! akimuona lazima anyamaze kutokana na huo msura mzito kama zege
 
Kama huna chakusema kuhusu maisha yako, au familia yako utakuwa unaisemea familia ya jirani au maisha ya mwenzio. Kwetu tunasema usipomsifua mkeo utamsifia mke wa mwenzio.
 
Wenzake wamesha ona impact ya M4c yeye anabenza kuwa naina kitu inawezekana ikawa ni yakurudi nyuma na sii yakuendelea.
 
Mi nilimsikiliza kwa makini nikagundua kuwa CHADEMA wamempagawisha,yaani kila alikuwa akiulizwa swali hata kama halina uhusiano na CHADEMA lazima kwenye jibu agusie CHADEMA, hata angeulizwa tano jumlisha tano ni ngapi angejibu ''kwangu ni kumi lakini kwa CHADEMA ni kumi na moja''CHADEMA msirudi Bunda tena vinginevyo mtamuuwa mzee wa watu.
 
Yupi mkuu, au ndiye huyu hapa?
Tyson.jpg
 
"Chadema nao wana makundi na ndiyo maana walitofautiana na marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA)… nao wana matatizo katika uongozi," alisema Wassira na kuongeza:

"Mbowe, Zitto na hata Dk Slaa nao wana makundi ndiyo maana Zitto alipotangaza kutaka kugombea urais alionywa, tena mmoja ya waliofanya hivyo ni muasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei."

Wassira alisema hata Shibuda hivi karibuni ameibuka na kuzungumza yake, lakini chama hicho kimeshindwa kumfukuza.
Alisema ndani ya CCM kuna makundi na kwamba, matatizo yanayojadilika huku akijigamba kuwa chama kikubwa kama hicho hakiwezi kukosa matatizo.

Kuhusu siasa za majukwaani, Wassira alisema CHADEMA wanaeneza propaganda ili Watanzania wakiamini chama hicho kuwa kitachukua nchi mwaka 2015.

"Haya ni majigambo tu, mimi ni mzoefu na nimeanza siasa tangu utotoni, hizi ni siasa ambazo unaweza kuzifananisha na uganga wa kienyeji," alisema Wassira.

Haya ndio mazungumzo ya Mh.wakati wa dk 45 ITV hapa mi najiuliza kwamba huyu jamaa amekua msemaji wa CHADEMA sasa kama ndio hivyo avue gamba nae avae gwanda.

Jiulize kwamba ni kwanini chama ambacho kimeweza kutawala kama sio kuongoza kwa muda wote huo hakiwezi kuongea moja kwa moja mpaka in comparizon to CHADEMA ukianza kufanya mlinganisho wa vyama kama CHADEMA ina maana kwamba CHADEMA tunawatisha na ndio maana lazima watutaje, wajilinganishe na mambo kama hayo na hii M4C ni mwisho wa gamba

"Mti wenye matunda mengi ndio hupigwa mawe mengi"; Ni CDM pekee inayowalaza macho kwa wakati huu ukizingatia kwamba wengi wao wamegeuza siasa kuwa mradi wa kujikimu kwa njia za ufisadi, wanajua kinachokuja ni watu kuozea jela na chama with the highest possibility kutekeleza jukumu hilo ni CDM pekee.
GOVERNMENT IN WAITING
 
wakubwa!ninakawaida ya kumsikiliza mtu yoyote hata kama kichaa,mlevi nk napenda kumsikiliza tu kwani huwa naamini kwamba ktk maneno yeke 20 basi kuna hata 1 laweza kuwa na point.

Lakini usitegemee mtu kama Wasira,ataongea point toka ananza kuongea hadi anamaliza hata kama angeongea wik nzima mfululizo.Kama kuna mashindano ya kulala kwenye mabunge,vikao,n.k basi mchukue wasira kwani ila kabla hawajafungua mashindano atakua alisha anza kukoloma
 
Mwezi mchanga.
 
Back
Top Bottom