Mhe. Rais,Mkapa na Kikwete nao sasa ni 'vifaa vya kijeshi' kama MV Bagamoyo?

Tupo kwenye mjadala wa madini. Kichwa cha habari ni MAKINIKIA. Mjadala umepamba moto. Tunakumbushana,tunasemana,tunatajana na kurekebishana. Kwa upana wa kitaifa.

Lakini,Rais na Mawaziri wako wawili wa Sheria na Katiba pamoja na yule wa Habari mmepunguza uwanja. Uwanja wa majadiliano. Mmekataza kutajwa kwa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwenye mjadala.

Nakumbuka kivuko cha MV Bagamoyo nacho kilijadiliwa. Kuhusu ununuzi wake na matumizi yake. Rais ukatufunga mdomo kwa kukikabidhi jeshini. Ukatuambia kuwa sasa kimekuwa kifaa cha kijeshi na ni risk kukijadili. Tukanyamaza

Je,Mzee Mkapa na Mzee Kikwete nao wamekuwa vifaa vya kijeshi na hivyo hawajadiliki? Waliotajwa tuwajadili?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Trump pamoja na kuwa yupo madarakani, kila siku anaandamwa na sasa imejulikana anachunguzwa kashfa ya Urusi. Sisi hili la mikataba ambayo imetutia umaskini haturuhusuwi kuwataja tena watu ambao hawapo madarakani. Only in Tanzania. Vyombo vya habari vya Marekani na nje vingekuwa Tanzania vingekuwa vimefungiwa vyote ingekuwa ni Cartoon network tu basi. Angalia May ambaye serikali yake inatoa misaada hapa anavyoandamwa. Sisi omba omba watu wetu waliokomba tulichopewa msaada, hawaruhusiwi kutajwa. cc Rada na mzee wa vijisenti.
 
Tunatakiwa kupigana na UJINGA HUU wa hawa watu wa CCM . .

Kokosekana kwa Uhuru wa habari ni hatari kwa usalama wa nchi yetu . . Viongozi wote walioshiriki ktk kashfa hizi wanastahili kusikilizwa kwa HAKI . . , tusiwaonee wadogo na kuacha wakubwa wakiendelea kula pesa za wizi .

Chenge na Mwanyika walifanya kazi walizotumwa na wakubwa wao chini ya kiapo na sheria zilizotungwa, tena kwa HATI YA DHARURA na Bunge la CCM . .
Hata JPM wakati huo alikuwa Mbunge wa CCM . .
 
...Mkuu,angetupa list/majina ya wengine ambao haturuhusiwi kuwataja katika hii vita ya Makinikia..maana mimi naona hata Shein nae anahusika
 
Back
Top Bottom