Mhe. Rais,Mkapa na Kikwete nao sasa ni 'vifaa vya kijeshi' kama MV Bagamoyo?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,078
2,000
Tupo kwenye mjadala wa madini. Kichwa cha habari ni MAKINIKIA. Mjadala umepamba moto. Tunakumbushana,tunasemana,tunatajana na kurekebishana. Kwa upana wa kitaifa.

Lakini,Rais na Mawaziri wako wawili wa Sheria na Katiba pamoja na yule wa Habari mmepunguza uwanja. Uwanja wa majadiliano. Mmekataza kutajwa kwa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwenye mjadala.

Nakumbuka kivuko cha MV Bagamoyo nacho kilijadiliwa. Kuhusu ununuzi wake na matumizi yake. Rais ukatufunga mdomo kwa kukikabidhi jeshini. Ukatuambia kuwa sasa kimekuwa kifaa cha kijeshi na ni risk kukijadili. Tukanyamaza

Je,Mzee Mkapa na Mzee Kikwete nao wamekuwa vifaa vya kijeshi na hivyo hawajadiliki? Waliotajwa tuwajadili?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
52,010
2,000
Ni marufuku kumsingizia fisi kuwa kala nyama
cd76ea7759eeaf84ed4c419bf8381010.jpg
 
lukesam

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
10,686
2,000
Najiuliza tu, itakuwa vipi akina Chenge na Karamagi wakisema waliyafanya hayo yote kwa baraka za wenyeviti wao wa baraza la mawaziri?

Kwanini jitihada inayotumika kuwanasua hawa wastaafu ni kubwa kuliko jitihada atakayotumia binadamu kumuweka tembo mabegani mwake?
 
Kipapatiro

JF-Expert Member
May 18, 2017
1,129
2,000
Tupo kwenye mjadala wa madini. Kichwa cha habari ni MAKINIKIA. Mjadala umepamba moto. Tunakumbushana,tunasemana,tunatajana na kurekebishana. Kwa upana wa kitaifa.

Lakini,Rais na Mawaziri wako wawili wa Sheria na Katiba pamoja na yule wa Habari mmepunguza uwanja. Uwanja wa majadiliano. Mmekataza kutajwa kwa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwenye mjadala.

Nakumbuka kivuko cha MV Bagamoyo nacho kilijadiliwa. Kuhusu ununuzi wake na matumizi yake. Rais ukatufunga
Tupo kwenye mjadala wa madini. Kichwa cha habari ni MAKINIKIA. Mjadala umepamba moto. Tunakumbushana,tunasemana,tunatajana na kurekebishana. Kwa upana wa kitaifa.

Lakini,Rais na Mawaziri wako wawili wa Sheria na Katiba pamoja na yule wa Habari mmepunguza uwanja. Uwanja wa majadiliano. Mmekataza kutajwa kwa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwenye mjadala.

Nakumbuka kivuko cha MV Bagamoyo nacho kilijadiliwa. Kuhusu ununuzi wake na matumizi yake. Rais ukatufunga mdomo kwa kukikabidhi jeshini. Ukatuambia kuwa sasa kimekuwa kifaa cha kijeshi na ni risk kukijadili. Tukanyamaza

Je,Mzee Mkapa na Mzee Kikwete nao wamekuwa vifaa vya kijeshi na hivyo hawajadiliki? Waliotajwa tuwajadili?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

kwa kukikabidhi jeshini. Ukatuambia kuwa sasa kimekuwa kifaa cha kijeshi na ni risk kukijadili. Tukanyamaza

Je,Mzee Mkapa na Mzee Kikwete nao wamekuwa vifaa vya kijeshi na hivyo hawajadiliki? Waliotajwa tuwajadili?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Nakutolea bastola kwakuwa umewataja wastaafu.....
 
pepsin

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
3,371
2,000
Magufuli anajishushia tu heshima yake.Mnafungia gazeti kwa sababu limemtuhumu Mkapa na Kikwete kwa wizi? Magufuli is not serious at all! This is "it cant be!!"
Kwani kamati za rais ndio zimechimbua kila kitu? Kwamba hamna other source of information nje ya hizo kamati mbili?
MATUMANI HEWA SAWA NA MAISHA BORA HEWA KWA KILA MTANZANIA
 
WilliK10

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
601
500
Tupo kwenye mjadala wa madini. Kichwa cha habari ni MAKINIKIA. Mjadala umepamba moto. Tunakumbushana,tunasemana,tunatajana na kurekebishana. Kwa upana wa kitaifa.

Lakini,Rais na Mawaziri wako wawili wa Sheria na Katiba pamoja na yule wa Habari mmepunguza uwanja. Uwanja wa majadiliano. Mmekataza kutajwa kwa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwenye mjadala.

Nakumbuka kivuko cha MV Bagamoyo nacho kilijadiliwa. Kuhusu ununuzi wake na matumizi yake. Rais ukatufunga mdomo kwa kukikabidhi jeshini. Ukatuambia kuwa sasa kimekuwa kifaa cha kijeshi na ni risk kukijadili. Tukanyamaza

Je,Mzee Mkapa na Mzee Kikwete nao wamekuwa vifaa vya kijeshi na hivyo hawajadiliki? Waliotajwa tuwajadili?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Wamefanya "mambo makubwa". Na kweli. Haya mambo sio ya kitoto
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
11,063
2,000
Anakiogopa kivuli chake na cha wastaafu!!! Mwanzoni alimsema JK kuwa amefanya mambo ya hovyo (uzinduzi wa Maktaba UDSM) leo amekomaa anawalinda kwa nguvu zote maana yeye pia ana mikono michafu.... nyumba na meli mbovu ya jeshi!! Ahhahahaha
 
Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
2,673
2,000
Ndugu yangu ukitafakari kwa makini utagundua kuwa swala la madini ni la kisiasa na si lakiuchumi. Bw yule wakati akipokea ripoti yapili ya makinikia alizungumza kwa unyonge sana kiasi cha kukaribia kumwaga machozi kiasi kwamba kila mmoja wetu aliguswa kwa hilo. Na kila mmoja wetu aliwanyooshea vidole watangulizi wake. Nakutuasa tushikamane kama taifa ktk hilo. Chakusikitisha ni pale aliposema wahusika wakuu waliotufikisha tulipo wasitajwe. Ametuvunja moyo watz. Watu wakisema na kuamini kuwa may be ilikuwa ni kiki ya kisiasa ya 2020 baada yakuvuruga kila kona yawezekana kukawa nakaukweli. But time will tell.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,514
2,000
Ndugu yangu ukitafakari kwa makini utagundua kuwa swala la madini ni la kisiasa na si lakiuchumi. Bw yule wakati akipokea ripoti yapili ya makinikia alizungumza kwa unyonge sana kiasi cha kukaribia kumwaga machozi kiasi kwamba kila mmoja wetu aliguswa kwa kwa hilo. Na kila mmoja wetu aliwanyooshea vidole watangulizi wake. Nakutuasa tushikamane kama taifa ktk hilo. Chakusikitisha ni pale aliposema wahusika wakuu waliotifikisha tulipo wasitajwe. Ametuvunja moyo watz. Watu wakisema na kuamini kuwa may be ilikuwa ni kiki ya kisiasa ya 2020 baada yakuvuruga kila kona. But time will tell.
Mimi huwaga simuamini bwana yule.
 
Nginana

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
839
1,000
Tupo kwenye mjadala wa madini. Kichwa cha habari ni MAKINIKIA. Mjadala umepamba moto. Tunakumbushana,tunasemana,tunatajana na kurekebishana. Kwa upana wa kitaifa.

Lakini,Rais na Mawaziri wako wawili wa Sheria na Katiba pamoja na yule wa Habari mmepunguza uwanja. Uwanja wa majadiliano. Mmekataza kutajwa kwa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwenye mjadala.

Nakumbuka kivuko cha MV Bagamoyo nacho kilijadiliwa. Kuhusu ununuzi wake na matumizi yake. Rais ukatufunga mdomo kwa kukikabidhi jeshini. Ukatuambia kuwa sasa kimekuwa kifaa cha kijeshi na ni risk kukijadili. Tukanyamaza

Je,Mzee Mkapa na Mzee Kikwete nao wamekuwa vifaa vya kijeshi na hivyo hawajadiliki? Waliotajwa tuwajadili?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Mzee Tupatupa,

Nimekuwa najiuliza kwa nini huu mjadala wa makanikia uanzishwe wakati huu wa bunge la bajeti ilhali ungekuwa ni wakati muafaka kwa wananchi kufuatilia na kufahamu jinsi serikali ilivyotekeleza bajeti ya 2016/17 ili waweze kupima utendaji wake?

Naona hii hadithi ya makanikia imefunika kabisa bunge la bajeti. Je hii imepangwa kiujanja au imetokea tu?

Naona kuna goli la mkono hapa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom